HII YA ZENJI KALI
Sakata la Mafuta Zanzibar'Hata yakiwa kidogo, mafuta ni yetu
tutagawana na mengine kujipaka'
WAWAKILISHI wa Zanzibar wamesema, "hata kama ujazo wa mafuta yanayoweza kupatikana Zanzibar ni sawa na glasi ndogo ya kupimia pombe (kinibu), mafuta hayo ni mali ya Wazanzibari, watagawana ili watakaoweza wajipake mwilini."
Kauli hiyo ilitolewa jana baada ya mshauri mwelelezi, David Reading, kueleza kuwa mafuta yanayowezekana kupatikana kisiwani humo ni kidogo na kupatikana kwake ni kwa gharama kubwa.
Mtaalamu huyo kutoka Uingereza aliitwa kwa ajili ya kuishauri Serikali ya Mapinduzi (SMZ) na Serikali ya Muungano, namna bora ya kugawana rasilimali itokanayo na gesi na mafuta.
Kauli hiyo ya Reading pia imesababisha wawakilishi kuingiwa na chuki dhidi ya Wazanzibari walio kwenye Serikali ya Muungano, wakiwaita kuwa ni vigeugeu mithili ya vinyonga na wasiojali masilahi ya Wazanzibari.
Akitoa maoni yake kuhusu suala la mafuta na gesi asilia kwa mshauri huyo mwelekezi, mwakilishi kutoka Chama cha Wananchi (CUF), Najma Khalfan Juma, alisema kuwa hata kama mafuta ya Zanzibar yatakuwa madogo kiasi cha ujazo wa glasi ndogo ya kupimia pombe ya haramu ya gongo (kinibu), Wazanzibari watagawana hata ikiwa kwa ajili ya kujipaka mwilini.
"Hata kama watajipaka mwilini au wengine watatumia kama dawa ya kuchulia misuli, itakuwa bora zaidi kuliko suala la mafuta kuwa la Muungano," alisema.
No comments:
Post a Comment