matukio fainali za kombe la kagame cup 2008

balozi wa rwanda nchini akiwavisha medali washindi wa pili uganda revenue authority

wadau wa castle lager walikuwepo pia

trupu la tbc one likirusha mambo laivu. kipa wa kimataifa wa zamani wa pan african juma pondamali 'mensah' (shoto chini) akiwa na juma nkhamia na crifford ndimbo wakifanya mambo

wanaume tmk walikuwepo kurusha mapanga yao shwaa shwaaa...

washindi wa tatu wa kombe la kagame cup 2008, wekundu wa msimbazi simba sc

mwenyekiti wa simba hassan dalali (mwenye kibandiko) akiwa na vingunge wa friends of simba

balozi wa kenya nchini mh. mbaya (mwenye miwani) akifurahia kombe la kagame na vijana wake wa tusker

warembo wa miss tz 2008 nao walikuwepo kushuhudia fainali za kombe la kagame cup

kocha wa tusker jacob 'ghost' mulee akionesha dola 30,000 keshi alizopokea kwa kutwaa ubingwa wa kombe la kagame cup 2008. rais paul kagame anatoa dola 60,000 kila mwaka kwa ajili ya kombe hilo ambapo mshindi wa kwanza analamba hizo dola 30,000 wa pili anabeba 20,000 na wa tatu anatia kibindoni dola 10,000. tanzania breweries kupitia kilaji chake cha castle lager wametoa milioni 80 pamoja na jezi na vifaa kama wadhamini wakuu

nahodha wa simba akionesha dola 10,000 walizovuna kama washindi wa tatu wa chee baada ya yanga kuingia mitini

washindi wa pili uganda revenue authority kabla ya mchezo wao na tusker waliolala 2-1

waamuzi wa uliokuwa mpambano wa simba na yanga wakipiga jalamba kabla ya mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ambao yanga hawakutokea uwanjani kwa sababu wanazozijua wenyewe

juu na chini ni mabingwa wapya wa kombe la kagame cup 2008 wakifurahia ushindi wao wa bao 2-1 dhidi ya uganda revenue authority


tusker fc kabla ya mchezo wao wa fainali

bosi wa biashara wa tanzania breweries limited david minda akiwavisha medali za ushindi wa tatu wachezaji wa simba sc

rais wa tff sir leodegar chilla tenga akiwavisha medali za ushindi wa pili uganda revenue authority

tunashukuru sana mzee wa fulanazzzzz kwa kazi yako nzuri yakutuhabarisha nakuona ulikuwepo kuleta vitu laivu toka neshno .
No comments:
Post a Comment