Wednesday, July 29, 2009

Toyota Pickup for Sale




TOYOTA PICKUP HILUX
YEAR 2003
PETROL
PRICE 16 MIL. FIXED!!
CONTACTS 0754 337957
0715 336063
DAWASCO MAMBO MSWANO
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Vodacom Ephraim Mafuru akizungumzia huduma ya kulipia maji kwa kutumia huduma ya simu ya mkononi M-Pesa wakati wa uzinduzi uliofanyika katika ofisi za Dawasco jana.waliokaa katika ni Mkurugenzi wa biashara wa Dawasco Raymond Mndolwa na Meneja habari wa DAWASCO Shabani Salum.

WATEJA WA DAWASCO SASA KUWEZA
KULIPA BILI ZAO KUPITIA VODAFONE M-PESA

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa mara nyingine imewawezesha wateja wake kulipa bili za maji kupitia Vodafone M-Pesa.Kwa sasa wateja wa vodacom wamewezakulipa bili zao za maji kwa kila mwezi kupitia Vodafone M-Pesa.Ni siku chache tu tangu kutangazwa kwa malipo ya LUKU kupitia Vodafone M-Pesa.

Mkurugenzi Masoko wa vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema katika makao makuu ya DAWASCO, kuwa kwa niaba ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Tungependa kuwakaribisha DAWASCO katika ulimwengu wa Vodafone M-Pesa. Vodafone M-Pesa ilianzishwa mapema mwaka jana(2008) kama huduma ya kusafirishia pesa kutoka kwa mtu mmoja kuelekea kwa mwingine.Huduma hii imeendelea kukua na kupanuka hadi kuwawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili,ada za shule na ulipaji wa mikopo.

Vodafone M-Pesa ni njia rahisi ya kutuma hela kwa kutumia simu za mkononi.Mtandao huu wa Vodacom M-Pesa uliyowawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili zao za maji DAWASCO.

Mafanikio ya huduma hii yamefanikiwa kwa ushirikiano baina ya Vodacom Tanzania na DAWASCO.Kwa Kampuni hii ya simu za mikononi ya Vodacom tunajua huu ni mwanzo tu, Bado tutaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na mashirika mengine katika kukuza na kutoa huduma hii kwa ubora zaidi kwa wateja wetu.alisema Mafuru

Akiongelea huduma hiyo Afisa biashara wa DAWASCO Raymond Mndolwa amesema, Sisi kama DAWASCO tutaendelea kutoa huduma iliyo bora kwa wateja wetu kupitia mitandao tofauti ya mawasiliano.

Tunatumai wateja wetu watafurahia kutumia huduma hii ya kulipa bili ambayo itarahisisha maisha Yao.

DAWASCO imeahidi uboreshaji
zaidi katika huduma zao
mjumbe wa FIFA aliyenyamazisha mgogoro wa TFF na ZFA

Huyu ndiye mjumbe maalumu wa FIFA kwa nchi za kusini mwa Afrika, Ashford Mamelodi ambaye majuzi amefanikiwa kunyamazisha zogo kati ya vyama vya soka vya bara na visiwani (TFF na ZFA) ambapo ZFA walikuwa wakidau kuwa wanachama kamili wa FIFA na si lazima wadandie mgongoni pa TFF.

Mamelodi akasawazisha kwa kusema katiba ya FIFA inatambua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni nchi moja na mwakilishi wake ni TFF pekee na kwamba ZFA haiwezi kamwe kuwa mwanachama wa FIFA kwa mantiki hiyo

onyo!

Uvutaji wa sigara hadharani kama huu ni hatari kwa afya yako na hata kwa wengine.

Ziara ya wanaume TMK Family na Tip Top yafana ile mbaya

Mh Themba ambaye hivi karibuni amezindua albamu yake iitwayo mtoto wa kichaga akiwa amepozi mara baada ya kuikamilisha ziara yao fupi na iliyofana kwa kiasi kikubwa
Chege na Mangwea pamoja
Madee na Berryblack wakiwa wamepozi baada ya kazi nzito
Baada ya mavuno Mkubwa Fella (kulia) akijiachia kimtindo na wanawa mara baada ya ziara yao kufana kwa kiasi kikubwa
Watu walikuwa nyomi ile mbaya
Berry Black toka Zenji nae alikuwepo bara kuwapa tafu wana TMK wanaume Family pamoja na Tip top conections kwenye ziara yao walioifanya hivi karibuni na kufana sana kama uonavyo pichani
Chege Chigunda a.k.a mtoto wa mama said naye akikamua jukwaaani
Keisha akiwajibika vilivyo jukwaani.


UZINDUZI WA ALBUM TATU MH TEMBA INAITWA MTOTO WA KICHAGA ALBUM YA FELLA INAITWA MKUBWA NA WANAWE NA ALBUM YA MADEE INAITWA PESA NA KUTAMBULISHA SINGO YAO MPYA YA TMK NA TIP TOP INAITWA CHAMA KUBWA,TOUR IMEFANYIKA SUMBAWANGA,MBEYA UWANJA WA SOKOINE NA IRINGA UWANJA WA SAMORA.

kwa mtindo huu ajali haziwezi kuisha hata kidogo.!


Ukiangalia mstari wa kati haumruhusu kufanaya hicho anachokifanya !!

NAONGEA NA WEWE VOTE for MWANAFA ft AY on Channel O Music Video Awards 2009


image

Tanzanian Bongo Flava artist Hamis Mwinjuma aka MwanaFA has been nominated by Channel O Music Awards.
Which is gonna be held in Johannesburg South Africa on 29th October 2009,
His video track name NAONGEA NA WEWE featuring AY has been nominated into two categories
The Most Gifted Group (DUO) and The Most Gifted East African Video.
MwanaFa and Ay they begging you to vote so as they can win awards,
Its obviously they can,and by winning this they’ll put up Bongo flava to the map.
Take your time and remember you are vote for our country and our musics,

HOW TO VOTE
To vote, MWANAFA The Most Gifted or Duo must SMS 4E to +27839208400
To vote, MWANAFA The Gifted East Africa Video must SMS 13B to +27839208400 (International SMS rates apply)
or vote on www.channelo.tv (web). Is where you can vote
You can vote as many as you want!
Regards;
MwanaFA & AY…
GOD BLESS BONGO FLAVA

Model ahukumiwa kuchapwa viboko 6 na Faini juu kwa kunywa Pombe hadharani, Malaysia.


image

Mahakama ya Sharia hapa Malaysia imemhukumu Mwanadada Kartika Sari Dewi Shukarno, 32 (Pichani) adhabu ya viboko 6 na faini ya Rm 5000 sawa na USD 1400 baada ya kupatikana na hatia ya kunywa pombe hadharani kwenye ukumbi wa starehe.

Kartika ambaye ni Mwanamitindo maarufu hapa Malaysia, Huku akibubujikwa na machozi alisema anatarajia kukata rufaa kwani kosa hilo kwake ni la kwanza lakini kwa mshangao wa wengi Kartika amesema kuwa ametupilia mbali suala la rufaa kwani ameonelea ni bora atumikie adhabu hiyo ili aweze kuendelea na maisha yake. “anasema rufaa inaweza kuchukua mwaka mmoja hadi miwili kusikilizwa jambo ambalo hana uhakika kama atashinda rufaa hiyo na pia litaendelea kumtesa moyo wake” alisema Mwanasheria wake.

image

Si kawaida kwa hukumu hii kupewa akina mama mara nyingi wamekuwa wakipewa wanaume lakini Hakimu huyo alisema kuwa ametoa hukumu hii ili iwe funzo kwa wengine waumini wa Kiislamu walio na tabia kama ya Kartika.

Ni majimbo matatu kati ya 14 nchini Malaysia yanayotumia kifungu hiki cha hukumu kaika Mahakama za Sharia.

Soma zaidi hapa, hapa na Hapa

Sinywi kilevi AY
Msaanii wa Muziki wa Kizazi kipya ‘Bongo Flava’ Ambwene Yesaya a.k.a AY ambaye ni Balozi wa Malta Guiness nchini Tanzania anataraji kuanza kampeni zake kama balozi baada ya miezi miwili toka sasa.

Balozi huyo wa mika miwili na anaevuda dola za Obama takribani elfu 40 kwa mwaka ameingia mkataba huo na kamupuni ya bia ya Afrika Mashariki EABL ya kuwa hatokunywa pombe (kilevi) ndani ya mika 2.

Mkataba huo unamlazimu AY kutokunywa kilevi chaina yeyote wala kuvuta sigara hadharani na badalayake awe anakunywa Malta Guiness pekee.

Pamoja nae pia yupo DJ na msanii maarufu toka Kenja Kenya Esther Wahome.
Mayala na Pinda
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto) akizugumza na Mtayarishaji Maarufu wa vipindi vya Televisheni na Mshauri wa Masuala ya Siasa katika Ubalozi wa Uingereza Nchini, Pascal Mayalla kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 28, 2009.
Meli yawaka moto Dar es Salaam
Meli ya Mizigo inayodaiwa kuwa ni ya Mfanyabiashara Bakhresa wa Dar es Salaam, Mv Pemba ikiwaka moto asubuhi jana katika mwambao wa Bahari ya Hindi eneo la Bandari zinapoegesha meli za Uvuvi na karibu kabisa na Gati za Boti za Zanzibar.
Jitihada za vikosi vya Zimamoto vya Jiji na Bandari vilifanya kazi ya ziada japo kunusuru mali na meli.

Tuesday, July 28, 2009

Treni ya watalii ilipowasili Dar es Salaam
Treni kitalii ya Rovis Rail kutoka Afrika Kusini imewasili Dar es Salaam katika stesheni ya TAZARA ikiwa na watalii zaidi ya 50. Treni hii itatumiwa na mashabiki na watalii wakati wa michuano ya kombe la Dunia nchini humo 2010. Nawatembeza kuiona ndani na nje.
Mabehewa yake.
maofisa wa TAZARA wakitoka katika mabehewa hayo. Hapai baa, ambapo abiria wanaweza kujipatia vinywaji vya aina zote.
Moja ya vyumba vya mapumziko.
Room ya daraja la pili ipo hivi.
Mhudumu mmoja wapo katika treni hiyo iliyo na mazingira tofauti na zetu tulizonazo.
Hapa ni maliwatoni.
Maofisa wa TAZARA wakiwa katika chumba cha kulala daraja la kwanza.
Kitanda cha daraja la kwanza.
Huu ni mgahawa ndani ya treni
Tunajifunza nini mlio na dhamana hii !!
Asante kwa picha mwanana Father kidevu.
JK awaenzi mashujaa wa vita vya kagera
JK akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakikagua baadhi ya Makaburi ya Mashujaa wa vita vya Kagera huko Kaboya, wilayani Muleba Mkoani Kagera Jumamosi hii. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.

Kwa picha zingine
kiota kipya cha minuso chazidi kushamiri...
kiota kipya cha minuso jijini dar cha mlimani city conference centre kwa nje
lango kuu
ndani sio kubaya...
AJALI YA KOROGWE KATIKA PICHA
HAPA NI ENEO LA KWAKOMBO WILAYA YA KOROGWE ILIKOTOKEA AJALI MBAYA YA BARABARANI AMBAPO BASI LA MOHED TRANS LILIGONGANA USO KWA USO NA LORI LA MIZIGO AMBAPO ABIRIA TAKRIBAN 20 WALIPOTEZA MAISHA YAO HAPO HAPO.
MDAU NJILI MWAKOBA ALYE IPITA ENEO HILO LEO ASUBUHI NA ANASEMA KWA MUJIBU WA POLISI WALIOPO KWENYE ENEO LA AJALI ABIRIA WALIOKUWEMO NDANI YA BASI LA MOHAMED TRANS HAWAKUZIDI 40 AMBAVYO NDIO KUSEMA BASI HALIKUJAA.
POLISI HAO WALIKATAA KUTAJA IDADI YA WALIOKUFA MPAKA SASA ZAIDI YA 28 WALIOFIA ENEO LA TUKIO AMBALO MDAU ALIFIKA KIASI CHA DK.45 BAADA YA TUKIO ILA HALI YA MAJERUHI WENGI IMESEMEKANA SIO NJEMA
SEHEMU YA AJALI JANA ASUBUHI
LORI LA MIZIGO
TELA LA LORI LILILOPATA AJALI
SEHEMU YA MABAKI YA BASI LA MOHAMED TRANS
Picha kwa hisani ya michuzi