Monday, May 31, 2010

GARI LA RAIS

Mi naogopa kusema, lakini nahisi kuna jambo kwa nini Mkurugenzi wa Mawasiliano alidai kuwa hii ilikuwa pancha wakati gari liling'oka tairi? Kweli kuna usalama kama rais inamtokea hivi sasa tutalaumu ajali za Abood ama Shabiby?
Hayo nimaneno ya mzee wa sumo.
Hii imekaaje !!!


Fundi umeme akichokoa umeme bila kuvaa vifaa vyovyote vya kumkinga Maeneo ya Tandale jijini Dar es salaam. Hapa ya kimkuta ya umeme ndipo atakaposema ninge !!
Tuwe makini jamani na maswala ya umeme maana kwa ufundi huu ndio kulipua nyumba na kadhalika na mjuavyo zima moto inavyo jivuta acha tu .Picha na Mdau Robert Okanda

Thursday, May 13, 2010

Stay blessed and enjoy the seasons of your life.
Different Seasons Flavours
The following pictures are of the same place but taken at different seasons!!
Lessons on Life
You cannot judge a tree, or a person, by only one season,
and that the essence of who they are and the pleasure, joy, and love that come
from that life can only be measured at the end, when all the seasons are up.
If you give up when it's winter, you will miss the promise of your spring,
the beauty of your summer, and fulfillment of your fall.
Moral
Don't let the pain of one season destroy the joy of all the rest.
Don't judge life by one difficult season.
Cameron Waziri Mkuu Mpya


Malkia Elizabeth akisalimiana na waziri mkuu mpya wa Uingereza David Cameron. Du hii tamu sana kweli wenzetu wako mbali kwa kila kitu hapa natumai ingetokea sijui kama huyo alieshindwa angeondoka kama alivyofanya Brown ? Tujifunze jamani maana kungangania madaraka utakukuta Africa. Tubadilike tunaweza kubadilika na kujiletea maendeleo yetu.
Kiota cha maraha club bilicanas
chanusurika kuwa jivu .
kiota maarufu hapa jijini kwa hapa jijini na pia ni cha kimataaifa kwa jina maarufu,Club Bilicanas kimenusurika kuwa jivu usiku wa kuamkia leo mara baada ya moja ya TV zilizowekwa ndani ya club hiyo kuleta shoti na kulipuka kabisa,kitu ambacho kilimpelekea kila mmoja aliekuwepo ndani humo kudhania ni bomu na kuanza kukimbia kutoka nje na kwa kuulinda uhai wake.lakini kwa bahati nzuri wafanyakazi wa jengo hilo walifanikiwa kuwahi kuudhibiti moto huo na kuonyehsa kujali kwa hali ya juu pasipo kujali uhai wao kuwa wanauweka mashakani ila walishirikiana kama mchwa bila kusahau kuwapo hongera sana kwa ujasiri wao.Bendi ya Twanga Pepeta ndio iliyokuwa ikitumuiza hapo siku ya leo katika ambapo kila siku za jumatano bendi hiyo hupiga katika kiota hicho. Mpaka tunaingia mitamboni hatujajua hasara iliopatikana na majeruhi.
Sean Kingston atua kwa ajili ya shoo ya kili award
Sean Kingston mwanamuziki maarufu toka nchini Marekani, ameshatuwa nchi usiku wa kuamkia leo hapa akiwa na Mkurugenzi wa masoko wa TBL,David Minja (kulia) pamoja na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (pili kushoto) wakitokea ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere .
JK na Guebuza wazindua daraja la umoja jana
Na itakuwa historia na kuwa ndio daraja refu kwa nchi hizi kwa sasa .
Daraja la Umoja kwa upande huu kama linavyoonekana pichani mambo sasa yatakuwa swafi zikiisha na hizo sehemu korofi kwa barabara hiyo .
kitu kinavyoonekana kwa juu ila maoni yangu kwa watumiaji wote nikijaliwa na mimi kulitumia ni kulitunza sio tunakuja kuchomoa vyuma kama kwa madaraja mengine yalivyofanyiwa !!
Daraja la Umoja kwa pembeni

Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji wakikata utepe kufungua rasmi daraja la Umoja huko Mtambaswala,wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara jana asubuhi Daraja hili linaunganisha nchi hizi mbili na ni kielelezo cha mshikamano na udugu wa kihistoria uliopo baina ya watu wa nchi hizo.

