Tuesday, July 29, 2008

Adadi aagwa Rasmi Jeshi la
Polisi.
Pichani ni IGP Mstaafu Afande Omary Mahita(Kushoto)Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu na kulia Kabisa ni IGP/Mkuu wa jeshi la Polisi wa Sasa Afande Saidi Mwema.
Kutoka Habari Leo
--------------
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Adadi Rajabu, amemwomba Mkuu wa Polisi nchini (IGP),Saidi Mwema,kutoa kipaumbele katika Kitengo cha DCI kwa kuwa ndio uti wa mgongo na kitengo muhimu katika kazi za polisi.Akizungumza katika sherehe za kumuaga zilizoandaliwa na Polisi Kitengo cha DCI Dar es Salaam juzi.


Adadi ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe,alisema idara hiyo ndio inayobeba lawama zote za polisi pindi uhalifu unapotokea.“Idara hii pamoja na kazi ya ukachero ni ngumu na haiwezi kuendelea bila baraka za IGP,mimi nilikuwa namghasi sana bosi wangu Mahita(IGP mstaafu Omari Mahita),inafikia kipindi hadi tunanuniana kwa siku mbili,” alisema Adadi.

No comments: