Thursday, October 28, 2010

Wednesday, October 27, 2010

mahojiano live ya dr slaa ndani ya clouds fm leo asubuhi.


Mahojiano LIVE ya mgombea Urais kwa chama cha CHADEMA Dr Willbroad Slaa na Clouds FM kupitia kipindi cha Power Breakfast leo asubuhi ,wakati huo mgombea Urais kwa chama cha CCM,Dk Jakaya Kikwete anatarajiwa kufanya mdahalo na vyombo vya habari mbalimbali katika ukumbi wa Anatoglo siku ya ijumaa,jijini Dar,kuanzia saa mbili usiku mpaka saa nne usiku.Sauti hii kwa hisani ya Mdau Shelu.

mpoto asherehekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima

Mrisho Mpoto akikabidhi msaada wa vyakula kwa mlezi wa watoto yatima.

Mwanamuziki wa miondoko ya kizazi kipya MRISHO MPOTO amewataka wadau mbalimbali kuwasaidia watoto yatima kielimu na kiuchumi hatua itakayosaidia watoto hao kufikia malengo yao kimaisha

Mrisho Mpoto amesema hayo wakati akisherekea siku yake ya kuzaliwa na watoto wa kituo cha CHAWAMA kilichopo SINZA jijini DSM ambapo pia amekiri mchango wa watoto wadogo katika mafanikio yake kimuzik.

Naye mlezi wa kituo hicho SAIDA HASSAN ameshukuru watu mbalimbali wanaovutwa kujua mahitaji ya watoto yatima na kutoa misaada yao hali iliyomfanya ashindwe kujizuia na kuwaombea Dua kwa mola.Zaidi Bofya Hapa

Baada ya hapo basi na tuburudike na wimbo wake wa Adella unaofanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki hapa bongo


jk aitikisa mwenye yanga jioni ya leo.


Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ,Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wanachama wa CCM katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar es Salaam leo jioni .
Umati wa wana CCM ukimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam. (Picha na FreddyMaro).

dk slaa aibananisha manzese na mwenge yanga jana jijini dar.

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake wa kampeni jana mchana.
Wapenzi na wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa na bango lenye ujumbe mbalimbali, katika mkutano wa mgombea urais kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam jana jioni.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, katika mkutano wa kampeni, kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jana jioni.Picha kwa hisani ya Joseph Senga wa Tanzania Daima.

Monday, October 25, 2010

Msalaba Mwekundu kutoa huduma ya kwanza siku ya uchaguzi
Na Mwandishi Wetu.

CHAMA cha Msalaba Mwekundu Nchini,(Tanzania Red cross Society-Red Cross) kupitia kikosi chake maalum cha Uokoaji na Maafa mkoa wa Dar es Salaam (Action Team) kimejipanga vyema kuhakikisha kinatoa huduma ya kwanza na ya dharura kwa kiwango cha juu siku ya Oktoba 31,wakati wa uchaguzi mkuu.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Red cross Mkoa wa Dar es Salaam, Mayasa Mikidadi muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa kikosi hicho.

Mayasa alisema kuwa Red Cross imejiandaa vya kutosha kutoa huduma ya kwanza na ya dharura wakati siku ya kupiga kura na matatizo yote ya dharura. “Ni hakika kazi iliyopo mbele yetu ni ngumu, lakini hakikika uwezo tunao na tutaifanya kwa nguvu zote ilikuakikisha kila mtanzania anapata haki ya kupiga kwa usalama kura zake” alisema Mayasa.

Aliendelea kusema kuwa, kikosi hicho kitafanya shughuli za uokoji siku hiyo ambazo zikiwalenga watu watakao kuwa wamezidiwa katika foleni, wagonjwa pamoja na kuwasaidia walemavu wa aina yote kusaidiwa kwa lolote litakalotokea wakati wa upigaji wa kura hizo.

Aidha, katika uchaguzi huo, ambao awali viongizi hao walikuwa kwa muda kwa kipindi cha miaka kadhaa, waliweza kujiuzuru na kupisha uongozi mpya ambao ulifanywa kwa njia ya amani huku wakichaguana kwa kanuni ya kupiga kura.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na: Dk. Suphian Juma (Kamanda Mkuu), Feruzi Mpili (Kamanda Msaidizi) huku nafasi ya Katibu ikichukulkiwa na Amina Mwalimu.

Uongozi huo mpya ulishukuru kwa kuchaguliwa kwao kutokana na kuwa na imani nao huku na kuaidi kushirikiana nao bega kwa bega na wanachama wa matawi yote mkoa.

Kwa upande wake, Kamanda mpya, Dk Suphian aliwashukuru wanachama wote kwa kumchagua huku akiwataka kila mwanachama kushirikiana bega kwa bega ilikufanikisha uongozi makini. “Naomba ushirikiano na kila mmoja ilikukijenga kikosi kwa hali ya juu na kuwa cha mfano wa kuigwa” alisema Dk. Suphian.

Katika uchaguzi huo ambao pia ulisimamiwa na Mratibu mkoa wa chama hicho, Grace Mawala, pamoja na Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Mambo ambao wote kwa pamoja waliwataka wanachama kuakikisha wanashirikiana na uongozi mpya.
mgambo wa jiji kutumia kulinda vituo vya kupigia kura siku ya uchaguzi mkuu

Na Mohammed Mhiona, wa Jeshi la Polisi

Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam wamesema watawatumia Askari Mgambo katika kusaidiana na Jeshi la Polisi katika kulinda Usalama wa vituo wakati wa zoezi la upigaji kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wakurugenzi hao waliyasema hayo wakati wa mkutano wa pamoja na Makamanda wa Polisi wa Mikoa mitatu ya Kanda ya Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo wametoa wito kwa kila askari mgambo kupiga ripoti kwa mshauri mgambo wa wilaya yake.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala Bw. Gbriel Fuime, na Mkurugenzi wa wilaya ya Temeke Bw. Stephen Kongwa, wamesema kuwa mgambo hao watakuwa sehemu ya walinzi wa vituo na watalipwa posho kama ilivyotagazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Wamesema Mgambo hao watahakikiwa na kupangiwa kazi na baadaye kutawanywa katika vituo watakavyopangiwa na wakurugenzi katika halmashauri husika.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Naibu Kamishna (DCP) Suleimani Kova, Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Absalom Mwakyoma, na Msaidizi wake ACP Charles Kenyela, walisema ni vema kila kukijitokeza jambo la muhimu, kuvitumia vyombo vya habari katika kutoa ufafanuzi ili kuwaondolea wananchi shaka katika mambo ya kuhiisi.

Mkutano huo pia umewashirikisha maafisa waandaamizi kutoka mikoa hiyo pamoja na wakuu wa Upelelezi wa mikoa hiyo.

Saturday, October 23, 2010

8 Foods That Lower Anxiety and Stress


dk slaa aichakachua monduli mjini.!


NITAGOMBEA KIPINDI KIMOJA-DR SLAA
Pichani Dk. Slaa akihutubia maelefu ya wananchi wa mji wa Mwanza siku ya Jumatano

Na Mwandishi Wetu.

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa amesema kuwa endapo wapiga kura watamchagua kuwa Rais wao basi atawatumikia kwa kipindi kimoja na hatogombea tena mwaka 2015. Dr. Slaa ametoa ahadi hiyo alipozungumza na kijarida hiki mapema wiki hii katika mazungumzo ya kina yaliyohusu kampeni yake,mipango yake na mwelekeo wa chama chake kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuwa tangu mwanzo alipoombwa kuwa mgombea wa Urais katika uchaguzi huu alishaamua kuwa akipata nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa kisiasa nchini basi hatotaka kugombea tena kipindi cha pili akimaliza muda wake wa Urais. Dk. Slaa alirejea maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere Ikulu “siyo mahali pa kukimbilia” na kuwa yeye hakuwahi katika maisha yake kuwazia wala kutamani cheo hicho, hivyo anataka kuingia kufanya aliyoahidi kufanya na kutoka kuwaachia wengine.

“Tangu mwanzo waliponiomba nilikubali nikiwa na nia ya kuwa Rais kwa awamu moja tu na kinyume na wengine sitoingia ili nitumie miaka miwili au mitatu kujifunza halafu nirudi kuomba niongezewe muda, mimi ninaingia tayari kufanya kazi kwani Urais hauna chuo” amesema Dk Slaa mara baada ya kumaliza mkutano wake mkubwa wa kampeni huko Shinyanga na akiwa anajiandaa na mikutano ya Mwanza na maeneo mengine nchini huku siku zikiwa zinakimbia kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 31 mwaka huu.

Akizungumzia kwa kina uamuzi wake huo Dr. Slaa amesema kuwa pamoja na kuzingatia usia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere yeye mwenyewe alikuwa na sababu zake nyingine za kutotaka kugombea tena kipindi cha pili. “Kwanza, kiumri nitakuwa nakaribia miaka sabini ifikapo mwaka 2015 (Dr. Slaa anatimiza miaka 62 Oktoba 29) sasa heka heka za kampeni tena na mambo ya kisiasa nataka niwaachie wengine ili na mimi nifurahie maisha ya kustaafu” ameelezea.

Pamoja na sababu hiyo Dr. Slaa ameelezea vile vile nia yake ya kuhakikisha kuwa utakapofika mwaka 2015 serikali ya Chadema na chama vitakuwa vimeandaa watu wa kutosha na wenye uzoefu wa kutosha kiuongozi ili waweze kuchukua nafasi baada yake.

“Unajua CCM wamewaandaa watu wao mbalimbali kiasi kwamba wana wigo mkubwa sana wa kupata viongozi wa serikali kwani wengi wamepata uzoefu wa aina mbalimbali kwa muda mrefu.

Kwa upande wetu ninataka tutumie miaka hiyo mitano kuandaa viongozi wapya kabisa wa kisiasa nchini nje ya wale walioko CCM ambao wanaweza kuiongoza serikali.”

Pamoja na sababu hiyo Dk. Slaa amesema kuwa lengo lake ni kuanzisha mabadiliko makubwa nchini ya kusahihisha makosa ya utawala wa CCM yaliyodumu kwa miaka 49. “Ni lazima tusahihishe makosa haya,hatuwezi kuendelea na njia ambayo tunajua tayari tumepotea.

Tutakuwa ni watu wa ajabu kama pamoja na kujua tumepotea tutaendelea kwa hiari yetu kuchagua kupotea miaka na miaka, hivyo nataka niweke msingi wa mageuzi makubwa ya utendaji kazi na utawala nchini ili tuweze kuwarithisha watoto wetu na watoto wa watoto wetu taifa bora zaidi lenye mafanikio na maendeleo zaidi”

Akizungumzia mwelekeo wa kampeni yake ambayo kwa maoni ya watu wengi inaonekana kuwa na uhai wa aina yake Dk Slaa amesema kuwa kama kuna watu walifikiri ameingia katika kinyang’anyiro hicho ili kubahatisha basi wamefanya makosa.

“Tumeingia kwa lengo la kushinda na siyo kusindikiza na kinachosimama kati yetu na ushindi ni wapiga kura!” Alisema kwa kujiamini.

Akijibu swali la ni kitu gani kimemgusa hasa katika kampeni zake zilizomchukua katika kona mbalimbali za nchi yetu Dk. Slaa amesema kuwa kati ya mambo ambayo yamemgusa zaidi na kumfanya awe shime zaidi ya kuwatumikia Watanzania kama Rais wao ni hali ya makazi ya wananchi wengi kijijini.

“Wananchi wetu wengi wanaishi katika nyumba ambazo kwa kweli kabisa hazistahili kuishi wanadamu.

Yaani miaka 49 ya uhuru bado watu wanaishi kama walivyoishi kabla ya uhuru na kabla ya kuja wakoloni!,hii ni dhambi ya taifa na ni aibu” alisema Dr. Slaa.

Katika mazungumzo hayo Dr. Slaa amewataka Watanzania kumchagua kwa kura nyingi na wasitishwe na kauli zenye kuwafanya wahofie kupiga kura au kutoona umuhimu wa kura bali wajitokeze kwa maelfu,wakishikana mikono katika familia kwenda kumchagua yeye pamoja na wagombea wote wa Ubunge na Udiwani ili aweze kweli kupata watu wa kushirikiana nao na wenye mtazamo mmoja.

Dr. Slaa amezungumzia mambo mengine mengi kuhusu kampeni yake, ajenda yake na malengo yake kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Mazungumzo hayo na Dr. Slaa yatarushwa siku ya Jumamosi asubuhi (saa za Marekani) kupitia mtandao wa http://www.bongoradio.com na baadaye yatapatikana kwa njia ya mtandao na Cds yakijumuisha mahojiano na wagombea wengine wa Uchaguzi huu
Failure

Failure doesn't mean - "You are a failure,"

It means - You have not succeeded.

Failure doesn't mean - "You accomplished nothing,"
It means - You have learned something.

Failure doesn't mean - "You have been a fool,"
It means - You had a lot of faith.

Failure doesn't mean - "You don't have it,"
It means - You were willing to try.

Failure doesn't mean - "You are inferior,"
It means - You are not perfect.

Failure doesn't mean - "You've wasted your life,"
It means - You have a reason to start afresh.

Failure doesn't mean - "You should give up,"
It means - "You must try harder.

Failure doesn't mean - "You'll never make it,"
It means - It will take a little longer.

Failure doesn't mean - "God has abandoned you,"
It means - God has a better way for you.
sweden kunani tena???

MUUAJI ATINGISHA JIJI LA MALMÖ NCHINI SWEDEN

Kuna mlenga shabaha anae washuti wahamiaji wanaoshi nchini Sweden Katika jiji la Malmö. Mlenga shabah huyo hatari anachagua wageni tuu ndio anaowapiga risasi.

Mpaka sasa idadi ya waliolengwa imefikia 15 ndani ya siku tatu..
Hali imezikuwa kuwa tata na wasiwasi sio kwa wageni tuu hata Polisi vichwa vinawauma maana mpaka sasa hawajapata muelekeo maalum ukoje.

Katika Mkoa wa Skåne ndiko kilipo chama cha wasiopenda na wana idadi kubwa sana ya wanachama wao kuliko miji mingine ya Sweden..Kwa habari zaidi soma Aftonbladet.se

Mdau wa Iceland

Thursday, October 21, 2010

onyesho la mavazi la swahili fashion week kuanza novemba 4,2010
Mbunifu wa Mavazi na Muandaaji wa onyesho la mavazi la Swahili Fashion Week,Mustafa Hassanali akizungumza mbele ya wandishi wa habari leo asubuhi ndani ya hoteli ya Southern Sun kuhusiana na uzinduzi wa onyesho hilo litakaloanza kurindima novemba 4 mpaka 6 ndani ya viwanja vya Karimjee hall.Kutoka kulia ni Mratibu wa mitindo Bw.Washington,Muwakilishi wa hoteli ya Southern Sun Bi.Judith Muyo,na kushoto kabisa ni Alex Galinoma kutoka EATV pamoja na Afisa habari wa tamasha la Swahili Fashion week,Bi Saphia Ngalapi.


Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week itafanyika Karimjee Hall kuanzi tarehe 4 hadi 6 November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .

Swahili Fashion Week itawaleta pamoja wabunifu wa mavazi 24 kutoka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili ili kuweza kuonyesha ubunifu wao katika kubuni mavazi ya aina mbalimbali kwa kutumia aina mbalimbali za malighafi.

Wabunifu watakaoonesha mavazi katika Swahili Fashion Week kwa mwaka huu ni pamoja na Ailinda Sawe, Manju Msita, Kemi Kalikawe, Christine Mhando, Shellina Ibrahim, Farha Naaz Sultan, Gabriel Mollel, Robi Morro, Asia Idarous, Zamda George, Khadija Mwanamboka, Jamilla Vera Swai and Made by Afrika. wabunifu kutoka Kenya ni Sonu Sharma, Moo Cow, KiKoromeo, John Kavike na Kooroo, na kutoka Uganda ni mbunifu Stella Atal.

“Pamoja na maonyesho ya mavazi, mwaka huu Swahili Fashion Week itakwenda sambamba na tamasha la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zenye asili ya mswahili kutoka mwambao wa Afrika mashariki”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaaji y tukio la Swahili Fashion Week.

“Tunafungua milango zaidi kwa ajili ya watazamaji wapya wa Swahili Fashion Week, amboa watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali. Tamasha hili ambalo linazileta pamoja bidhaa mbalimbali za sanaa na utamaduni wa mswahili, pia litahamasisha ubunifu zaidi katika bidhaa zinazokwenda sambamba na maisha halisi ya jamii ya watu wanaoongea lugha ya Kiswahili kwa kukutana pamoja na kubadilisha mawazo na kujifunza uzoefu mpya katika masuala yanayohusiana na sanaa kwa ujumla.” Aliaongeza Hassanali.

Pamoja na maonyesho, pia kutakuwepo aina tofauti za burudani kutoka kwa vikundi

Mbalimbali vya muziki, uchoraji wa hina, usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazo washirikisha wabunifu wa mavazi.

Aidha Swahili fashion Week imeandaa aina tofauti za zawadi zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji vya aina mbalimbali vitakavyooneshwa, ikiwa ni pamoja na zawadi ya mwaka kwa mbunifu anaechipukia.

Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery LTD, 1 & 1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.

Tuesday, October 19, 2010

Dr alivyoipasua nzega na kahama kwenye kampeni zake za urais

Dk. Willibrod Slaa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Kahama mjini Kahama, mkoani Shinyanga jana jioni.
Dk. Willibrod Slaa akisalimiana na baadhi ya watawa waliohudhuria mkutano wa kampeni zake kwenya Uwanja wa Sabasaba mjini Nzega jana asubuhi.
Dk. Willibrod Slaa akihutubia katika mkutano wake wa kampeni kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Nzega, Tabora.

mr II nae aendelea kupasua miamba ya kampeni.

Mgombea ubunge wa jimbo la Mbeye Mjini kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu akiwahutumia maelfu ya wakazi wa Mwanjelwa,Mkoani Mbeya hivi karibuni,hiyo ikiwa ni sehemu yake ya lala salama za kampeni ambazo zinaelekea ukingoni kwa hivi sasa.

kampuni ya TCC YAFADHILI MAFUNZO YA MAOFISA WAANDAMIZI WA POLISI MAREKANI

Mkurugenzi wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa watatu wa Jeshi la Polisi waliokabidhiwa tiketi na fedha za kujikimu ili kuweza kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Maofisa wa Polisi utakao fanyika Oktoba 22-28 mwaka huu katika mji wa Oralndo , Florida nchini Marekani.Wengine kutoka kushoto ni SACP.Jamal Rwambow, ACP, Renatus Mbushi,ASP.Emmanuel Mkilia na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Sigara Tanzania, Paul Makanza aliyekabidhi udhamini huo. TCC imekuwa ikiwadhamini maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi kuhudhuria mkutano huu tangu mwaka 2001.( Picha na Executive Solutions.)

meli ya hospitali ya china yatia nanga dar,kutoa matibabu bure kesho.


MKUU wa Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lugalo, Meja Jenerali Salim Salim, akipewa zawadi maalu na Kamanda wa Meli ya China, yenye vifaa na madaktari wa kutoa huduma za matibabu,Bao Yuping, alipotembelea meli hiyo leo katika Bandari ya Dar es Salaam.
MGANGA Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya Lugalo, Meja Jenerali Salim Salim, akionyeshwa machine ya upimaji magonjwa ya moyo iliyomo katika meli ya China, alipotembelea meli hiyo leo, katika Bandari ya Dar es Salaam, ambako imetia nanga ikiwa na madaktari watakaotoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa mbalimbali hapo kesho. Kushoto ni Kamanda wa meli hiyo, Bao Yuping na kulia ni Balozi wa China hapa nchini Liu Xinsheng.Kwa habari na picha zaidi kung'uta hapa.

Saturday, October 9, 2010

hoja ya haja toka kwa US Blogger
Gharama ya kura yangu

Ndugu Watanzania. Mwaka huu wa-Tanzania tumepata tena nafasi ya kufanya maamuzi magumu nchini mwetu, maamuzi ya kuchagua viongozi watakaokuwa na majukumu ya kutuendeleza kama Taifa.

Ninaamini swala la uchaguzi ni zito na muhimu sana na kila mmoja wetu ana wajibu mkubwa wa kuwa makini kwa sababu uzembe katika kupiga kura huzaa uongozi wa kibabaishaji na ni ndoto za alinacha kutegemea viongozi wabovu, wapenda rushwa na wasio na sifa kuleta mabadiliko yoyote.

Natambua kila mmoja wetu ana vigezo vyake vya nani atakayempa kura zake, nimeona niwaeleze vigezo vyangu ili tuweze kubadilishana mawazo.

Urais:
Anayekubali midahalo; Ninaamini Rais anayenifaa ni yule amabaye anaelewa matatizo ya kitaifa na mwenye upeo wa kuelewa nini kifanyike katika kukabiliana na matatizo hayo. Ili niweze kumtathmini na kumpima na wagombea wengine lazima awe tayari kuingia kwenye midahalo ili nikiwa kama mpiga kura nipate nafasi ya kumhoji. Siko tayari kumpigia kura mgombea anayefanya kampeni kama tape recorder, yaani anakuja jukwaani kusema anayotaka yeye tu na kuondoka.

Elimu ya Bure; hakuna taifa linaloweza kuwa na mategemeo ya maendeleo bila ya kuwaelimisha wananchi wake. Tanzania ya leo inakabiliwa na tatizo la masikini kuendelea kuwa masikini na matajiri wanazifi kuwa matajiri, njia muhimu ya kuwakomboa walio wengi ni kuwapa elimu yenye manufaa wananchi wote. Siko tayari kukubali hoja ya kwamba haiwezekani, nataka kiongozi ambaye anathubutu kubana matumizi yasiyo ya lazima ya Serikali kama magari ya fahari ili elimu ipatikane.

Uwajibikaji kifedha; Nataka Rais ambaye hawachekei wahalifu wenye tabia ya kudokoadokoa fedha za umma. Fedha za umma zitumike kwa kile kilichokusudiwa tu na kwa kufuata taratibu zilizopo . Nimechoka kusikia ripoti za kitaalamu zinazothibitisha wizi na Rais hawaagizi wasaidizi wake kuwapeleka wahusika kwenye vyombo vya sheria. Matatizo yetu mengi yangeweza kupungua endapo matumizi ya fedha za umma yangeboreshwa.

Serikali iliyo wazi; nimechoshwa na tabia ya kuendesha kazi za Kiserikali kisiri kama kibaka anayekwenda kuiba usiku wa manane. Nakataka Rais atakayetuletea Sheria inayogusa maswala ya Open Records ambayo inamruhusu kila Mtanzania kupata taarifa zinazohusu maamuzi ya Serikali. Kama Serikali imetoa zabuni kwa kampuni yoyote basi tuwe na nafasi ya kujua undani kama vile makampuni mangapi yaliomba tenda, vigezo gani vilitumika, etc. Kwa mikataba ambayo inaweza kuwa ya siri kama ya kiusalama nayo iwe monitored na kamati ya uchumi ya Bunge ili angalau tuwe na wabunge watakaotuwasilisha kudhitibi utoaji wa zabuni.

