Sakata la Ze Comedy Lachukua
Sura Mpya.
*EATV Sasa Waishtaki TBC..
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa(TBC)Bw Tido Mhando akiongea na waandishi wa
Habari Leo jijini Dar es Salaam.
-----------------
KAMPUNI ya Televisheni ya East Afrika (EATV) la Dar es Salaam limelishitaki Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokana na sakata la kundi wachekeshaji la ze Comedy.Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi mkuu wa TBC,Tido Mhando alisema wamepokea barua ya kushitakiwa na kampuni ya EATV kuhusu ze comedy wakati hawafahamu suala waliloshitakiwa na kampuni hiyo.
“Masuala ambayo Ze Comedy wamewashitaki EATV ndio wamewashitaki TBC wakati bado hawajaanza kuwatumia katika kurusha vipindi vyao na hatujui kwanini wametupeleka mahakamani” alisema Mhando“Ni kweli tumeingia mkataba na ze comedy baada ya kumaliza mkataba na EATV na tukazungumza nao kipengele kwa kipengele ili waweze kurusha matangazo yao”alisema Mhando.
Aidha Mhando alisema hawakufanya jambo lolote kwa kurusha matangazo yao baada ya suala hilo kwenda kisheria na wameona wasubiri mahakama itoe maamuzi ya kesi hiyo ili waweze kurusha matangazo yao“Ni hali ya kusikitisha kuona vijana wenye nguvu za kufanya kazi zao za kuwaingizia kipato wanakaa bila ya kuwa na kazi yoyote ya kufanya na watu wachache wanang’ang’ania majina hayo yasitumike na mpaka kufikishana mahakamani”alisema Mhando.
Aidha,Mhndo,alisema wameingizwa katika kesi ambayo hawakuitegemea kwa kuweza kuingia gharama za kutafuta wanasheria wa kuwasaidia wakati kuna kesi nyingine mahakamani ya Ze Comedy kuishitaki EATV.
Kundi hilo linaundwa na wasanii saba ambao ni Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Lucas Muhuvile‘Joti’Sekioni David ‘Seki’,Mujuni Sylivery‘Mpoki’,Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga'Alex Chalamila‘Mc Regan’na Joseph Shamba‘Vengu’Wasanii hao walikuwa wakifanya maigizo katika Kituo cha EATV,lakini baada ya kumaliza mkataba wake,liliingia katika matatizo baada ya kituo hicho kudai kuwa wao ndiyo wenye hakimiliki ya Ze Comedy.
Kundi hilo ambalo karibuni lilitangaza kudhaminiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia channel ya TBC1,lilifungua kesi katika mahakama kuu ya kitengo cha biashara,ikiishitaki EATV,ikidai Sh milioni 200 na kituo hicho kiwaache huru.
No comments:
Post a Comment