Thursday, December 31, 2009

tanzania yajiandaa vyema na kombe la dunia 2010
aina ya bango litalotumika katika kampeni ya TTB na TFF ya kuhamasisha umma kwenda kuishangilia Taifa Stars itapocheza na Ivory Coast January 4, 2010 katika uwanja wa taifa jijini Dar
Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010 Mh. Dr. Shukuru Kawambwa akiongea leo na wanahabari ofisini kwake jijini Dar kuhusu maandalizi ya kamati hiyo na kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo. Wengine toka kulia ni Dan Mrutu Kutoka Baraza la Biashara na Frolence Turuka katibu mkuu wa wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya juu

Rais wa TFF akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. Wengine ni Dk Shukuru Kawamba, Mh. Frolence Turuka na Bw. Dan Mrutu.

BILIONI SABA ZATENGWA KWA KAMPENI YA FIFA WORLD CUP 2010
Jumla ya shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo.

Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk Shukuru Kawamba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010, amesema leo pesa hiyo itatumika kwa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na vya kimataifa, ulinzi na kuzigharamia timu na wageni.


Dk Kawambwa kasema televisheni za Supersport kutoka Afrika Kusini na SunVideo kutoka Brazil ziko tayari kufanya kazi ya kutangaza mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania na maadalizi ya timu mbalimbali zitakazokuwa hapa nchini. Vyombo vingine ni BBC, Dautchwelle, Al jazeera VOA na vingine vingi.

Ameelezaa kuwa kampeni hiyo itaanza mapema wakati Timu ya Ivory Coast itapowasili nchini Januari 2 na kucheza na timu ya taifa Taifa Stars januari 4 na pia itacheza na timu ya Rwanda Januari 7 ambayo itawasili hapa nchini Januari 6 kwa ajili ya mchezo huo.

Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Leodegar Chilla Tenga amesema tayari TFF wana mawasiliano na nchi nyingi zilizofanikiwa kuingia kwenye Fainali za Kombe la Dunia chini Afrika Kusini.

Tenga kazitaja nchi walizokwisha wasiliana nazo kuwa ni pamoja na Ujerumani, Italy, Denmark, New Zealand, Brazil, Australia, Korea Kaskazini,Japan, Argelia na Nigeria na nchi zingine ambazo bado mazungumzo yanaendelea.

Wakati huo huo Bodi ya Utalii (TTB) ikishirikiana na TFF wameanza kampeni ya kuhamasisha umma wa watanzania kwenda kuiunga mkono na kuishangilia Taifa Stars wakati wa mechi yake na Ivory Coast katika mchezo wa kirafiki Januari 4 kwenye uwanja wa Taifa.

Katika kampeni hii kutakuwa na mabango makubwa na madogo ya matangazo, vipeperushi, matangazo ya redio, magazeti na televisheni pamoja na vijarida ili kuhamasisha mashabiki kwenda kushangilia timu yao.

No comments: