Tuesday, July 21, 2009

african lyon timu ya mfano bongo
Mh. Mohamed Dewji akiwa na kocha wa African Lyon Eduardo Almeida toka Ureno
Mkuu , naomba nirushie hii. Jumapili jioni nilienda kuangalia mechi ya African Lyon FC timu iliyopanda daraja msimu huu ikicheza dhidi ya vijana wa Jangwani Yanga.
Mpira uliisha huku Yanga wakilambwa mabao matatu. Kilichonifurahisha ni kuwa timu hiyo haijasajili majina makubwa na wamejikita zaidi kukuza vipaji kwani line up yao ilijaa chipukizi wadogo ambao walionyesha kiwango cha hali ya juu.
Kwa nyepesi nyepesi nilizokuwa nazo ni kuwa timu hiyo ambayo inafadhiliwa na Mbunge wa Singida mjini Mohammed Dewji “ MO” amejenga hosteli bab kubwa kule Mbagala kwa ajili ya vijana hao, na on top of that nasikia anataka kujenga uwanja in coming years.
Na kwa wale tulioangalia mpira jumapili kama vijana hao wakitunzwa vizuri basi watafika mbali. Binafsi siwafagilii Simba na Yanga kwa sababu wanakuwa wanaharibu vipaji vya watoto wengi na hakuna maendeleo tunayoona zaidi ya sasa kuwanyenyekea wachezaji wa kigeni badili ya kuendeleza vipaji vya ndani. Hata Uingereza wanalalamika hilo, taifa lenye ligi inayopendwa kuwa wageni wanaifanya timu yao ya Taifa iwe inalega lega.
Ili mpira wetu ukue timu inabidi zianze kuwekeza kwenye timu za vijana. Wenzetu Uingereza wachezaji lazima wapitie Academy za vijana ukienda Manchester, Liverpool, Arsenal hizo zote zinakuwa na njia za kupata wachezaji wapya.Akina Gerrard, Rooney, Messi wote wamepitia kwenye Academy za vijana ambao wanalelewa vizuri na kuandaliwa mazingira ya kuwa professional footballers.
Hivyo naunga mkono hostel ya African Lyon ambayo imejengwa kwa ajili ya wachezaji ni hatua nzuri kwa ajili ya kuendeleza soka la bongo.

Nikikumbuka enzi za Simba kuitoa Zamalek chini ya uongozi wa Mo, I believe hii African Lyon itafika mbali, na watanzania tuamke na tujaribu kuendeleza soka nchini kwetu kwa kuziunga mkono timu zenye mipango na muongozo. Its time to think beyond Simba and Yanga.
Baada ya kutoka uwanjani nikaenda kwenye tovuti yao na nikacheki habari za kipigo cha Yanga zishawekwa kwenye website yao.

MDAU NV

No comments: