Tuesday, September 16, 2008

Tumeunda Kamati Kutafuta
Viongozi anaotaka Kukihujumu
Chama-Dr Slaa...
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk.Wilbrod Slaa akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Dar es Salaam jumamosi.Kulia ni Balozi Christopher Ngaiza.Picha na Mdau Bernard Rwebangira
-----------
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeunda Kamati Ndogo kwa ajili ya kuchunguza viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kukihujumu,imefahamika.Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Wilbroad Slaa alisema hayo jumamosi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tamko la Kamati Kuu ya chama hicho baada ya mkutano wake uliofanyika hivi karibuni.
Dk.Slaa alisema kwa muda sasa kumekuwa na mikakati inayofanywa na baadhi ya watu ndani na nje ya chama hicho kwa lengo la kuhujumu taswira ya chama hicho na Mwenyekiti wake wa Taifa,Freeman Mbowe.Alisema hujuma hizo ndani ya chama zimekuwa zikihusisha baadhi ya viongozi wa chama hicho katika maeneo mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji kwa umma.Bofya na Endelea....>>>>>>>>>

No comments: