wastaafu wa eac wavamia ikulu, kandoro awapoza
".....bwa'mdogo chunga sana....ohoooo." anaonekana kusema mstaafu mmoja akimwambia askari kanzu baada ya wastaafu hao wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki kuandamana hadi geti kuu la ikulu kudai mafao yaowastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki wakiwa wamekaa nje ya lango kuu la ikulu kudai mafao yao jioni hii. hata hivyo mkuu wa mkoa wa dar abbas kandoro alifanikiwa kuwashawishi wastaafu hao kutumia busara na njia za kiungwana kudai mafao yao. waliondoka wakiwa wameridhika baada ya kuahidiwa kuwa malalamiko yao yatafikishwa pahala pake
baadhi ya mabango waliyobeba wastaafu hao
".....asante mwanangu, virungu si suluhu pekee ya matatizo", anaambiwa kamanda selemani kova baada ya wastaafu kutumia busara na kukubali ombi la mkuu wa mkoa abbas kandoro kwamba watafute ufumbuzi kwa njia ya amani
wastaafu wakimpongeza mkuu wa mkoa abbas kandoro kwa kuahidi kusikiliza kilio chao na kukipeleka pahala pake
mkuu wa mkoa wa dar abbas kandoro (mikono kifuani) mkuu wa wilaya ya ilala patrick tsere (shoto) mkuu wa kanda maalum ya polisi ya dar selemani kova (tatu shoto) na maafande wakiwasikiliza wastaafu
mmoja wa viongozi wa wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki akiwashauri wenzie wasikie ombi la mkuu wa mkoa wa dar abbas kandoro kuwataka watafute ufumbuzi kwa busara na amani
mkuu wa mkoa mh. abbas kandoro akiwasili na mkuu wa wilaya ya ilala mh. patrick tsere
No comments:
Post a Comment