Saturday, July 26, 2008

Oliver Mtukudzi awasha Moto
Washington DC..
Yule nguli wa Muziki toka barani Africa Oliver"Tuku"Mtukudzi, usiku wa kuamkia leo amefanya onesho moja kali katika ukumbi wa Zanzibar On The Waterfront hapa Washington DC,onesho linaloonwa na wengi kama moja ya maonesho bora kabisa kufanyika ukumbini hapo mwaka huu.
Akiwa na kundi lake la the Black Spirits,Mtukudzi aliweza kuwakonga washabiki waliofurika ukumbini hapo wengi wao kutoka nchini Zimbabwe si tu kwa uwezo wake mkubwa wa kucharaza gitaa,bali kuimba na kutawala jukwaa katika kucheza muziki.

Washabiki wengi(ambao walikuwa na uwiano mzuri wa mchanganyiko wa rangi na mataifa) walionekana kukunwa na nyimbo nyingi za mkongwe huyo hasa ule wa Ndakuvara ambao kabla yake alielezea historia yake kuioanisha na ya wengi waishio sasa ambao huenda shule bila kujua kile wafuatacho shuleni.

Ktk show hiyo,Oliver alitanguliwa na msanii mcheza ala Nana Frimpong toka Ghana na mwadada chipukizi Loide toka Guinea Bissau na Msumbiji ambao hata hivyo hawakuonekana kuzikonga vyema nyoyo za washabiki.
Bandio M.T

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Dah!! Wakati huooooo bado "mwandishi" wa wenzangu. Sasa hivi naripoti CHOMBONI mwenyeweeeee.
Karibu www.changamotoyetu.blogspot.com