Thursday, May 13, 2010

Kiota cha maraha club bilicanas
chanusurika kuwa jivu .
kiota maarufu hapa jijini kwa hapa jijini na pia ni cha kimataaifa kwa jina maarufu,Club Bilicanas kimenusurika kuwa jivu usiku wa kuamkia leo mara baada ya moja ya TV zilizowekwa ndani ya club hiyo kuleta shoti na kulipuka kabisa,kitu ambacho kilimpelekea kila mmoja aliekuwepo ndani humo kudhania ni bomu na kuanza kukimbia kutoka nje na kwa kuulinda uhai wake.lakini kwa bahati nzuri wafanyakazi wa jengo hilo walifanikiwa kuwahi kuudhibiti moto huo na kuonyehsa kujali kwa hali ya juu pasipo kujali uhai wao kuwa wanauweka mashakani ila walishirikiana kama mchwa bila kusahau kuwapo hongera sana kwa ujasiri wao.Bendi ya Twanga Pepeta ndio iliyokuwa ikitumuiza hapo siku ya leo katika ambapo kila siku za jumatano bendi hiyo hupiga katika kiota hicho. Mpaka tunaingia mitamboni hatujajua hasara iliopatikana na majeruhi.

No comments: