Tuesday, July 14, 2009

kuvuja kwa pakacha....
Mambo Kadidi,
Kwanza naomba nikufahamishe kwamba mie ndio nimesharudi nyumbani na nimeshaanza kuseto. Libeneke sio kali sana kama nilivyokuwa nahofia. Ukiondoa wadau kuwa slow slow katika kila kitu, mambo bado ni mswano. Bongo tamu bwana, asikwambie mtu...Nikikumbuka nilivyokuwa naota kibyongo kwa boxi na sasa mambo tambarare tu. summer time mwaka mzima!

Waama baada ya salamu, leo naomba tukumbushane tulikotoka ambapo kabla ya kuletewa mifuko ya plastiki tulikuwa tukitumia vifungashi kama hili PAKACHA kufungia bidhaa zetu bila kuathiri mazingira yetu. Lakini siki hizi, dah! bila fuko la 'Rambo...'

Mdau Lilly

No comments: