Monday, July 28, 2008

YANGA 'JELA' MIAKA MITATU!
Taarifa rasmi zilizopo hapa mjini ni kuwa CECAFA wameifungia Dar Young Africans kwa miaka mitatu kushiriki mashindano yanayoandaliwa na shirikisho hilo. Tafsiri yangu ya haraka ni kuwa hili ni pigo kubwa kwa kandanda ya Tanzania. Nadhani viongozi wa Cecafa wangetumia busara na kuepuka adhabu hii ambayo kimsingi kuna wasio na hatia waliokumbwa nayo. Hawa ni wachezaji wa Yanga ambao walichofanya ni kufuata maelekezo ya viongozi wao. Wachezaji wale mpira ndio kazi yao. Hawakufanya fujo. Wakuadhibiwa hapa ni viongozi kwa vile ndio waliofanya 'fujo' ya nje ya uwanja.

Mimi ni Simba, lakini katika hili nadhani kuna Simba wengine wengi kama mimi tunaofikiri sawa. Hivyo basi, ni wajibu wetu Wana- Simba kushiriki mapambano ya kuhakikisha watani zetu Yanga wanapunguziwa adhabu hiyo au kuachiwa huru kabisa. Na huu SI UTANI WA SIMBA NA YANGA.

No comments: