Thursday, December 31, 2009

TAARIFA KWA UMMA TOKA BENKI KUU
MAKAZI YA GAVANA WA BENKI KUU

TAARIFA KUHUSU UJENZI WA MAKAZI YA VIONGOZI WAKUU WA BENKI KUU YA TANZANIA

GAVANA WA Benki Kuu na manaibu wake kwa mujibu wa mikataba ya kazi zao, wanastahili kupewa nyumba ya kuishi kila mmoja. Hapo awali Gavana alikuwa anaishi Barabara ya Mahando kiwanja namba 387Masaki na Naibu Gavana Barabara ya Msese kiwanja Namba 43.

Awali Benki Kuu ilikuwa na viongozi wakuu wawili, Gavana na Naibu wake mmoja. Baada ya mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2006, Benki Kuu ina viongozi wakuu wanne; Gavana na Manaibu wake watatu. Kila mmoja wao, kwa mikataba iliyowekwa anastahili kupata nyumba ya kuishi.

Mwaka 2006, kabla ya uteuzi wa viongozi wa sasa wa juu, Benki Kuu ilifanya uamuzi wa kujenga nyumba mbili zaidi kwa makazi ya viongozi walioongezeka. Iliamuliwa nyumba hizi zijengwe kiwanja namba 57 Barabara ya Mtwara Crescent na kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe maeneo ya Oysterbay.Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned).

Timu ya wataalamu waelekezi ikiongozwa na M/S SKY Architects Consultants iliajiriwa kutengeneza michoro na ramani za nyumba hizo. Michoro miwili ilichaguliwa, moja kwa kila nyumba ili wataalamu hao watengeneze ramani kamili ya ujenzi. Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba. Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.

Huduma zilizogharimiwa katika ujenzi wa nyumba hizi ni pamoja na mashine ya umeme (generator), mashine ya kupoza hewa na matenki ya kuhifadhi maji. Wakati huohuo, shughuli zingine zilizofanyika ilikuwa ni kutengeneza mahali pa kuegesha magari pamoja na bustani.

Wataalamu hawa baada ya uchoraji huu walifanya tathmini ya vifaa vinavyohitajika na maelekezo kwa wazabuni ili itumike kualika zabuni. Taratibu zote za manunuzi zilifuata sheria ya manunuzi katika kuwaalika wazabuni na kuteua wakandarasi. Kila nyumba ilikuwa ni mradi unaojitegemea na kila moja ilifanyiwa zabuni peke yake.

Izingatiwe kuwa ujenzi wa nyumba hizi ulipangwa na kuamuliwa kabla ya uteuzi wa Profesa Benno Ndulu kujiunga na Benki Kuu Septemba 2007.

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008.Wakandarasi wote wa daraja la pili au la juu zaidi walialikwa kuwasilisha zabuni na walitakiwa kulipa ada ya shilingi 50,000. Wakandarasi 12 walituma maombi na kuchukua hati za zabuni.Lakini kati ya hao 10, waliwasilisha maombi yao kabla ya kufikia tamati ya kupokelewa maombi hayo Machi 25,2008.

Zabuni hizi zilifunguliwa na Bodi ya Zabuni ya Benki Kuu na kufanyiwa tathimini ikishirikisha mtaalamu mwelekezi wa mradi huo na Idara ya Miliki ya Benki Kuu. Mapendekezo kutoka kwa wakandarasi yalikuwa na viwango vya gharama kuanzia Shilingi 1,399,184,549.00 hadi shilingi 1,847,763,537.00 kwa kiwango cha juu. Baada ya tathmini ya zabuni hizo na kufanya masahihisho ya tarakimu zilizowasilishwa, mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited. Gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26.

Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja. Mkandarasi huyu aliteuliwa na Bodi Zabuni (DSM) ya Benki Kuu ikaridhia kuwa M/S Remco (International) Limited ishughulikie maswala aya vipoza hewa; M/s Ginde EAP Services Ltd ishughulikie maswala ya maji safi, mabomba na maji taka na M/s Pomy Engineering Co.Ltd ishughulikie maswala ya umeme. Makampuni yote hayo yamesajiliwa Tanzania.

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo wa ushindani wakianza na wakandarasi watano (5) ambao waliwasilisha maombi yao na kuishia na uteuzi wa M/s Holtan Builders Ltd ambayo gharama yake ya Shilingi 1,272,348,512.00 (fixed price) ilikuwa ni ya chini kuwashinda wengine na makubaliano ya kukamilisha ujenzi katika muda wa wiki 24. Mkandarasi huyo alitumia kampuni zifuatazo kwa shughuli zingine: M/s Jandu Construction & Plumbers Ltd kwa shughuli za mabomba, maji safi, na maji taka, M/s Barkley Electrical Contractors Ltd kwa maswala ya umeme na M/s Remco (International) Ltd kwa shughuli za vipoza hewa. Mkandarasi ndiye mlipaji wa gharama za shughuli hizi zote zinalipiwa kutokana na gharama ileile iliyokubalika kwa mkandarasi mkuu.

Watendaji wote wa miradi hii wanaonyeshwa kwenye mabango ambayo bado yapo kwenye viwanja hivyo. Uteuzi wa Gavana Ndulu, Manaibu Gavana, Dkt. Enos Bukuku na Bw.Lila Mkila ulifanyika wakati mipango ya awali ya kujenga nyumba hizi

ilikuwa imeshaanza. Benki Kuu ilikodisha nyumba mbili, mojakiwanja namba 480 Barabara ya Bray, Masaki na nyingine kiwanja namba 591,Msasani Peninsular kwa matumizi ya viongozi hao wawili ambao walikuwa bado wanaishi kwenye nyumba zao mbali na ofisi.

Kati ya Oktoba 2007 aliporipoti kazini kama Naibu Gavana hadi Aprili 2008, Profesa Ndulu aliishi kwenye nyumba yake iliyoko Mbezi Beach, na Naibu Gavana Mkila naye pia aliishi nyumbani kwake kabla ya kuhamia kwenye nyumba hizi zilizokodishwa.

Benki Kuu iliamua kumhamisha Naibu Gavana Juma Reli kwenda Barabara ya Mahando Masaki ili kuruhusu matengenezo ya nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni Barabara ya Msese. Naibu Gavana Dkt.Bukuku anaishi kwenye nyumba yake na Benki Kuu inatoa posho ya nyumba kulingana na mkataba.

Nyumba hizo mbili zilizojengwa chini ya miradi iliyotajwa, sasa hivi zimekamilika.Gavana wa Benki Kuu, Profesa Ndulu alihamia nyumba namba 12 Barabara ya Tumbawe Desemba 17,2009 na Naibu Gavana Mkila alihamia nyumba namba 57 Mtwara Crescent Desemba 4,2009

Kama ilivyo kiutaratibu, ukaguzi wa mahesabu yanayohusu miradi hiyo utafanyika kisheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ndiye mkaguzi wa mahesabu ya Benki Kuu; ambaye ameanza kufanya kazi hii tangu mwaka 2007. Yeye ameiteua kampuni ya Ernst & Young kama wakaguzi wa kumsaidia kutekeleza jukumu hili.

IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA UMMA NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA
SEPTEMBA 30, 2009
BOT GOVERNOR'S OFFICIAL RESIDENCE
CONSTRUCTION OF THE BANK OF TANZANIA EXECUTIVE RESIDENCES

Bank of Tanzania Executive officers are entitled to official residence provided by the Bank. Initially the Bank used to have only two executive officers, the Governor and one Deputy Governor. The Governor was living at BOT house No. 387 Mahando Street and Deputy Governor at BOT house No. 43 Msese Road. As a result of the changes made in section 8 of the Bank of Tanzania Act, 2006, the Bank has now four Executives, the Governor and three Deputy Governors, for whom it is obliged to provide official accommodation.

In 2006, in advance of the presidential appointment of the current office bearers, the Bank decided to construct two additional executive accommodations, one on plot No. 12 Tumbawe Road and another on plot No. 57 Mtwara Crescent at Oysterbay, Dar es Salaam. A team of consultants led by M/S SKY Architects Consultants was engaged to provide schematic drawings that were reviewed by the Bank and two of these, one for each plot, were selected for detailed design stage.


Each residence was designed to be a one storey building with five bedrooms, visitors lounge, family lounge, dining area and associated service rooms. The outbuildings include servant’s quarter, car ports, swimming pool, boundary wall, security systems and guard house. Services include power generator, central cooling system and water storage facilities while external works include landscaping and paved car park.

The consultants then prepared bills of quantities and technical specification that were compiled to form tender documents ready for tender process. All procedures in line with procurement laws and regulation were adhered to, when determining the cost of each of the residences as well as in selecting contractors and sub contractors. Each residence was considered as an independent project and a separate tender process was carried out for each one.

It is important for the public to know that, the planning and decision to have these houses constructed was done before Prof Benno Ndulu was appointed at the Bank of Tanzania.

Tenderers for works at plot No. 12 Tumbawe Street were invited using competitive open tender advertised on the Daily News of 26th February 2008. Interested contractors of class II and above were invited to apply for tender document and were instructed to pay non-refundable tender fee of Tshs 50,000/=.

A total of 12 contractors applied and collected the tender documents, but only 10 submitted their bids before deadline, 25th March 2008. The received tenders were opened by BOT Tender Board and forwarded to Project Consultant via the Bank of Tanzania Estate Management Department for evaluation. Tender results read during tender opening ranged from the lowest tender price of Tshs 1,399,184,549.00 to the highest price of Tshs 1,847,763,537.00.

After tender evaluation, which involved preliminary examination of tender, arithmetic correction and detailed analysis, the lowest evaluated bidder was determined to be M/s Electrics International Co. Limited at a corrected tender price of Tshs 1,274,295,025.26. Evaluation report was deliberated by BOT Tender Board and it was approved to award construction works to M/s Electrics International Co. Limited at a fixed contract price of Tshs 1,274,295,025.26 and 32 weeks completion period.

Contract agreement between the Bank and the contractor was signed on 3rd June 2008 and construction works started immediately thereafter. Subcontractors for specialized works were nominated and approved by the BOT Tender Board. These included M/s Remco (International) Ltd for Air Conditioning installation, M/s Ginde EAP Services Ltd for plumbing and drainage systems and M/s Pomy Engineering Co. Ltd for Electrical installations. All these companies are registered in Tanzania.

Tenderers for house no. 57 Mtwara Crescent were invited through a competitive tender method where 5 short-listed contractors were invited to collect tender documents and bid for work. Submitted tenders went through the same tender process detailed above that resulted into M/s Holtan Builders Ltd being determined the lowest evaluated bidder at Tshs 1,272,348,512.00 and 24 weeks completion period.

Subcontractor nominated and approved in this case were M/s Jandu Construction & Plumbers Ltd for plumbing and drainage systems, M/s Barkley Electrical Contractors Ltd for electrical installation and M/s Remco (International) Ltd for Air Conditioning installation. The cost for specialized works undertaken by subcontractors for each site is included on the fixed contract prices for respective main contractor. Likewise, lists of project parties for both works are displayed on the sign boards that are still erected at the front side of respective plots.

While the two projects were still on preliminarily stages, appointment of the three new executive officers to Bank of Tanzania was completed. The Bank was thus compelled to rent two residential houses one on plot No. 480 Bray Road Masaki and another on plot No. 591 at Msasani Peninsular.

One house was allocated to Professor Benno Ndulu, by then the first Deputy Governor, and another to Deputy Governor Lila Mkila. Prior to moving to this rented house; between October 2007 and April 2008, Prof Ndulu lived in his own house in Mbezi Beach. Likewise Deputy Governor Mkila stayed in his own house before moving to the rented premise.

These movements were to facilitate easy access to the office in light of traffic congestion in the city. It was decided to relocate Deputy Governor Juma Reli to house No. 387 Mahando Street to give way for planned refurbishment required at house No. 43 Msese road. Deputy Governor Enos Bukuku is residing in his own private house, and is paid housing allowance in lieu of occupying official residence as entitled – pending the planned refurbishment of Plot No. 43 Msese road residence.

The construction of the two executive residences has now been completed. Both Governor Ndulu and Deputy Governor Mkila, who were residing in rented houses have relocated to the new Bank of Tanzania official residences. The Governor has relocated to house No. 12 Tumbawe Road since 17th December 2009 and Deputy Governor Mkila to house No. 57 Mtwara Crescent since 4th December 2009.

As it is with all other Bank of Tanzania projects, these too will be subject to the usual audit process. It might be important for the public to know that, as stipulated in the Bank of Tanzania Act 2006 the Controller and Auditor General (CAG) is the external auditor for the Bank. The CAG has retained the services of the Ernst and Young, an international audit firm to support the external audit work of the Bank.

Issued by Public Relations & Protocol Department
BANK OF TANZANIA
30TH DECEMBER 2009

black is beautiful and white is wonderful?
A woman suffering from skin disorder due to sking lightening creams

THE zeal to look beautiful and a colonial mentality that white skin is superior is fast driving Tanzanian women into their graves as they risk their lives by using skin lightening creams that in the end turn lethal.

The problem is not only confined to Tanzania as selling of whitening creams is a lucrative business in Africa worth millions of US dollars a year. In some countries that allow the use of these lethal substances, shelves in pharmacies are stacked high with lotions, creams and soaps all promising to make women whiter and supposedly more beautiful.

But, in countries like Tanzania, where the use and importation of skin lightening creams is banned, the business is thriving as these dangerous creams are smuggled into the country while dealers on the other hand are discrete.

Read the rest of this mkorogo story:
tanzania yajiandaa vyema na kombe la dunia 2010
aina ya bango litalotumika katika kampeni ya TTB na TFF ya kuhamasisha umma kwenda kuishangilia Taifa Stars itapocheza na Ivory Coast January 4, 2010 katika uwanja wa taifa jijini Dar
Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010 Mh. Dr. Shukuru Kawambwa akiongea leo na wanahabari ofisini kwake jijini Dar kuhusu maandalizi ya kamati hiyo na kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo. Wengine toka kulia ni Dan Mrutu Kutoka Baraza la Biashara na Frolence Turuka katibu mkuu wa wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya juu

Rais wa TFF akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. Wengine ni Dk Shukuru Kawamba, Mh. Frolence Turuka na Bw. Dan Mrutu.

BILIONI SABA ZATENGWA KWA KAMPENI YA FIFA WORLD CUP 2010
Jumla ya shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo.

Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk Shukuru Kawamba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010, amesema leo pesa hiyo itatumika kwa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na vya kimataifa, ulinzi na kuzigharamia timu na wageni.


Dk Kawambwa kasema televisheni za Supersport kutoka Afrika Kusini na SunVideo kutoka Brazil ziko tayari kufanya kazi ya kutangaza mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania na maadalizi ya timu mbalimbali zitakazokuwa hapa nchini. Vyombo vingine ni BBC, Dautchwelle, Al jazeera VOA na vingine vingi.

Ameelezaa kuwa kampeni hiyo itaanza mapema wakati Timu ya Ivory Coast itapowasili nchini Januari 2 na kucheza na timu ya taifa Taifa Stars januari 4 na pia itacheza na timu ya Rwanda Januari 7 ambayo itawasili hapa nchini Januari 6 kwa ajili ya mchezo huo.

Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Leodegar Chilla Tenga amesema tayari TFF wana mawasiliano na nchi nyingi zilizofanikiwa kuingia kwenye Fainali za Kombe la Dunia chini Afrika Kusini.

Tenga kazitaja nchi walizokwisha wasiliana nazo kuwa ni pamoja na Ujerumani, Italy, Denmark, New Zealand, Brazil, Australia, Korea Kaskazini,Japan, Argelia na Nigeria na nchi zingine ambazo bado mazungumzo yanaendelea.

Wakati huo huo Bodi ya Utalii (TTB) ikishirikiana na TFF wameanza kampeni ya kuhamasisha umma wa watanzania kwenda kuiunga mkono na kuishangilia Taifa Stars wakati wa mechi yake na Ivory Coast katika mchezo wa kirafiki Januari 4 kwenye uwanja wa Taifa.

Katika kampeni hii kutakuwa na mabango makubwa na madogo ya matangazo, vipeperushi, matangazo ya redio, magazeti na televisheni pamoja na vijarida ili kuhamasisha mashabiki kwenda kushangilia timu yao.

BREKING NYUUUUZZZ: SIMBA WA VITA HATUNAYE TENA
KIPENZI CHETU SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA HATUNAYE TENA.
MZEE KAWAWA AMETUTOKA LEO ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA TOKEA JANA BAADA YA KUPATA MATATIZO YA KIAFYA.
ALIZALIWA LIWALE MWAKA 1926 AMBAPO BAADA YA KUSHIKA NYADHIFA MBALI MBALI ALIKUWA WAZIRI MKUU KUANZIA JANUARI 22, 1962 HADI FEBRUARI 13, 1977 AKIFUATIWA NA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE. BAADAYE ALIKUWA KATIBU MKUU WA CCM KABLA YA KUSTAAFU.
RAIS JAKAYA KIKWETE AKITETA NA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA KATIKA MOJAWAPO YA PICHA ZA MWISHO ZA KUTUMIMIKIA TAIFA ENZI ZA UHAI WAKE
MZEE KAWAWA AKIWA MMOJA WA WAKUU WALIOPIGANIA UHURU AKIWA KATIKA TAFRIJA YA KUSHEREHEKEA UHURU WA TANGANYIKA. YEYE NA MWALIMU WALIKUWA WATU WA KARIBU NA WALILITUMIKIA TAIFA KWA MOYO WOTE
MZEE KAWAWA AKIWA NA MKEWE BUNGENI DODOMA. PAMOJA NA UTU UZIMA DAIMA ALKIKUWA MSTARI WA MBELE KULITUMIKIA TAIFA
MZEE KAWAWA AKITUNUKIWA TUZO YA AMANI YA MARTIN LUTHER KING NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
MZEE KAWAWA ALIKUWA HAKOSEKANI KWENYE VIKAO MUHIMU VYA CCM
MZEE KAWAWA ALIKUWA RAFIKI WA KARIBU NA WANAHABARI. HAPA AKIWA NA CHARLES HILARY WA BBC WAKATI AKIWA JIJINI LONDON, UINGEREZA, KWA MATIBABU
MZEE KAWAWA ALIKUWA MPENZI MKUBWA WA MICHEZO. HAPA AKIWA REFA KATIKA MCHEZO WA WABUNGE NA MAWAZIRI ENZI HIZO
MZEE KAWAWA AKIWA NA TAIFA STARS
MZEE KAWAWA AKIWA MGENI RASMI KWENYE ONESHO LA MISS TANZANIA AMBAPO MSHINDI ALIIBUKA RICHA ADHIA ALIYE NYUMA YAKE
MZEE KAWAWA AKIWA NA MWALIMU NA RAIS WA ZANZIBAR ENZI HIZO MZEE ABOUD JUMBE. PEMBENI NI RAIS SAMORA MACHEL WA MSUMBUJI
AKIWA KAMA KIONGOZI WA VITENDO MZEE KAWAWA ALIKUWA MIONGONI MWA WATU WA KWANZA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA MUJIBU WA SHERIA MARA TU LILIPOANZA RASMI
MZEE KAWAWA AKIWA NA MWALIMU PAMOJA NA KIONGOZI WA DINI WA DHEHEBU LA ISMAILIA DUNIANI H.H. THE AGA KHAN


mafuriko barabara kuu ya moshi-arusha
Juu na chini ni gari aina ya fuso iliyokua inatokea Arusha kuelekea moshi ikiwa imeangushwa na mafuriko yaliyokuwa yamekatiza barabarani kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha mkoani Kilimanjaro fuso hiyo ilianguka katika mbele kidogo ya kijiji cha kwa Sadala wilayani Hai mkoani kilimanjaro. Mafuriko hayo yalizuia magari kupita kwa muda wa lisaa na nusu.(picha na Woinde Shizza)
Fuso likiwa limelala ubavu
maji yaendayo kasi yakikatisha barabara



KIJANA ACHOMWA MOTO MBEZI RUBOKO LEO
MPITANJIA AKIANGALIA MABAKI YA MWILI WA KIJANA MMOJA ASIYEJULIKANA AMBAYE WAKAZI WA MBEZI RUBOKO JIJINI DAR WENYE HASIRA KALI ALFAJIRI YA LEO WAMEMCHOMA MOTO HADI KUFA BAADA YA KUKUTWA AKIIBA VITU VYA NDANI KWENYE NYUMBA YA KARIBU NA ENEO LA TUKIO.
AJALI ENEO LA KWENKULU KARIBU NA MKATA
kama kawaida magari yatokayo Dar yalikuta kuna foleni ndefu sehemu ya ajali ambapo Lori lililodondoka katikati ya barabara na kuziba njia katika kijiji cha kwenkulu wilayani handeni ktk barbar kuu iendayo arusha
Lori la kijani lilijaribu kuinua bila mafanikio
Likaja kiboko yake Lori la TANESCO ndio likaliinua na kulitoa barbarani
mwishowe lilisalim amri na kuinuka na safari zikaanza kama kawa.
hakuna aliyeumia na bidhaa yote ya matairi ilibaki salama
Picha na KAM wa Globu ya Jamii

Wednesday, December 30, 2009

libeneke la culinary chamber lanukia, kuzinduliwa mwaka mpya
mambo ya kuchonga chonga pia
yatakuwepo ktk blog ya culinary chamber
Asalaam alaykhum ankal Kadidi,

Wajina, blog yetu ya CULINARY CHAMBER itazaliwa rasmi tar 1/1/2010. Hivi sasa article za awali zinamaliziwa pamoja na picha baadhi. Imani yangu ni kuwa wataalamu wa fani hii watachangia kwa moyo mmoja ili wadau wote wapenda misosi waweze kufaidika kwa utaalamu wa mapishi mbali mbali yatakayoporomoshwa. Nnaimani ushirikiano utakua mzuri ili tuboreshe blog yetu. Mwanzo mgumu ila penye nia pana njia tutafika tu kwa juhudi na uchakarikaji.

Pokea picha hizo ambazo nilibahatika kushiriki pia mashindano ya finger foods ambayo lengo haikua kupata mshindi ila ni kubadilishana ujuzi toka kwenye vyuo mbali mbali vya culinary duniani vyenye ushirikiano wa pamoja toka nchi za Croatia, USA, Uk, France, Italy, Malaysia , Indonesia, India, Korea, China, Singapole, German, Austria, Swistzerland, Netherland, spain na Belgium.
Picha za vyakula na habari zaidi watazipata ktk blog ya Culinary Chamber.
Baada ya mashindano hayo jioni ilikua ni bonge la party wanafunzi waliochukua kozi ya general hotel management na mambo ya matukio walitoa perfomance safi yenye ladha ya mataifa yao ilikua super sana ankal michuzi.
Ila kubwa kuliko yote ni pale nilipooona bendera ya taifa langu imepanda juu kama heshima ya mshiriki toka Tanzania. ohhhhhh.... nilihisi machozi kunidondoka kwa furaha.

Ndugu zangu nawaomba sana sana tushirikiane. Shule hii ni bure wala hakuna gharama yeyote kwa hiyo yeyote mwenye ujuzi atoe, msijifiche. Huu ndio wakati muafaka wa kubadilishana utaalamu kwani hakuna anaejua zaidi. Wote tunajua kiasi kwa hiyo tukichanganya maarifa inakua safi mambo yanakamilika na kunoga au vipi kaka misupu? hahahahhahaa
HAPPY NEW YEAR TO ALL !
nashukuru sana kwa maoni yenu yote
nayaheshimu sana mungu awabariki.

Chef Issa
Chef Issa akiwa na Chef Leonard ambaye ni senior lecturer wa culinary wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan Univeristy

usiku baada ya mashindano ilikua ni bonge la party na bendera za nchi washiriki zote zilipandishwa. Cheki bendera yetu inavyowaka.

Tuesday, December 29, 2009

kelvin na gatty wameremeta
mdau kelvin na mai waifu wake gatty wakiselebuka wakati wa mnuso wao ukumbi wa hellenic club jijini wikiendi ilopita baada ya kumeremeta kanisa la St. Alban. Chini wakila keki kwa pamoja kuonesha wao sasa ni mwili mmoja na binadamu hawatenganishi

Hongera jombi kwa kupata jiko na kutuonyesha njia madogo zako huku nyuma. Nawatakia kila la kheri katika maisha yenu na pia muendelee kuwa na furaha katika maisha yenu yote kama hapo mlivyo hapa Duniani ni hayo tu .
Anko Kadidi.


Bongo jamani !!!
Mdudu gani anatusumbua !!

Ankal kama nilivyokuahidi hali ya barabara ya Tarakea to Marangu hivi sasa si shwari. Yaani tumelazimika kusimama masaa sita baada ya barabara kuzuiliwa na Dar Express kama unavyoona ikiwa imejikita kwenye udongo, na kidogo tu iwamwage abiria zaidi ya hamsini waliokuwemo. Kama hiyo haitoshi likaja basi dogo la fuso hapo na kuziba barabara kwa kukwama na kusababisha usumbufu wa zaidi ya magari mia.
Picha na stori na Mdau Isaya Philip
Hapa ni Rombo Mkuu kilometa tatu tu kutokea Rombo kuelekea Marangu ambapo mdau Isaya Philip alilazimika kuacha vekesheni na kushirikiana na wadau kuwatoa wajenga nchi
zege halilali hapa....
Anko naninihii jionee hapo wakati nyie mnahangaikia barabara za gorofa na kusota kwenye foleni huko kwenu wenzenu wanahangaikia huku mitaa ya Tarakea barabara ya changalawe tu ili waondokane na adha hii ya kufanya kazi ngumu ya kusukuma magari kabla ya kazi zao za msingi
kimbembe Tarakea





kp na Busara zake !!


nyundo mtindo mmoja dar
bomoa bomoa ya majengo makuukuu kupisha mapya inaendelea kwa kasi jijini dar, ingawa kasi hiyo haijaelekezwa pia katika miundombinu kama vile mifereji ya maji taka na safi, sehemu za maegesho na kadhalika. bila shaka wahusika wanajua wanachokifanya. hapa ni katika mduara wa mtaa wa jamhuri karibu na DTV

basi a meridian express lapata ajali mkata jioni jana

wananchi kijiji cha Mkata mkoani Tanga wakiangalia

basi la Meridian lililogongana na lori jioni jana sehemu hizo

Mie ndo natoka vekesheni Roitoktok huko Kenya mpakani mwa Tanzania, nimepita njia ya Tarakea, yaani haifai. Baadaye kidogo ntakutumia taswira za huko.
Hapo juu ni ajali nimeikuta sehemu za Mkata mkoa wa Tanga ambapo basi la Meridian limegongana na lori. Dereva wa Meridian kajitahidi sana kuokoa maisha ya abiria kwani lori lilihama njia na dereva wa Meridian akasave kidogo kwa kuingia kwenye reserve ya barabara.
Hadi naondoka saa kumi jana hamna aliyekufa ila majeruhi walikuwa kibao na polisi walikuwa hawajafika.

Mdau Isaya Philip
tarehe ya mwisho ya usajili wa namba za simu yasogezwa hadi juni 30 mwakani
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Mkomwa akimbrifu Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe aliyetembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya kimataifa ya mawasiliano huko Geneva mwezi oktoba mwaka huu. Katikati ni Naibu katibu mkuu wa ITU Houlin Zhao


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesogeza mbele kwa miezi sita zaidi tarehe ya mwisho la zoezi la kusajili namba za simu nchini ili kutoa fursa kwa wote wanaomiliki namba hizo kujisajili.

Tarehe ya mwisho ya kusajili
namba ya simu sasa ni Juni 30, 2010.

Awali TCRA ilitoa iliwajulisha wananchi kuwa kuanzia tarehe 1 Julai 2009 makampuni yote ya simu za mikononi yataanza kusajili wateja wao waliopo na wapya ili kuhakiki umiliki wa namba za simu wanazozitumia. Zoezi hili limeendelea kwa miezi sita na mwisho ulikuwa tarehe 31 Desemba 2009.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Mkomwa amesema jana jijini Dar kwamba zoezi la kusajili simu limeenda vyema na kwamba takriban namba za simu milioni 6 zimeshasajiliwa.

Amesema ulazima wa kusogeza tarehe ya mwisho mbele umetokana na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme na vitambulisho hasa sehemu za vijijini. Akaeleza imani yake kwamba ifikapo Juni 30 mwakani kila mmoja atakuwa ameshasajili namba yake.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inawahimiza wananchi kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo ambavo yametayarishwa kwa mfumo wa maswali na majibu kwa mujibu wa tangazo hilo la awali:

1. Swali: Kwa nini usajili namba ya simu?
Jibu: Kwa ajili ya kukulinda wewe na namba yako dhidhi ya matumizi mabaya ya simu.

2. Swali: Kitambulisho cha aina gani kitahitajika wakati wa usajili?
Jibu: Ili uweze kusajiliwa unahitaji kufika kwenye ofisi ya kampuni yako ya simu au wakala
wake na moja ya vitambulisho vifuatavyo ambapo utawapatia kivuli chake:-
(i) Kitambulisho cha mpiga kura
(ii) Pasipoti
(iii) Kitambulisho cha mfuko wa pensheni
(iv) Leseni ya udereva
(v) Kitambulisho cha SACCOS
(vi) Kitambulisho cha benki
(vii) Kitambulisho cha ajira pamoja na barua ya mwajiri
(viii) Kitambulisho cha chuo cha elimu ya juu
(ix) Kitambulisho cha uanachama kwenye kilabu
(x) Barua ya serikali za mitaa ikiwa na picha, sahihi na muhuri


3. Swali: Nisipojisajili ifikapo tarehe 30 juni, 2010 nini kitatokea?
Jibu: Namba yako itafungwa ili usiweze kuitumia kwenye mtandao wa simu nchini Tanzania.

4. Swali: Nani na wapi ninaweza kusajili namba yangu ya simu?
Jibu: Unaweza kusajiliwa na kampuni yako ya simu za mkononi au mawakala wao waliopo sehemu mbali mbali nchini.

5. Swali: namba ngapi za simu (simcard) ambazo ninaweza/ninaruhusiwa kusajili?
Jibu: Idadi yoyote kadri utakavyo.

7. Swali: Kuna uhakika gani wa usiri wa taarifa zangu nitakazotoa kwa kampuni ya simu za mkononi au wakala wao?
Jibu: Kampuni zote za simu nchini zinawajibika kwa mujibu wa sheria, kutunza taarifa za wateja wao ikiwa ni pamoja na taarifa za matumizi.

8. Swali: Taarifa zipi zinahitajika wakati wa usajili?
Jibu: Tafadhali angalia mfano wa fomuya usajili hapo chini:-


Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
promosheni ya shangilia taifa stars yazinduliwa jana
Meneja uhusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akiwa na wachezaji wa timu ya Taifa walioshika jezi zenye majina yao jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya shangilia taifa stars ishinde jana kwenye kiwanda cha Serengeti jijini Dar.

Promosheni ya shangilia Taifa Stars inaanza leo kabla timu hiyo kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya Ivory Cast Januari 4 na 7 jijini Dar.
Ivory Coast inajiandaa na mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Angola.
Promosheni hiyo itawafanya mashabiki mbalimbali wa soka katika baa mbalimbali kujishindia zawadi mbalimbali na jezi za timu ya Taifa pamoja na tiketi za kuingilia katika michezo hiyo neshno
libeneke la tembeatz.blogspot.com oye!

hii ni story ya twiga wa Arusha national park kutokuwa na sehemu ya mwisho ya mkiani ambayo huwa na manyoya. Juu ni taswira za twiga amba tulibahatika kukutana nae ndani ya Arusha park akiwa hana sehemu ya mwisho ya mkia wake.
------------------------------

hepi besdei ya siku ya kuzaliwa profesa mwandosya Jana
Profesa Mark Mwandosya akilishwa keki na mjukuu wake jana wakati wa hepi besdei yake ya kuzaliwa iliyofanyika kijijini kwake Lufilyo, Rungwe. jana kagota miaka 60
Profesa Mwandosya akipokea zawadi toka kwa wajukuu akisaidiwa na mwanae

Monday, December 28, 2009

Chef Issa Hongera tuko pamoja !!!




Habari Kaka Safari,
Natumai hujambo ndugu yangu mimi ni shabiki mkubwa wa blog yako ya kadidi, Nimemaliza masomo yangu ya culinary kwa mafanikio makubwa sana pokea picha za graduation yangu na picha nikiwa jikoni wakati wa mafunzo. mwezi wa 6 mwaka huu nilichaguliwa kama muafrica pekee kuhudhulia moja ya tamasha kubwa duniani la art Basel switzerland katika fani ya misosi. Nimepata shahada ya Arts in European culinary Management inayotambulika na Manchester Metropolitan University UK na International Hotel Management Institute Switizerland. Nitakua ni Executive chef mdogo kuliko wote Tanzania kua HACCP certified na kufungua na kuongoza five star hotel. Elimu niliyoipata nataka kushea na ndugu zangu kwa kufungua blog itakayoitwa CULINARY CHAMBER january narudi nyumbani kabla ya kuifungua rasmi blog nahitaji kupata ushauri kwenu wakonge wa blog hapo nyumbani nawatakia wapenzi wote wa blog hii kheri ya mwaka mpya 2010 peace and love to all kaka unawakilisha vilivyo Big up.

Chef Issa