Thursday, July 31, 2008

Kipanya na busara zake...

Usafiri Bongo Noma
Tupu..




Shida ya usafiri bongo inazidi kushika kasi siku hadi siku kama muonavyo pichani mdau akila lifti ya bure baaada ya daladala kujaa hii ndio shida wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam wanayopata kila kukicha na kwa wanafunzi ndio usiseme balaa tupu.Asante ya Picha Michuzi

Mwiguni George aliyefika katika eneo na kumsaidia Chacha na wenzake!
Mkazi wa eneo la Pandambili, Mwiguni George aliyefika katika eneo la tukio dakika chache baada ya ajali akieleza hali ilivyokuwa. Wanaosikiliza ni ni Kamanda Peter Kivuyo(pili kulia), Kamanda wa Usalama Barabarani wa Mkoa Vitus Nikata ( wa pili tatu kushoto) na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kongwa Ramadhan Kalowa (wa pili kushoto).
Deus Francis Mallya aliyetoa maelezo yenye utata na sasa watu wanamgeuzia kuwa kuna jambo analificha!

STORI MPYA KIFO CHA WANGWE

Utata umejitokezo iwapo marehemu Mbunge Chacha Wangwe aliyefariki katika ajali ya gari Jumatatu usiku alikuwa akiendesha gari hilo ama la.
Kwa mujibu wa mtu aliyefika katika eneo la tukio dakika chache baada ya ajali hiyo, Mwiguni George alimkuta marehemu Wangwe akiwa katika kiti cha mbele cha abiria huku sehemu ya kichwa chaki kikiwa kimebanwa ubavuni mwa kiti hicho na mlango wa nyuma.
Akizungumza Jumanne mbele ya Peter Kivuyo, Kamanda wa Usalama Barabarani wa Mkoa Vitus Nikata na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kongwa Ramadhan Kalowa, mtu huyo alieleza kwamba alikuta mwili wa marehemu Wangwe ukiwa umebanwa ubavuni mwa kiti na mlango wa nyuma huku mkanda wa usalama katika gari ukiwa bado upo mwilini mwake.
“Nilikuwa nyumbani nasikiliza kipindi cha michezo, mida ya saa mbili na nusu usiku hizi, nikasikia kishindo kikubwa, nikakimbilia eneo la ajali. Nilipofika katika eneo la ajali nilimkuta kijana mmoja akiwa analizunguka gari huku akipiga kelele za kuomba msaada,” alieleza Bw. George.
Hata hivyo, mtu huyo alieleza mashaka yake kuwa kulikuwa na watu watatu katika gari hilo na sivyo wawili kamba mabavyo ilitangazwa katika vyombo vya habari.
Deus Francis Mallya alikaririwa mara mwili wa marehemu ulipofikishwa katika hospitali ya Mkoa ya Dodoma akisema kwamba walikuwapo wawili katika safari hiyo na kwamba marehemu Wangwe ndiye aliyekuwa akiendesha gari.
“Nilisikia katika taarifa ya habari kuwa walikuwa wawili. Marehemu ndiye aliyekuwa akiendesha gari na mmoja ndiyo amepona. Mimi ninamashaka, kwani nahisi kuwa na mtu wa tatu na kwamba marehemu hakuwa anaendesha gari wakati wa tukio,” alisema George.
“Nilipofika katika eneo la ajali kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akiwatawanya watu walioanza kufika kwa ajili ya kutoa msaada wasilikaribie gari. Hata hivyo tulianza kuutoa mwili wa marehemu uliokuwa katika kiti cha abiria upande wa mbele,” alieleza George.
“Nilimvua mkanda wa usalama katika kari ambao bado ulikuwapo mwilini mwake, kisha tukamtoa kupitia mlango wa dereva kwani mlango upande aliokuwa amekaa haukuweza kufunguka,” alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Goerge, hata hivyo, mtu huyo wa tatu alielekeza kutolewa kwa fedha alizokuwa nazo marehemu ndani ya mfuko wa koti, jambo ambalo lilimfanya shuhuda huyo kuhisi kuwa alikuwa pamoja nao.
“Tulianza kutoa vitu vya marehemu, na mtu huyo alielekeza kuwa kuna fedha ndani ya mfuko wa koti,” alieleza na kuhoji kuwa “Sasa mie nikajiuliza kama hakuwa nao alijuaje kuwa marehemu aliweka fedha ndani ya mfuko wa koti,”?
Hata hivyo shuhuda huyo alieleza kuwa wakati pilikapilika zilipokuwa zikiendelea, hakuweza tena kumuona mtu huyo wa tatu, ambaye alitoweka.
Maelezo hayo ya Bw. George yalipelekea Kamanda Kivuyo kuagiza askari waliokuwapo katika eneo hilo kuchukua maeleo ya shuhuda huyo kwa ukamilifu.
“Kwanza nakupongeza sana kwa ujasiri wako, na moyo wa kizalendo wa kutoa msaada kwa marehemu,” Kamanda Kivuyo alimweleza shuhuda huyo.
Maelezo hayo yanaleta mkanganyiko kutokana na taarifa za awali kuwa marehemu Wangwe alikuwa akiendesha gari na kwamba walikuwapo watu wawili katika gari hilo.

Mwananchi limefanyiwa mabadiliko ya sura na hivyo kuwa na kiwango cha juu zaidi na ndio limeingia mitaani na sura mpya. Hapa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL Sam Shollei akiuza gazeti hilo lenye sura mpya katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Jamaa alizikusanyakusanya mia tatu, biashara kweli shughuli kubwa!
Wafanyakazi wote waliingia mtaani kutangaza bidhaa hiyo inayotuweka mjini. mwandishi Oliver Albert anaonekana akinadi gazeti hilo Barabara ya Morogoro maeneo ya Ubungo.
Ukichukulia kuwa mambo yameongezwa jamaa alikuwa anajinoma kwa kusoma mwananchi lenye akili zaidi.

Hata wauzaji wa magazeti walisherehekea kwa kupiga maji kabla ya kazi ya katika sherehe zilizofanyika mikoa mbalimbali nchini kwenye ofisi za Mwananchi. Hawa ni wa Dodoma walisherehekea na Meneja wa mkoa Aidan (Mwenye kamera, sasa hii picha sijui alipiga yeye ama nani?)

Chacha enzi za uhai wake baada ya kunyoa rasta!
Gari alilokula nalo mzinga likiwa linaondolewa barabarani maeneo ya Pandambili, Dodoma juzi.
Mallya, jamaa aliyekuwa na Chacha katika gari lililopata ajali.
Rais kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Chacha.
Gari lililohitimisha maisha ya Chacha likiwa limeharibika vibaya, watu wanajiuliza kumbe huyu mtu hakuwa Fisadi alitumia tu kataksiii wakati wengine wana mashangingi!!!!!!!!

UJUMBE WA UKIMWI

Jamaa wengine message zao zinashangaza hebu cheki hili gari lilivyoandika 'Hata ukipima utakufa tu!'.

SARA RAMADHANI

Haya ndio yaliyomkuta baada ya kuingia marathon!!!!!!!!!!!!!!!
Nilisahau kusema kuw amichuano hii inafanyika mjini Singida na ni ya Kitaifa nchini ila binti huyu Sara Ramadhani wa Arusha alifanya vyema kwa kukimbia mita 5000 na kuibuka wa kwanza.
Mkuu wa mkoa akamvisha medali ya dhahabu lakini baadae jioni akaibuka katika marathon ikawas sooo!!!!!!!!!!! hadi sasa yuko hospitali!!!!

ELISHA MDANI YA UNO


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa DK. Asha-Rose Migiro akiwa na mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC1 Elisha Elia Mwakagali (kushoto) na Afisa wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Maura Mwingira (kulia) baada ya mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulika masuala ya Uchumi na Jamii Jijini NEW YORK nchini MAREKANI hivi karibuni.

MICHUANO YA RIADHA TZ

Kumbe bongo kuna vipaji vya kuttosha jamani yaani watu wanafukuza upepo na michezo mingine ya riadha si mchezo, JK angejua kuwa si football pekee angewekeza na huku. Cheki dada huyu alivyofiti katika kurusha tufe.
Hapa Said Thomas wa Arusha akirusha mkuki jamaa ni mmoja wa wakali ma mchezo huo nchini.
Sasa wanawake mita 100m ndio si mchezo cheki wanavyofanya mambo tofauti ni uwanja tu lakini wakipata zulia sijui tatanzania wanaweza kufanya makubwa sana.
Walioshiriki mita 5000wakifanya warm up kabla ya mpambano.