Uchumi na Biashara; Kabla ya uhuru tulikuwa ni wazalishaji wa malighafi kwa ajili ya mataifa makubwa, leo hii baada ya karibu miaka 50 bado tunafanya hayohayo. Nataka rais mwenye jibu ya kubadilisha Tanzania kutoka nchi inayozalisha malighafi na kuwa taifa linalozalisha bidhaa za viwango vya juu zilizokamilika.

Serikali na Bunge; Kuna haja ya kuwa na mapinduzi ya katiba. Katiba ina matatizo kadhaa, moja wapo ni hili ya wabunge kuwa mwaziri. Kwa mtizamo wangu hii ni conflict of interest kwa sababu haiwezekani wabunge wajidhibitu wenyewe, tunahitaji clear separation ya hizi nguzo mbili za dola. Mfumo wa sasa hauthamini fedha za walipa kodi, mfano sasa hivi mawaziri wako majimboni kwenye kampeni lakini Serikali inawalipa mamilioni ya mishahara. Wakirudi maofisini Serikalini hawaonekani majimboni mpaka wakati wa uchaguzi ujao wakati wanalipwa fedha kama wabunge. Hawa wanatafuna fedha za bure kwa kuwa haiwezekani wafanye kazi mbili zinazohitaji muda mwingi. Mfumo huu unatumaliza.

Kuimarisha mahakama; leo hii mahakama zetu zinakabiliwa na matatizo ya kdaji kutokana na ukata. Nataka Rais ambaye atahakikisha mahakama zetu zinapata bajeti ya kutosha ili wananchi wapate haki zao katika kipindi muafaka.

Katika nafasi ya Ubunge halikadhalika kura yangu itakwenda kwa Mbunge anayeunga mkono matakwa haya.

Je, wewe una masharti gani kwa anayetaka kura yako?

By US Blogger
Usblogger11@gmail.com
service road barabara ya mandela road
Ankal pole kazi
Naomba kuuliza. Hivi hii sehemu ya barabara service road inamaanisha ku-service vimeo ama vipi. Mfano huyu jamaa ndo kageuza garage hapo. Naomba kugahamishwa
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

Monday, October 4, 2010

Ajali mbaya sana yatokea kinondoni jioni ya jumamosi.
Gari aina ya Subaru lenye namba za usajiri T 193 AZL ikiwa katika hali mbaya sana mara baada ya kupata ajali jioni ya jumamosi maeneo ya Kinondoni,Ubalozi wa Ufaransa.gari hii ambayo ilikuwa ikitokea maeneo ya Kinondoni Morocco kuelekea mjini,ilipoteza muelekeo mara baada ya gari moja kuingia ghafla katika barabara kubwa huku gari hii ikiwa katika mwendo wa kasi sana na kumfanya dereva wa gari hii kushindwa kuikontroo gari hii na kwenda kugonga moja ya nguzo za taa za barabarani na kuifanya ikapinduka.ndani ya gari hii kulikuwemo na watu watatu ambao wawili walijeruhiwa na kukimbizwa hospital na mwingine kufanikiwa kutoka bila jeraha lolote.
Sehemu iliyokuwepo nguzo ya taa za barabarani iliyogongwa na gari hiyo na kuifanya ikang'oka kabisa katika sehemu yake.
Mmoja wa waliokuwemo ndani ya gari hiyo (anaetumia simu) ambaye hakutaka kutaja jina lake akijaribu kuwasiliana na ndugu na jamaa kuhusiana na ajali hiyo iliyowakuta.
Askari wa Usalama barabarani,akipata maenezo mafupi toka kwa mashuhuda wa ajali hiyo.