libeneke taasisi ya moyo Jana
mtendaji mkuu wa taasisi ya moyo (thi), dk. ferdinand masau, akiongea na waandishi jana hospitalini kwake. chini ni moja ya ambulensi zilizofika tayari kuwahamisha wagonjwa kuwapeleka hospitali ingine.
hadi globu hii ya jamii ilipokuwa inaondoka hospitalini hapo kiasi cha nusu saa iliyopita, hakuna mngonjwa hata mmoja kati ya 11 waliobakia aliyehamishwa na wala hakukuwa na dalili za kutimuliwa kwa wafanyakazi wa thi na vifaa vyao.
asubuhi daktari wa nssf alifika na kuangalia wagonjwa wote ambao inasemekana ni mmoja tu aliyekutwa mahututi. habari zinasema nssf wameshaandaa jopo la madaktari bingwa kadhaa. katika hospitali ya taifa ya muhimbili tayari kuwapokea wagonjwa hao wakati wowote.
akiongea asubuhi dk. masau alisisitiza msimamo wake wa kuiomba serikali kubariki maombi yake ya kuhakikishiwa kupata wagonjwa wa moyo kabla wafadhili wake hawajakubali kumpa pesa za uendeshaji ikiwa ni pamoja na za pango.
amedai kwamba baraka hizo za serikali zimekuwa zikipigwa danadana tokea enzi za mh. anna abdallah alipokuwa waziri wa afya. na kwamba endapo kama angepata baraka hizo mgogoro wake na nssf haikuwa na haja ya kuwepo kwani pesa angekuwa ameshapata.
alisema pia kwamba mwenye nyumba wake hajakamilisha ujenzi wa baadhi ya sehemu za taasisi hiyo kama ilivyoanishwa kwenye mkataba wao, jambo ambalo pia amesema linachangia wafadhili kusita kutoa mkwanja.
nssf wako tayari kuchukua jengo lao wakati wowote kuanzia sasa na kwamba hiyo haikuwa amri yao bali ni ya mahakama baada ya kufuata taratibu zote kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo.
kasema bila baraka hizo wafadhili wake toka marekani na ujerumani wanasita kutoa misaada zaidi kwani uhakika wa kupata wagonjwa wa moyo unakuwa haupo. wadau wengi wameiomba serikali iangalie namna itavyoweza kutatua tatizo hilo bila kuumiza kila upande - nssf, wagonjwa na dk. masau
No comments:
Post a Comment