Wanaume mita 5000 ndio usiseme walikuwa wanawatoka wenzao kama mchezo tu.

MAMBO YA KIPOLISI

Haki ya Mungu niko Singida nimekutana na huyu kamanda wa polisi mkoani huku anaitwa Celina Kaluba nikaogopa kumbe wakinamama nao wako fiti sijui inatakiwa tuwe na IGP mwanameke? Lakini kali kuliko ni Central polisi nimeogopa baada ya kukuta hili Hummer imewekwa sijui imetumika kwa ujambazi ama kwa hela za kifisadi lakini imearrestiwa.! ama matajiri hawaruhusiwi bongo?


Maonyesho ya sabasaba na vituko ni vingi kama huyu Charlie Champlin ambaye alikuwaanafanya mambo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere sema weupe wake umezidi tu!

Yaani kibaka ni kibaka tu! jamaa huyu alifikishwa mahakama ya wilaya ya Tameke kwa kosa la kumchapa mtu panga hakuwa na hofu mpaka anasomewa mashtaka na kurejeshwa rumande alikuwa anajiona shujaa. Imagine ukutane nae mtu kama huyu halafu hana senti mfukoni!

CHAI MAHARAGE

Unguja makubaliano huwa ziko saana lakini hii Chai Maharage imekutwa ikikatisha mitaa ya Dar es Salaam na kula vichwa sijui ndio vinakuja kureplace vipanya ama vipi? Sumatra itabidi wafafanue magari ya abiria ni yapi?
Majengo ya Kale Hatari Tupu
Bagamoyo....


Mtoto wa mtaa wa Mwambao Bagamoyo,akicheza karibu na ukuta wa jengo linalodaiwa kujengwa mwaka 1830,majengo mengi ya kale ambayo yange takiwa kuhifadhiwa na kuwa kumbukumbu badala yake yameachwa na uongozi wa mji huo kama muonavyo pichani na kutishia maisha ya watu,kwani yakianguka ni hatari kwa utalii wa mji huo.Picha ya Mdau Deus Mhagale.
Balozi wa Cuba amtembelea
Rais Karume..


r

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume(Kulia),akizungumza na balozi wa Cuba Nchini Tanzania,Mh Felipe Ruiz O Farril aliyemtembelea Ikulu Mjini Zanzibar na kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.Picha na Ramadhan Othman Ikulu/Zanzibar
Uraia wa nchi mbili
utaangamiza nchi,uzalendo..
-------
MNAOJALI kusoma historia na kazi za uandishi za watu wenye uchungu na nchi yao,
msikieni Shaaban Robert katika shairi lake,
“Fahari ya mtu”,akisema:
“Fahari ya kila mtu,kwanza ni taifa lake,Kutimiza wake utu,
afe au aokoe,Pasipo hofu ya kitu, halipendi liondoke

Fahari ya kila mtu,ya pili nchi yake,Mtu hakubali katu,
kutawaliwa pake,Hilo haliwi kantu,halina heshima kwake.

Fahari ya kila mtu,ya tatu ni nchi yake,Kuwaye chini ya watu,
wageni wa nchi yake,Ni jambo gumu kwa mtu,japo vipi aridhikie,
Pasipo nje. hofu ya kitu,hulipenda liondoke”.
Shaaban Robert.
Ni jambo la kuhuzunisha na kugadhabisha pia,kuona zama hizi,baadhi ya Watanzania wenzetu, hasa wanasiasa,wametekwa nyara na ubepari na mitaji ya kimataifa kiasi cha kupoteza uzalendo na moyo wa kuona fahari kwa taifa lao na kuabudu vya
Bofya na endelea>>>>>
Kimwana wa Face Of Tanzani aelekea
Sauzi Afrika..



Pichani ni Mkurugenzi wa Beautiful TanzaniA Agency,Irene Kiwia,(kushoto),akiwa na kisura wa Tanzania (Face of Tanzania)Emmy Melau(katikati),muda mfupi kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,Dar es Salaam leo.
---
Na Msimbe Lukwangule.
Mshindi wa kwanza wa shindano Face of Afrika,Emmy Melau ameondoka nchini leo kuelekea nchini Afrika kusini ambako amekwenda kufanya kazi katikakampuni ya O Model Africa aliyojiunga nayo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Emmy alipata tiketi ya kuwa kisura wa Tanzania katika shindanolililofanyika hivi karibuni, alifanikiwa kutwaa ushindi huo baada yakuwabwaga wenzake katika hatua ya fainal iliyofanyika jijini Dar esSalaam.Akizungumza katika Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar esSalaam kabla ya kuondoka,Emmy alisema anawashukuru watanzania kwakumuunga mkono wakati wa shindano la kumsaka kisura wa Tanzania nakuwapongeza waandaaji wake kampuni ya Beautiful Tanzania Agency.

Emmy alisindikizwa na baadhi ya ndugu zake,akiwemo mama yakemzazi,Oliver Thomas, mama yake mlezi,Nancy Wilson,na dada yake HappyLaizer,pamoja na mkurugenzi wa Beautiful Tanzania Agency,Irene Kiwiaaliyekuwa amefuatana na Flora Lauro.Emmy aliahidi kufanya kazi kwa bidii zote ili kuliletea sifa taifa la Tanzania kutokana na utendaji wake.
Ya Mungu Mengii.....




An interracial couple from Germany recently welcomed twins into the world,But when brothers Ryan and Leo arrived they had an extra surprise for their parents-they were born with different coloured skin.One is black and the other white.
Toleo la Raia Mwema Wiki Hii...
*Giza nene kifo cha Wangwe



TANGU baada ya habari za kifo kwa ajali ya gari za Mbunge wa Tarime Chacha Zakayo Wangwe (52)zilipofahamika hapa juzi usiku,mji huu ulikumbwa na simanzi kubwa.

Hiyo ilitokana na sababu kwamba wengi wa watu hapa,hata umma wa kawaida,ulimwona Wangwe kuwa mmoja ya wapambanaji wazuri ndani ya kundi dogo la Wabunge wa Upinzani wapatao 43 sasa.
Wangwe alifariki dunia katika eneo la Pandambili,Kongwa,majira ya saa 2.55 usiku akitoka hapa kwenda Dar es Salaam ambako taarifa zinasema alikuwa awahi mazishi ya mwana Tarime mwingine,Bhoke Mnanka,ambaye anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.kwa mengi zaidi juu ya Habari hii na Makala Mbalimbali zilizokwenda shule ikiwemo Rai ya Jenerali Ulimwengu Bofya na Endelea ......>>>>>
MAMBO YA NASIB
MWANUKUZI..
-------

Across the iron barsOutside the windowIt is full of iceDread cold is running To a minus degreeCelciusStanding Inside this babylon cageWatching with a sharpClear visionIs a person in colour BlackIn the white senseOf this wordWings flapping Like an summer birdPeace and cool'pon the blue sky high With the nerves of the deepest Ocean waves
A mahogany soul In a long searchIn a long marchA blood trailDemanding freedomSo real! Picking the flowers of survival Along the wayOn one handA fertile seed Carrying the sprouting spiritsOf African roots on the other Not losing sightOn each passing nightAnd a fastly clearing dayDespite three Solid decades In a white man Oppressor jail!

This poem was composed and a thousand times performed by Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi either solo or with the band.
Rais wa Madagaskar awasili
Nchini...



Rais Jakaya Kikwete (Kushoto)akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Madagaska Mac Ravalomanana mara baada ya kuwasili nchini jana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.Picha na Rwebangira.
Deus Mallya... Sema ukweli utoe utata !!!



Pichani ni Deus Mallya,jamaa aliyekuwa na Marehemu Chacha Wangwe katika ajali mbaya ya gari iliyotokea jumatatu na kusababisha mauti Kifo cha Mh Chacha Wangwe ambapo Utata Mkubwa umejitokeza iwapo marehemu Chacha Wangwe aliyefariki katika ajali hiyo ya gari Jumatatu usiku alikuwa akiendesha gari hilo ama la.

Kwa mujibu wa mtu aliyefika katika eneo la tukio dakika chache baada ya ajali hiyo, Mwiguni George,alimkuta marehemu Wangwe akiwa katika kiti cha mbele cha abiria huku sehemu ya kichwa chaki kikiwa kimebanwa ubavuni mwa kiti hicho na mlango wa nyuma.Kwa mengi zaidi juu ya Habari hii Endelea kwa Kubofya Hapa na Hapa.....>>>>>

Wednesday, July 30, 2008

Kipanya na Busara zake....

Ajali ya Chacha
Wangwe...



Pichani ni gari lililohitimisha maisha ya Mbunge wa Tarime,Mh Chacha Wangwe(Chadema)ambacho kimeshtua Bunge na serikali kutokana na utata wa mazingira ya ajali yenyewe,hivyo kulazimisha uchunguzi.Picha kwa Msaada wa Mdau Faraja Tranquilino wa Dodoma
Mahakama Kuu yatupilia Mbali
Ombi la EATV...





Pichani ni Kundi la Ze comedy wakishagilia kwa pamoja muda mfupi baada ya
Mahakama kuu kutupilia mbali ombi la EATV dhidi ya kikundi hicho..
--------
Na Emmanuel Mrema.
Mahakama Kuu,Kitengo cha Biashara imetupilia mbali pingamizi ya kituo cha televisheni cha EATV dhidi ya kikundi cha wachekeshaji cha Ze Comedy.Akisoma uamuzi huo,Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Catherine Urio alisema pingamizi tatu zilizotolewa na EATV dhidi ya Ze Comedy hazina nguvu ya kuizuia mahakama isiendelee kuisikiliza kesi hiyo.Katika pingamizi hizo,EATV ilidai kuwa walalamikaji hawakuwa na sababu za msingi za kuwashitaki,hawakufuata taratibu za kisheria za kufungua kesi hiyo mahakamani na kwamba kiapo kilichotolewa na mshiriki mmoja kati ya wote hakijafuata taratibu za kisheria.
Jaji Urio alisema pingamizi la kwanza na la pili hajatolea uamuzi kwa kuwa unaingilia kesi ya msingi,lakini la tatu la kiapo kuna matatizo kidogo ambayo kisheria hayasumbui na kisheria inaruhusiwa waleta maombi kurekebisha kiapo hicho ili kesi iendelee kusikilizwa.
“Mahakama imeona ni vizuri warekebishe kiapo kingine ili haki itendeke kwa wote,”alisema Urio.Urio alisema mahakama itapokea maombi ya kiapo hicho kutoka kwa Ze Comedy Agosti mosi na Agosti 7 itapokea kutoka EATV ili iweze kukaa na kutolea uamuzi wake Agosti 15 mwaka huu.EATV inaongozwa na wakili wake Blandina Gogadi na Justin Kimaro wakati Ze Comedy inaongozwa na wakili Peter Swai.
Wasanii hao walikuwapo kusikiliza kesi yao ambao ni Emmanuel Mgaya‘Masanja’,Lucas Mhuvile‘Joti’Sekioni David‘Seki’,Mujuni Sylivery‘Mpoki’,Isaya Mwakilasa‘Wakuvanga’Alex Chalamila‘Mc Regan’na Joseph Shamba‘Vengu’.Kundi hilo lilikuwa likifanya maigizo katika Kituo cha EATV,lakini baada ya kumaliza mkataba wake na kuhamishia matangazo yake Televisheni ya Taifa,TBC1,limeingia katika matatizo baada ya kituo hicho kudai kuwa wao ndiyo wenye hakimiliki ya Ze Comedy.
Kundi hilo ambalo hivi karibuni lilitangaza kudhaminiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji,lilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Kitengo cha Biashara, kuishitaki EATV na pia,likidai kulipwa Sh milioni 200 kutokana na kusababisha kutofanya kazi zake.
tbc yaonesha msiba wa mh. wangwe laivu
wafanyakazi katika chumba cha habari cha dailynews na habari leo wakifuatilia msiba wa hayati chacha wangwe kupitia luninga ambapo tbc imekuwa ikitangaza laivu toka dodoma karibu kutwa nzima jana.
BREKING NYUUZZZZZZZZZZ
waamuzi wa iliyokutaka kuwa mechi ya yanga na simba jumapili neshno wakiangalia saa siku hiyo yanga walipokula kona
kocha mkuu mpya wa simba na kaimu katibu mkuu wakiangalia saa yanga walipoingia kizani
SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI A.K.A TFF IMEIFUNGIA TIMU YA YANGA KUTOSHIRIKI MICHEZO YOYOTE YA KIRAFIKI NA KIMASHINDANO YA KIMATAIFA NDANI NA NJE YA NCHI KWA KIPINDI CHA MIAKA 2 KUANZIA LEO.
KATIBU MKUU WA TFF FREDERICK MWAKALEBELA AMESEMA MCHANA HUU KWAMBA KAMATI YA UTENDAJI, IKITUMIA MAMLAKA YA KIKATIBA YALIYOMO KATIKA IBARA YA 34 (1Q) INAYOELEZEA MAENEO YA MAMLAKA YA KAMATI YA UTENDAJI, IMEAMUA KUTOA ADHABU KALI KWA YANGA ILI IWE FUNDISHO KWA YANGA YENYEWE NA TIMU ZINGINE ZENYE MAWAZO YA KUGOMEA MICHEZO.
KWA MUJIBU WA KAMATI HIYO YA UTENDAJI, YANGA WALIFANYA MAKOSA YAFUATAYO:
1. KUAIBISHA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU, TFF NA NCHI KWA JUMLA
2. KWENDA KINYUME NA TABIA YA UANAMICHEZO
3. KUHUJHUMU KWA KUSABABISHA MAPATO YA MCHEZO KUPUNGUA
4. KUSABABISHA TFF KUKOROFISHANA NA WADHAMINI WALIOWEKEZA PESA NYINGI KUDHAMINI MASHINDANO
5. KUIDHALILISHA TFF KAMA CHAMA MWENYEJI WA MASHINDANO YA UKANDA WOTE WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI NA WAANDAJI CECAFA
6. KUHATARISHA USALAMA WA WATU NA MALI ZAO
7. KURUDISHA NYUMA HATUA NA HARAKATI ZA KULETA MAENDELEO YA KWELI KATIKA SOKA
AIDHA, PAMOJA NA ADHABU HIYO, MWENYEKITI WA YANGA MH. IMNI MADEGA NA KATIBU MWENEZI WA KLABU HICHO FRANCIS LUCAS WAMEPEWA SIKU SABA KUANZIA LEO WATOE MAELEZO NA KUTHIBITISHA MADAI YA KUWEPO KWA MAKUBALIANO YA KULIPWA SH. MILIONI 50 KABLA YA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA.

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza
azindua Kitabu cha Kiswahili cha
“Mbinu za Ujasiriamali” ...
Dr Imani (Kulia)akimkabidhi nakala ya Kitabu cha Ujasiriamali Mh. Mwanaidi Majaar – balozi wa Tanzania London na maafisa wengine wa ubalozi.
Dr Imani akimkabidhi nakala ya kitabu Mh. Bi Suzan Stephen–
Mzee katibu wa CCM London (UK).
----
Kitabu hiki kinaeleza maana na umuhimu wa kupata mafunzo ya ‘Ujasiriamali’.Kinaeleza kuwa ili uwe mjasiriamali mwenye mafanikio huna budi kufahamu mambo
mbalimbali kama vile:

. Mbinu za kukabili ongezeko la ushindani wa kibiashara
.Jinsi ya kuunganisha mtaji na uzoefu wako ili kupata mafanikio zaidi
.Nafasi na umuhimu wa matumizi ya teknolojia na utunzaji kumbukumbu na taarifa sahihi za kibiashara
.Nafasi na umuhimu wa utafiti wa kibiashara kabla na wakati wa kuendesha biashara ili kuongeza ubunifu mpya katika biashara yako.

Kwa hiyo,hiki ni kitabu kidogo kinachotoa mwongozo juu ya mbinu za kuwa mjasiriamali makini na mwenye mtazamo wa kimaendeleo.Kimeandikwa kwa lugha nyepesi na ambayo inaeleweka kwa urahisi.

Dkt Imani Silver Kyaruzi,ni mwalimu na mtafiti wa ujasiriamali na uchumi.
Ana Shahada ya Udaktari wa Falsafa(PhD)ya Uchumi na Ujasiriamali(Chuo Kikuu cha Birmingham)

Shahada ya Pili(MBA)katika Ujasiriamali na Biashara(Chuo Kikuu cha Central England)
na Shahada ya Kwanza (BA Hons) katika Biashara na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Woverhampton.
Wachapaji:
Mkuki na Nyota Publishers
www.mkukinanyota.com
Kwa nakala wasiliana na
Ndugu Deo Simba:
Mkuchika Akisoma Bajeti ya Wizara
Yake Bungeni...
Waziri wa Habari,Utamadunina Michezo,Capt.George Mkuchika akisoma bajeti ya wizara hiyo kwenye ukumbi wa bunge mjini Dodoma Juzi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Kipanya na busara zake ..