BREKING NYUUUUZZZ: SIMBA WA VITA HATUNAYE TENA
MZEE KAWAWA AMETUTOKA LEO ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA TOKEA JANA BAADA YA KUPATA MATATIZO YA KIAFYA.
ALIZALIWA LIWALE MWAKA 1926 AMBAPO BAADA YA KUSHIKA NYADHIFA MBALI MBALI ALIKUWA WAZIRI MKUU KUANZIA JANUARI 22, 1962 HADI FEBRUARI 13, 1977 AKIFUATIWA NA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE. BAADAYE ALIKUWA KATIBU MKUU WA CCM KABLA YA KUSTAAFU.
RAIS JAKAYA KIKWETE AKITETA NA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA KATIKA MOJAWAPO YA PICHA ZA MWISHO ZA KUTUMIMIKIA TAIFA ENZI ZA UHAI WAKE
MZEE KAWAWA AKIWA MMOJA WA WAKUU WALIOPIGANIA UHURU AKIWA KATIKA TAFRIJA YA KUSHEREHEKEA UHURU WA TANGANYIKA. YEYE NA MWALIMU WALIKUWA WATU WA KARIBU NA WALILITUMIKIA TAIFA KWA MOYO WOTE
MZEE KAWAWA AKIWA MMOJA WA WAKUU WALIOPIGANIA UHURU AKIWA KATIKA TAFRIJA YA KUSHEREHEKEA UHURU WA TANGANYIKA. YEYE NA MWALIMU WALIKUWA WATU WA KARIBU NA WALILITUMIKIA TAIFA KWA MOYO WOTE
MZEE KAWAWA AKIWA NA MKEWE BUNGENI DODOMA. PAMOJA NA UTU UZIMA DAIMA ALKIKUWA MSTARI WA MBELE KULITUMIKIA TAIFA
MZEE KAWAWA AKITUNUKIWA TUZO YA AMANI YA MARTIN LUTHER KING NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
MZEE KAWAWA ALIKUWA HAKOSEKANI KWENYE VIKAO MUHIMU VYA CCM
MZEE KAWAWA ALIKUWA RAFIKI WA KARIBU NA WANAHABARI. HAPA AKIWA NA CHARLES HILARY WA BBC WAKATI AKIWA JIJINI LONDON, UINGEREZA, KWA MATIBABU
MZEE KAWAWA ALIKUWA MPENZI MKUBWA WA MICHEZO. HAPA AKIWA REFA KATIKA MCHEZO WA WABUNGE NA MAWAZIRI ENZI HIZO
No comments:
Post a Comment