Daraja hilo lenye urefu wa meta 720 na upana wa meta 13.5 ni kiunganishi kizuri kwa nchi hizi na tunatarajia litatumiwa kwa maslahi ya watu wa Tanzania na Msumbiji, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya barabara. Ni ukombozi kwao.

Wazo hilo lililotolewa na marais waasisi; marehemu Julius Nyerere wa Tanzania na Samora Machel wa Msumbiji mwaka 1975 na kutekelezwa na viongozi waliofuata na kukamilishwa na waliopo sasa.

Wazo limesimamiwa na mkandarasi M/s China Geo- Engineering ambaye alisimamiwa na Mhandisi Mshauri NorConsult kutoka Norway, kwa uvumilivu wao na juhudi kubwa za kukamilisha daraja hilo, ambalo litabaki kuwa alama ya uhusiano mzuri na wa kihistoria wa nchi hizi.

Saturday, May 8, 2010

Hizi zilikuwa heka heka za
mkutano mlimani city !!


Du jamani naona imeishia kati ila kwa kasi walio kuwa wanafanya wangekuwa wamemaliza. Bongo tunaweza kufanya kazi kasi ila mpaka iwepo sababu sijui kwa nini !! Tubadilike huku maeneo yangu yakutafuta riziki lilikuwa linapita gari la serikali sasa ambacho kilikuwa kinanishekesha jamaa alikuwa akitangaza eti tufanye usafi maeneo ya karibu na barabara kwa maana kuna ujio wa wageni nikapata jibu kuwa tunafanya usafi mpaka wageni waje !!
Tubadilike jamani sio zama za kusubiri mpaka vitu vitusukume hatuoni jiji lilivyopendeza kwa muda mfupi kama ikiwa tabia yetu ya ndani kuhusu usafi mambo yatakuwa mswano sana.

Thursday, May 6, 2010

Du mti chali !! round ya mlimanicity (jana)
du ila leo kitu kiko sawa sikuwa na kichukulia picha changu . Hongereni sana wahusika maana jana ulikuwa hivyo leo umesimama kama unavyotakiwa. Na pia usafi uliofanyika katika barabara hii naomba uendelee kwa maana tunaweza jamani hii ni kwa wahusika mnaohusika na mamlaka hizi sitaki kuamini kuwa mkutano ukiisha barabara itaachwa. tubadilike !!

MAISHA YA WAWILI (NDOA)
Ieleweke hii nimeipata mahali naomba nioshee na wadau wote wa haka kablog kangu twende kazi !!!
HIVI karibuni nilitembelea mikoa ya Mwanza, baadaye Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine nilikutana na baadhi ya watu na kuzungumza kuhusu mambo tofauti yakiwemo ya ndoa.

Karibu watu wengi niliokutana nao walizungumzia kero katika ndoa huku baadhi yao wakiomba kujua mbinu za kuachana kutokana na kile walichosema kwamba ndoa zimekuwa ni za shida, badala ya faraja waliyoitarajia wakati wanaingia.

Kaka, mimi ni muumini wako, nimekuwa nikisoma sana vitabu na makala ambazo umekuwa ukiandika kwenye magazeti, niliposikia unakuja, nikaona nije nikuone, alisema mama mmoja ambaye aliomba uandikwe mkasa tu, si jina lake.
Nisaidie la kufanya ili niachane na mume wangu maana sioni faida ya kuwa naye.
Swali:Ulitarajia faida gani wakati unaingia kwenye ndoa?
Jibu: Nipate mtu ambaye naweza kusaidiana naye katika maisha,sasa amekuwa ni kero, mambo mengi anajifanyia, kwa mfano sina kazi, yeye ameajiriwa na pia ana biashara, sijui hata huo mshahara wala chochote kuhusu biashara yake, niko tu nyumbani, maisha yangu siyaelewi yanakoelekea.

Swali: Kwa hiyo kuachana ni tiba?
Jibu:Eeeh, bora nijue moja kwamba sina mtu.
Kuna watu wengi ambao matarajio yao kwenye ndoa yamekwenda tofauti. Tafiti zinaonyesha kuwa hali imekuwa mbaya zaidi siku hizi, idadi ya ndoa inaongezeka.
Huenda wewe ukawa ni mojawapo wa waathirika wa matarajio ya ndoa, ulitarajia mazuri, sasa mambo unaona yanakwenda mrama. Fahamu kuwa wewe si mtu wa kwanza.

Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya ndoa hazina amani au matarajio yaliyokusudiwa. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa chuo kikuu cha Loveology kilichoko eneo la West Hollywood, California, Marekani hakuna ndoa ambayo haina mikwaruzo.

Tofauti iliyoko ni akili za watu waliomo kwenye ndoa, kwamba wengine wanapokuwa na mikwaruzo wanaimaliza mara moja wakati wengine wanaikuza.

Mtafiti maarufu katika masuala ya uhusiano Dk D.Ava, ambaye ni kati ya wakufunzi wa uhusiano anasisitiza kuwa jambo la msingi kwa wanandoa ni kufahamu kuwa mikwaruzo ipo na kinachohitajika ni kwa wanandoa wenyewe kuwa na kawaida ya kukaa pamoja kuondoa tofauti zao.

Aidha utafiti mwingine wa chuo kikuu cha Curtin cha Australia, unaeleza kuwa siri ya wanandoa kuwa na maisha bora, kwanza kujuana kwa kina kabla ya kuanza uhusiano.

Tofauti na ilivyokuwa miaka mingi ya nyuma kwamba watu walikuwa wakijuana kabla ya kuanzisha uhusiano, siku hizi wengi wanakurupuka, na hicho ndicho kinachosababisha ndoa nyingi kuvunjika.

Inasikitisha sana kuona watu waliooana tena wengine kwa harusi za kifahari sana, ndoa zao hazina matunda wala kudumu. Kiapo kile walichokula pale mbele ya Watumishi wa Mungu kwamba tutapendana katika raha na shida kinakuwa batili, leo wala hakikumbukwi tena na badala yake kunatokea vitu vinavyoitwa nyumba ndogo na kubwa.

Kwa Wakristo ambao kimsingi kwao hakuna talaka, baadhi ya wanaume wamekuwa wakihama nyumbani na kuhamia nyumba ndogo au wanafanya siri na wengine wanalala pamoja hakuna tendo la ndoa wala kusemezana. Wengine tendo la ndoa wanapata baada ya kutumia nguvu, maana mwenzake hana hamu naye hata kidogo.

Matajiri, wenye vyeo, wasomi n.k nyumba zao zinatisha. Wengi wao wanaigiza tu kuwa wanapendana lakini hakuna ndoa. Sasa tufanyeje ili kuziponya familia hizi zinazosambaratika.

Inawezekana wewe au mimi ni mmoja wa wenye tatizo hili tufanyeje? Kuna baba mmoja ambaye ameoa lakini akawa ana msichana amempangishia na kumhudumia kwa kila kitu, kanisani ni mzee wa usharika kwa sababu ni tajiri, je wewe kama mwenye kuona hali hii unafanya nini?

Ni watu wangapi wanaimba kwaya leo wanafanya huduma mbalimbali kanisani na hata misikitini lakini nyumbani hakukaliki? Tunawasaidiaje watu wa aina hii au tunaishia kusema chini-chini tu basi? Tafakari chukua hatua.

MUHIMU KUZINGATIA:
*Ni muhimu kwa wanandoa kuepuka mazoea, yaani wawe wabunifu, kwa mfano wanaweza wakawa wanapeana zawadi za kushtukiza, au wanaandaliana safari za kushtukiza, hii inamfanya mwenzi wako aone kwamba unamkumbuka.

*Ni muhimu kuwa muwazi. *Mme/mke amsaidie mwenzake kutimiza malengo yake *Utayari wa kusamehe ni jambo jingine muhimu katika kuimarisha ndoa

*Usikumbushie makosa yaliyopita, lakini zaidi ya yote ukikosea kubali na kuwa tayari kuomba msamaha. *Usilale kabla hujamaliza kulizungumza tatizo au kero inayowasumbua kiasi cha kufanya msielewane.

*Kama kuna umuhimu, wa kupinga hoja ya mwenzako, basi fanya hivyo kwa upendo. *Ndugu yangu mmeoana kwa maana kwamba mnapendana, ni vizuri mshirikishe mwenzake mipangilio yako ya kila siku.

Zaidi ya yote jitahidi kutokasirika au kuendekeza tabia za kununa-nuna, kuna tatizo lizungumzwe yaishe.

Ambacho nataka kifahamike katika makala haya ni kwamba matatizo ni sehemu ya maisha, ndoa kama ndoa ni sehemu ya maisha, elewa kuwa utakuwa na mikwaruzo ya hapa na pale, cha msingi ni kujua namna ya kusuruhisha kasoro hizo, hatimaye muweze kwenda sawa.

Siri moja ya msingi sana katika maisha yetu ni kuhakikisha tunakuwa na mawazo kwamba inawezekana. Ukiamini, kwanza ni jambo la msingi, halafu mambo mengine yanafuatia. Ukiamini kwa uhakika kwamba nataka kuwa fulani, kisha ukaanza kuchukua hatua za kuelekea kule ambako unataka, kwa hakika hakuna jambo ambalo litakushinda.

Ninachotaka kieleweke hapa ni kwamba msingi wa maisha ya watu wengi ni nafsi zao, kama unakata tamaa, ndio kusema ni sawa na kifo, ni sawa na kusema aaah basi inatosha, kwa hiyo inakuwa ni mwisho wa kuendelea kuwaza tofauti juu ya kile ambacho umekuwa ukikiwaza.

Wakati fulani miaka minne iliyopita niliwahi kukutana na jamaa mmoja akawa anaomba ushauri juu ya namna gani anaweza kufanya ili kuhakikisha anaishi vizuri kwenye ndoa yake hasa baada ya kumfuma mkewe akiwa na wanaume wengine katika nyakati tofauti wakifanya ngono.

Watu wengi wanapokuwa kwenye uhusiano na wanapoona wenza wao labda wamekuwa na uhusiano na mtu au watu wengine, wanafikiria kutalakiana, lakini huko ni kukosea, unapaswa kukaa naye na kuzungumza naye, ili kujua msingi wa yeye kuwa vile, kisha angalieni mbele, namna gani mnaweza kwenda mbele katika hali ya mafanikio.

Kabla ya kuwa naye, kwa watu walio wengi ni kwamba waliwahi kuwa na watu au mtu mwingine, ni kweli inauma kusikia au kuona ana mwingine, lakini si sahihi kufikiria kutalikiana, cha msingi ni kukaa na kuangalia ni namna gani uhusiano wenu unaweza kuendelea kuwa mzuri, kwa kuondoa msingi wa mmoja kuwa hivyo, yaani kuanzisha uhusiano na mtu mwingine.

Katika uhusiano kuna mambo mengi ambayo unapaswa kuyazingatia, lakini leo tutayaangalia mambo 20, ambayo naamini kwamba kama kweli utayafanyia kazi kwa dhati, kwa hakika uhusiano wako utakuwa mzuri na wenye kuvutia, wala hutakuwa na majonzi tena, baadhi ya mambo hayo ni yafuatayo;

1. Ufanye ubongo wako kutafakari kwa makini yale malengo ambayo umekuwa ukiyawaza kabla ya kuoana kwenu. Je, umewahi kutaka ndoa ya namna gani na sasa unafanya nini?

Waza namna gani unaweza kuwa na ndoa nzuri. Kwa hakika ukifikiria hilo, utafanikiwa. Maisha yetu yanajengwa na fikra, ukiwaza mabaya, utapata mabaya, ukiwaza mazuri, kwa hakika utayapata.

2. Kama kwa mfano ndoa yako tayari imeingia shida, endelea kutafakari kwanini ina matatizo na nini nifanye iwe nzuri?

3. Zaidi, penda kufanya mazuri kwa mwingine, acha kuwaza aaah mbona mimi namfanyia mazuri, halafu yeye ananifanyia mabaya. Endelea kufanya mazuri mengi kwa mwenzi wako hata yeye anaonekana kufanya mabaya, hatimaye naye atakuwa mzuri, kwa maana ya kukufanyia mazuri pia.

Atawaza aaah huyu mtu mbona namfanyia mabaya tu, wakati yeye ananifanyia mazuri, mwishowe atabadilika, ndivyo inavyoaminika kitaalam.

4. Mfanye mwenzi wako ajione ni mwenye thamani na umuhimu mkubwa katika maisha yako. Je, unamthamini mwenzi wako? Tafakari, chukua hatua.

5. Mara zote tafakari ni nini ambacho nikimueleza mwenzi wangu atakuwa mwenye furaha?

6. Tafakari kabla ya kufanya au kuzungumza jambo. Wengi wa watu wanaharibu uhusiano kwa midomo na mikono yao, wakati mwingine unaweza kufikiri unamfanyia mtu kitu kizuri, kumbe sio.

Ni vizuri sana kulizingatia hili. Wakati mwingine kama huna la kuzungumza, ni vizuri kukaa kimya, kuliko kuzungumza 'utumbo'.

7. Shukuru kwa kile unachofanyiwa. Wakati mwingine yawezekana mwenzi wako anakufanyia kitu au anakununulia kitu, hata kama hukipendi, mshukuru kisha sema;
Lakini ukininunulia na kitu Fulani siku ukipata fedha nitapenda pia Usionyeshe kudharau, hata kama labda amekununulia kitu ambacho kutoka moyoni hujapenda.

8. Uwe msikilizaji mzuri. Tena wakati mwingine kama mwenzi wako anazungumza jambo, tulia msikilize hata kama labda ulikuwa unachezea simu nk. Ni makosa makubwa kwa mfano mwenzi wako anazungumza halafu wewe uko bize na kitu kingine ambacho labda wakati huo si cha lazima kukifanya.

9. Jali hisia za mwenzi wako.

10. Acha kauli za kulaumu au kutusi waziwazi, kama mwenzi wako amekukosea, pata muda wa kukaa naye faragha. Ni makosa makubwa kumtusi au kumsema mtu waziwazi, hapo ndipo huzaliwa mabaya mengi, baadhi yake ni vile unaweza kuona watu wakati fulani wakipigana waziwazi
kitaalam watu huwa hawako tayari kudharauliwa hadharani.

11. Acha kuwaza mambo yasiyowezekana. Kwa mfano ni makosa kuamini kuwa katika ulimwengu huu unaweza kumpata mwanamke au mwanaume ambaye ni msafi au mzuri asiye na makosa kwa asilimia mia. Kama unafikiria hilo, ni vizuri ukakaa pasipo kuoa au kuolewa, kwa sababu hayuko, hata Mungu anajua hilo.

Wakati mwingine baadhi ya mambo si makosa, bali yako tofauti na vile ambavyo tungependa iwe, kwa mfano wako watu wangependa kuona dunia haijaumbwa kama hivi ilivyo leo nk, japo ndio uamuzi wa Mungu.

12. Usitoe menno yenye kusababisha maumivu. Kama inatokea mwenzi wako anazungumza maneno yenye kusababisha maumivu, zungumza maneno mbadala, usikuze maumivu. Ongeeni kama watu mliokomaa, acheni kuendekeza migogoro.

13. Zifahamu vema tabia za mwenzi wako na namna gani unaweza kufanya ili kuhakikisha uhusiano wenu unakwenda mbele.

14. Badala ya kuwa na kitabu cha makosa ambayo mwenzi wako anayafanya, ni vizuri ukawa na daftari la mambo mazuri, ambayo mwenzi wako anakufanyia. Tafakari mazuri, zaidi kuliko makosa.

15. Andika tabia nzuri za mkeo au mumeo, badala ya labda sura yake mbaya nk.
16. Angalia ni namna gani unaweza kumfanya mwenzi wako kuwa na tabia nzuri zaidi ya alivyo sasa.

17. Uwe tiba kwa matatizo ya ndoa na uhusiano wenu kwa ujumla. Acha tabia ya kulalamika, kuipiga kelele ovyo.

18. Kumbukeni nyakati zile za furaha na fikra ambazo mmekuwa nazo kuhusu uhusiano wenu. Ongezeni manjonjo yale ya kupendana, na si kufikiria mabaya tu kama ilivyo kwa baadhi ya watu.

19. Angalieni ni namna gani mnaweza kushirikiana katika kuimarisha uhusiano wenu, pia angalieni namna ya kushirikiana katika kazi mbalimbali hasa biashara nk.

20. Ishi kana kwamba unakufa kesho. Mabaya yaliyofanyika jana acha yabaki kuwa ya jana, wala msiyape nafasi kuendelea kuwaumiza vichwa na akili zenu.

Waza leo na kuendelea mbele, achana na jana. Kumbuka watu walikuwa wanatambaa, leo ni watu wazima wanatembea, maisha ni mabadiliko, mtu anaweza kuwa mbaya leo, kesho akawa mzuri, na kinyume chake


NINATEGEMEA KUWA KWA YEYOTE MWENYE MAWAZO ZAIDI KUHUSU HII KITU AYATOE ILI KUWAPA MWANGA WENGINE AU WENZETU AMBAO WANATEGEMEA KUVUTA JIKO!!!! AU VIPI? KAZI KWENU.

Saturday, May 1, 2010

katiba ya jamhuri ya muungano katika libeneke la wizara ya sheria
Habari kadidi na wadau,
Katiba ya nchi tayari inapatikana katika
tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria
Samahani kwa usumbufu wowote uliotokea, kwa vile ndiyo kwanza na Wizara imeingia katika Libeneke hili.
Tunaendelea kujiweka sawa kadri siku zinavyoendelea.
Mambo mengi tu mazuri yataendelea kuongezwa katika Tovuti hiyo.
Ahsanteni kwa maoni,
Mdau Geofrey Chami
BREKING NYUUUUUZZZZZ: Kapuya atangaza kima cha chini cha mishahara sekta Binafsi.
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya (shoto) akitangaza viwango vipya vya mishahara kwa kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Viwango hivyo vya kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi vinazigusa sekta za Afya,Huduma za Kilimo, Viwanda na Biashara, Mawasiliano, Sekta ya Madini, Bandari na sekta ya Uvuvi, Wafanyakazi wa majumbani,sekta ya ulinzi Binafsi na Hoteli. Habari na Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.


Ufafanuzi wa viwango hivyo.
1. Huduma za Afya - Tshs 80,000/=
2.Sekta ya Kilimo - Tshs 70,000/=
3.Viwanda na Biashara - Tsh. 80,000/=
4. Usafirishaji na Mawasiliano
-Huduma za anga 350,000/=
- Clearing and Fowarding 230,000/=
- Mawasiliano ya Simu 300,000/=
- Usafiri wa nchi kavu 150,000/=

5.Madini - Migodini 350,000/=
- Wachimbaji wadogo -150,000/=
- Wauzaji wadogo na watoa leseni 250,000/=
- Brokers Licenses 150,000/=

6. Maji (Bahari na Uvuvi) - Tsh. 165,000/=

7.Majumbani:
- Majumbani (mabalozi na wafanyabiashara wakubwa)- isiwe chini ya Tsh 90,000/=
- Maafisa wenye sitahili ya kulipiwa huduma hii -isiwe chini ya Tsh.80,000/=
- Wengineo - Tshs 65,000/=

Mahotelini:
- Hoteli kubwa za kitalii - 150,000/=
- Hoteli za kati - 100,000/=
- Hoteli ndogondogo,mabaa, nyumba za wageni na migahawa- 80,000/=

8. Ulinzi Binafsi.
-Makampuni makubwa na makampuni ya kigeni - 105,000/= - Makampuni mengineyo- 80,000/=

9. Sekta nyingine ambazo hazikutajwa - 80,000/=
du hii imekaaje wadau maana mh !!
LIBENEKE LA GREGORYMLAY.BLOGSPOT.COM
Kaka KADIDI hongera kwa kazi ya kuliendeleza libeneke la Jamii.
Naomba unirushie Libeneke langu maalum kwa Wadau wa Teknolojia ya Mawasiliano (IT).

Litakuwa likiwaletea bandika bandua ya IT News n' Tricks za maana, kwa manufaa ya Kuliendeleza gurudumu la IT nchini.
http://gregorymlay.blogspot.com/
--
Thanks & Best Regards,
Gregory Mlay
0713 500 608
Best and Unique Web Design
http://www.greatdesign.co.tz
Two Designers present Tanzania
Origin Africa Designer Showcase









CONTACT PERSON: Mr. Mustafa Hassanali

TELEPHONE NUMBER: +255-78-4303880

EMAIL ADDRESS: media@swahilifashionweek.com

WEBSITE URL: http://www.swahilifashionweek.com

Inaugural “Origin Africa Designer Showcase”

Two Designers present Tanzania

Collection Made from Local Fabrics Made in Tanzania

Inaugural “Origin Africa Designer Showcase” had be held on 28 April 2010 in Nairobi at the Laico Regency. It is hoped that this will promote opportunities for local talent and local manufacturers to work together to develop a strong African fashion industry.

Shamra Shamra za Wold Cup 2010 zinaripuka kila Kona ya duniani






Shamra Shamra za Wold Cup 2010 zinaripuka kila Kona ya duniani

FFU wa The Ngoma Africa Band kutumbuiza Munich! Ujerumani.
mahala: Pfarrheim,St.Joseph, Joseph Platz 1.München,Germany
ile bendi mashuhuri ya mziki wa dansi uko ughaibuni,The Ngoma Africa band ali maarufu kwa majina ya kutisha tisha,kama vile FFU, wazee wa kukaanga mbuyu,
yenye maskani yao uko Ujerumani, watapereka mzuka wao wa dansi mjini Munich
au bayern Munchen,kusini mwa Ujerumani.ambako wamehalikwa kwenda kutumbuiza siku ya Jumamosi 8 may 2010,katika kusherekea "FIFA World Cup 2010" kwa mara ya kwanza mashindano ya kombe hilo kufanyika Afrika.
Jumuiya za mshirika mbalimbali yasio ya Kiserekali ,Kikiwemo chama cha urafiki kati ya wajerumani na tanzania,ndio walioandaa onyesho ilo uko Munich,ujerumani ya kusini,ambako ndipo mjio huo ndio makao makuu ya timu maarufu ya kandanda ya Bayern
Washabiki wa kandanda na washabiki wa mziki wa mataifa mbali mbali watapata
bahati ya kujumuika na kujimwaga uwanjani kwa kusakata mziki wa dansi kutoka
kwao bendi ya "The Ngoma Africa Band".bendi ambayo imezoeleka na washabiki
kwa tabia za kuperekana puta na wa shabiki kwa kutumia mdundo wake wa dansi!
Ni juzi tu bendi hiyo mashuhuri iliachia singo CD yake mpya "Jakaya Kikwete 2010".
Kikosi cha Ngoma Africa band,kitarajiwa kutua mjini Munich kwa kazi moja tu!
nayo ni kuwapa burudani ya kukata na mundu washabiki!Burudani ya pata shika na nguo kuchanika,kila moja na wake!
Wakazi na washabiki wa Muchen aka Bayern Munich kaeni mkao wa kula
pia unaweza kusikiliza mziki wao at http://www.myspace.com/thengomaafrica
Muchen.