Monday, September 29, 2008

Tenga Tena


KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kauli moja leo imempendekeza Leodegar Tenga kugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo utakaofanyika mwezi Desemba mwaka huu.
JK akihitimisha ziara yake marekani
JK akiongea na bwana george haily wa marekani huko washington dc,bwana haily ni kiongozi wa taasisi ya vyuo vya tekinologia barani afrika iliyopewa jina la nelson mandela akizungumza na rais wa kituo cha maendeleo duniani,center for global development,dr.nancy birdsall huko washington mwisho wa wiki
JK akizungumza na waandishi wa habari wa tanzania aliofuatana nao kwenye msafara katika hoteli ya intercontinental jijini new york mwisho wa wiki
Tutatokomeza malaria ifikapo 2015- Rais Kikwete
Na Mwandishi Maalum, New York, Marekani
Tanzania itatokomeza kabisa ugonjwa wa malaria katika miaka saba ijayo, yaani ifikapo mwaka 2015, kwa kutumia njia tatu zilizothibitishwa kimataifa kuwa zinamaliza ugonjwa huo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema leo (Jumapili, Septemba 28, 2008) mjini New York, Marekani.

Vile vile, amesema kuwa ziara yake kwenye Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York imekuwa ya manufaa makubwa kwa sababu Afrika imefanikiwa kuwasilisha sauti yake katika masuala muhimu yanayohusu Bara hili.
Rais Kikwete anaondoka leo kurejea nyumbani.

Akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania walioandamana naye katika ziara hiyo kuhusu mafanikio ya ziara hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa moja ya mafanikio ya ziara yake ni kwamba Tanzania imepata uhakikisho kuwa itaweza kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2015.

Amesema kuwa ahadi mpya za kupambana na matatizo ya Afrika, ukiwemo mwelekeo mpya wa kupambana na magonjwa, na hasa malaria, inayoua watu wengi zaidi katika Afrika, ni moja ya mafanikio ya ziara yake kwenye UN.

“Katika Tanzania, tunapambana na malaria kwa njia tatu zinazokubalika duniani- kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanatumia vyandarua vyenye dawa, tunanyunyizia dawa za kuuwa mbu katika madimbwi ya maji, na pia kuhakikisha kuwa wagonjwa wanapata dawa,” amesema Raia Kikwete katika mahojiano hayo kwenye Hoteli ya Intercontinental, mjini New York, Marekani.
Amesema kuwa njia zote tatu tayari zimeleta mafanikio makubwa Tanzania Visiwani ambako vifo kutokana na malaria vimeteremka mno, kutoka vifo 120,000 hadi 60,000 tu kwa mwaka.

“Na mafanikio hayo yanatokana na matumizi ya asilimia 40 tu ya vyandarua Tanzania Visiwani, lakini Zanzibar haiwezi kutomokeza malaria bila kuhakikisha kuwa Bara nayo inakuwa salama.
Hii ni mara ya tatu, tunafikia hatua ya kutokomeza malaria Tanzania Visiwani na bado ugonjwa huo umerejea kwa sababu Bara haitiliwa maanani,” amesema Rais Kikwete.

Ameongoza kuwa Tanzania inahitaji kiasi cha vyandarua milioni 15 vyenye dawa, kwa kila Mtanzania kulala bila bugudha ya mbu, na kuwa vyanzo mbali mbali vya misaada vimekwishahakikisha kuwa vyandarua hivyo vitapatikana baada ya awamu ya kwanza ya vyandarua milioni 5.2 kuwa vimepatikana.

“Kama mlivyosikia, Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, pekee yake ameahidi kutoa kiasi cha vyandarua milioni 100 katika miaka michache ijayo. Tanzania itanufaika na sehemu na vyandarua hivyo. Pili, tunao msaada wa sekta binafsi ambayo pia itatoa vyandarua. Mpango ni kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2015 ni dhahiri utafanikiwa,” amesisistiza Rais.

Rais Kikwete ambaye aliwasili mjini New York, Marekani Jumapili iliyopita, ameliwakilisha Bara la Afrika kwa maana ya kushiriki katika mikutano kadhaa muhimu ikiwa sehemu ya mikutano ya mwaka huu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Mikutano hiyo ni pamoja na ule iliojadili mahitaji ya maendeleo ya Afrika, Mkutano wa Mjadala wa Baraza Kuu la Mwaka huu, Mkutano kuhusu Malengo la Maendeleo ya Milenia (MDG’s) na yanavyotekelezwa katika Afrika, na mikutano kuhusu Afya ya Mama na Mtoto, pamoja na ule kuhusu malaria.
Rais Kikwete amesisitiza ujumbe wake katika mkutano wa mwaka huu wa Baraza Kuu kuwa sasa ni dhahiri kuwa Afrika siyo Bara lisilokuwa na matumaini, la ovyo, na lenye kukatisha tamaa.

“Nimewaeleza wenzangu kuwa Afrika siyo Bara la ovyo tena. Ni Bara linaloinuka. Demokrasia inapiga hatua, tunaendesha changuzi bora zaidi, hali ya kisiasa imeimarika zaidi, tuna amani ya kutosha, ni kweli bado tunayo matatizo pale Somalia, Darfur, na Mashariki mwa Congo, lakini kwingine hali ni rushwa,” amesema na kuongeza:

“Uchumi wa Afrika unakua kwa asilimia kati ya asilimia tano na sita. Lakini bado bara letu na watu wetu ni masikini. Huu ndio mpaka wa mwisho wa jitihada za binadamu kuleta maendeleo. Kati ya nchi 50 masikini dhalili katika Afrika, 34 ziko Afrika. Kazi bado ni kubwa na hivyo wakubwa hawa wanatakiwa kutelekeza ahadi zao za kusaidia Afrika ambazo wamezitoa katika mikutano mingi tu,” amesema Rais.

Amesema kuwa nchi tajiri duniani zinazo wajibu wa kihistoria na ulazima wa kiroho kuzisaidia nchi masikini, kwa sababu isitoshe ziliahidi zenyewe kutoa misaada hiyo. Hii ndiyo njia pekee ya kuisaidia Afrika kufikia malengo ya Milenia. Kikao cha hapa kilikuwa kinaangalia hili, yaani jinsi ya kuisaidia Afrika kuongeza kasi ya kuweza kufikia Malengo la Milenia.

“Wala siyo kwamba wakubwa hawa wana tatizo la kufanya hivyo. Wanazo pesa za kutosha kuisaidia Afrika kuweza kufikia Malengo haya. Miaka miwili iliyopita aliyekuwa Katibu Mkuu wa UN, Kofi Annan aliomba kiasi cha dola za Marekani bilioni 50 ambazo zingeiliwezesha Bara la Afrika kufikia malengo ya Milenia,”

Ameongeza: “Hiki ni kidogo sana. Fikiria wakubwa hawa wanatoa ruzuku ya kiasi cha dola bilioni 365, kiasi cha bilioni moja kila siku, kuwalipa wakulima wake wasilime chakula cha kutosha. Japan inatoa kiasi cha dola saba kila siku kwa ng’ombe mmoja. Pamba ya Mali haiwezi kuuzika duniani kwa sababu ya pamba ya Marekani inauzwa bei ya chee … hizi ndizo tunaita trade distorting subsidies …”

Rais amesema kuwa kinachoitajika ni utashi wa kisiasa wa kuisaidi Afrika,
kwa sababu kiasi alichoomba Anan ni kidogo sana kulinganisha na ruzuku kwa nchi tajiri kwa watu wao.
Big Brother Africa 3: Lucille OUT!
Namibian favourite Lucille (pictured with presenter kabelo) became the second housemate to be evicted from M-Net’s Big Brother Africa 3 house last night (28 September) during a live broadcast on DStv Channel 198.

Despite not originally being nominated by her fellow housemates, Lucille still found herself on the nomination list after Head of House TK used his power to replace himself with her.

The travel and tourism student spent 35 days in the house – and won more than her share of fans and admirers!

Nigeria’s Uti – also up for eviction with Ricco from Angola – reacted angrily to the news when host KB announced that Lucille was the next housemate to be evicted, smashing a window in the glass house and kicking furniture around until Ricco finally calmed him down.

The live eviction show kicked off with a sultry performance by dynamic Ghanaian duo Irene & Jane – who will also be performing at the Channel O African Music Video Awards in October.

Viewers then got to catch up with the first Big Brother Africa evictee Latoya as she embarked on a busy week of interviews before returning home to a rapturous welcome at the airport in Dar es Salaam. Meanwhile a whistle-stop tour of Angola, Nigeria and Nambia saw friends and family of the nominated housemates sharing their thoughts on their contestants’ chances of being evicted – along with encouragement and well-wishes!

It was a long week on Big Brother Africa – with the task providing the most entertainment as the contestants created their own game show
– Desperate Housemates – ultimately leading to them winning their 100% wager with Big Brother, who congratulated them for their “glitzy and colourful” show.


Tensions were also high, though, after TK had introduced a game earlier in the week which saw the contestants writing anonymous notes about each other which were then read out – leading to some home truths being aired and outrageous reactions shared!

This week also saw an alliance spring up between Lucille, Ricco and Mimi after their discussion about Sheila and how her innocuous actions seem to be adding up to something more sinister. Saturday also saw a visit from SuperSport’s Thomas Mlambo, who commentated on an intra-house soccer match!

But Sunday night was eviction time and KB met the shy Namibian outside the famous Big Brother doors after the big announcement and immediately asked Lucille if she was surprised to be eliminated. “Not at all – I was sure that TK was going to replace himself with me because he still believes I stole his cigarettes!” she said.

With that, attention turned to the house as Ricco and Uti were told that they could re-join their housemates. Whereas the returning contestants had previously been warmly greeted with excited chatter, Uti and Ricco walked through the door without a word – with the housemates clearly shocked to see Lucille had departed. The silence was only broken briefly when Uti kicked over a table.

KB asked Lucille if she felt that Uti was upset because she had left, or because he hadn’t. “I’m not sure,” she said. “Maybe he’s just releasing some stress from the week”.

Lucille then watched her nomination on the screen on stage – to see that only TK had nominated her when he replaced himself with her!

She went on to say, “Big Brother Africa has been such an amazing experience – I’ve met people from so many different countries and tasted all sorts of food,” she said after laughing her way through TK’s clip. “I would have showered naked if I was here ‘til the last – if only my parents weren’t watching!”

Africa voted overwhelmingly to evict Lucille this week – she garnered 11 votes (Botswana, Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, SA, Tanzania, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Rest of Africa), while Uti received 2 (Angola and Namibia) and Rico.

Don’t miss a second of the 24/7 coverage on DStv Channel 198 to see how the contestants adjust to life without Lucille – and don’t forget to catch up on all the latest news by visiting
www.mnetafrica.com/bigbrother.
Athumani apelekwa nje kwa matibabu.
Mhariri wa Picha wa Magazezeti ya HabariLeo na HabariLeo Jumapili, Athumani Hamisi akipandishwa katika gari la wagojwa tayari kwa safarai ya uwanja wa ndege ambako alikuwa akisafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi kufuatia ajali ya gari aliyoipata mamepa mwezi huu Wilayani Kilwa. Athumani aliumia zaidi kifua na shingo alisafirishwa jana kwa ndege ya ATCL.
Blog hii inamuombea kwa Mungu amjalie afya njema haraka na matibabu mema.
Hii ni Dar es Salaam
Mkazi wa Kigogo mwisho Dar es Salaam akichota maji kwenye bomba la maji lililopasuka katikati ya mreji wa maji taka unaopita eneo hilo jana. Uchotaji maji wa namna hii ni hatari maana amiminapo maji hayo katika ndoo nyingine hudondokewa na matone ya maji taka.
futari kwa makamu wa rais
makamu wa rais dk mohamed ali shein na waziri mkuu mh. mizengo pinda wakifuturu jana nyumbani kwa makamu wa rais. wa pili shoto ni kaimu mufti mkuu, sheikh suleiman gorogosi

Saturday, September 27, 2008

chibiriti alipokaribishwa dar
Ndugu yangu kadidi,


Aisee nashukuru safari yangu ya kurudi huku Cesena, Italy, ilimalizika salama na jamaa wote nilikuta wazima. Wanawasalimia sana wadau wote na kutoa pole ya mfungo kwa wote wasio makobe.

Nakutumia picha hii ya mzinga niliolishwa na daladala pale magomeni siku ya pili tu toka nilipofika Dar. Unaweza kuita karibu mgeni maana jamaa alikuwa amechomekewa na daladala ingine, sasa wakati anarudi rivasi, mie ndio nakatiza na hilo gari dogo. Nikasikia kochooo!


Bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila gari iliumia vibaya mlango wa nyuma kama unavyoona. Majeraha yangu makubwa ni hasara niliyoipapa kwani huyo dereva wa daladala alinikomalia na kusema yeye hana kosa ati mie ndiye niliyemgonga.

Zogo liliendelea hadi kituo cha polisi magomeni ambako jamaa alikazania kuwa mimi ndiye mwenye makosa, akisema sheria inatamka wazi kwamba aliyegonga kwa nyuma ndiye mwenye makosa. Nilijitahidi kujieleza, wapi. Ah, nikaachana nao na kurudi nyumbani. Kesho yake nikapeleka gari kwa fundi wa mabodi akaninyooshea na kupiga rangi. Nilitumia visenti kibao.


Namalizia kwa kutoa wito kwa wenzangu wanaorudi nyumbani wawe wangalifu sana na madaladala. madereva wake wengi hawana adabu na sheria za barabarani wao hawazingatii kabisa, tena hata mbele ya askari trafiki.

Ni mimi yuleyule
B. Chibiriti
jengo la benjamin william mkapa magharibi
hivi ndivyo lionekanavyo jengo la benjamin william mkapa towers katika makutano ya mtaa wa jamhuri street na wa azikiwe avenue ambamo hivi sasa makao makuu ya NSSF yamehamia toka kule barabara ya bibi titi road. pia wamo shirika la maendeleo ya petroli na maduka kibao na saluni kama vile mariedo, dekorfraft na kadhalika
ali kiba akiwa njiani kuelekea wichita
ali kiba akiwa universal studios
akiwa na wadau mbalimbali aliokutana nao orlando
ali kiba na wadau na chini kwenye kisiwa cha maraha
Alikiba akiwa ndani ya orlando florida kabla hajaelekea Wichita Kansas ambako ameahidi kufanya mavituzz heavy akishirikiana na chipukizi mwingine kwenye miondoko ya bongo flava" LBT".
Alikiba anapenda kuwashukuru wale wote waliojitokeza kwa mamia kumsupport Washington d.c na Minnesota, Anawahaidi wakazi wote wa kansas kujitokeza kwa wingi kwa sababu amepania kuwasuuza roho zao na show kabambe.
Usingoje kuhadithiwa hakikisha unajionea mwenyewe kipaji cha mwanamuziki wetu kutoka nyumbani.
Wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini kijana huyu anapendwa hivi kila pembe ya dunia. Jibu ni rahisi sana. Ukiwachilia mbali kipaji na uwezo wake mkubwa wa kutawala jukwaa, nje ya jukwaa hana nyodo, halewi wala havuti na pia hufika kazini katika muda aliopangiwa na akianza amenza, tofauti na wasanii wengi wengine wa kibongo ambao hujisahau kwa kujiona wao ni wao.

njia panda masaki


Njia panda masaki hapa panavyoonekana leo mchana, pamebadilika sana baada ya huo mjengo wa nguvu kujengwa eneo hilo.

fiesta 2008 full kujiramba babake



Josee Chamelione toka Uganda akiwa jukwaani kwenye siku ya miss Tanzania 2008,Josee atakuwepo ndani ya tamasha la Fiesta 2008 ambalo safari hii inaanzia octoba nne ndani ya uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Tamasha hilo linalodhamiwa na kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager kauli mbiu yake ni FIESTA JIRAMBE,mbali ya msanii huyo pia atakuwepo Nyota Ndogo kutoka Kenya,Mangwea,Ay,Wanaume Halisi,Wanaume TMK family,Marlow,Mwasiti,Dully Sykes,Mwana FA, Chid Benz wa La familia,Prof Jay,Ray C na wengineo kibao.

precision air yafuturisha mawakala wake wa dar


Imam Haroub Hamis akiomba dua baada ya kumaliza kufturu jioni hii
Kutoka shoto ni meneja wa precision air Bw.Omar Othman,Shehe Haroub Hamis ambaye ni imam wa msikiti wa Ibad Rahman Ilala Bungoni,kaka nanihiiii pamoja na ustadhi Hala wakipata ftari leo jioni viwanja vya karimjee


baadhi ya wageni waalikwa wakipata ftari safi kabisa iliondaliwa na shirika la ndege ya Precision air

Ftari ilikuwa safi kabisa



Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la ndege la precision air pamoja na wageni waalikwa wakipakuliwa ftari jioni hii viwanja vya karimjee


Mambo ya ftari haya ilioandaliwa na shirika la ndege la Precision air leo jioni viwanja vya karimjee




Shirika la ndege la Precision air leo jioni iliandaa ftari kwa ajili ya Travel agents waliopo jijini Dar iliofanyika kwenye viwanja vya Karimjee
















shukrani sana michuzijr.blogspot.com

odinga azindua gazeti la Mtanzania


Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga akiangalia sura mpya ya gazeti la Mtanzania alipozindua juzi.

Friday, September 26, 2008

Kp na busara zake !!

kampuni mpya ya ringtones yazinduliwa jijini Dar





Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya biashara ya mawasiliano ya CELLULANT ,Bw. Jide Harisson akifafanua zaidi juu ya ujio wa kampuni hiyo hapa nchini,ambapo pia alisema kuwa ujio wa kampuni hiyo ni mkombozi kwa msanii wa Kitanzania


Vichwa kutoka Baucha Records (kati ni Mull B wa Clouds fm) wakijadiliana jambo kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa kampuni ya Cellulant jijini Dar


Msemaji wa kampuni ya Cellulant Bw.Khamis Dacota akifafanua zaidi kuhusiana zaidi na huduma za kampuni hiyo,pia alibainisha kuwa wimbo wa msanii atakae ingia nao mkataba utauzwa kwa shilingi 600 na msanii atalipwa shilingi mia


Msanii kutoka kundi la Wanaume Family Rich One akiomba ufafanuzi zaidi kuhusiana na kampuni hiyo ya Cellulant inavyofanya kazi, na kwamba msanii anatalipwa kiasi gani kwa kila wimbo


Msanii wa kizazi kipya kutoka kundi la wagosi wa Kaya.Dr John Mkoloni (mic) akiuliza swali kwa wataalamu wa kampuni hiyo mpya ambayo itaanza kufanya kazi zake muda si mrefu





Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo fupi,ambayo kwa asilimia kubwa walikuwa ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya



Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya biashara ya mawasiliano ya CELLULANT ,Bw. Jide Harisson akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika jana jioni ndani ya hotel ya Southern Sun (zamani Holiday In).Bw Jide alisema kuwa kampuni hiyo ni mpya na itajihusisha na masuala ya kuuza kazi za sanaa kupitia teknolojia ya mawasiliano ambayo ni simu.

Bw.Jide alisema kuwa wasanii wanaweza kuuza na wateja wa simu wanaweza kununua kazi mbalimbali kwa kupitia Cellulant kwa njia mbalimbali kama sms,kupiga namba maalumu pamoja na kuchagua nyimbo.Aidha ameongeza kuwa katika suala la uwazi kwa upande wao ni la asilimia mia moja,na kwamba wana namna ambayo msanii anaweza kuhakikisha nyimbo yake imetumika mara ngapi na kiasi gani anastahili kupata.

RAIS KARUME USO KWA USO NA ODINGA

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE DK AMANI ABEID KARUME, AKISALIMIANA NA WAZIRI MKUU WA KENYA MHE RAILA OMOLO ODINGA,ALIYEFIKA IKULU NDOGO YA MIGOMBANI jana (KATIKATI) NI WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR SHAMSI VUAI NAHODHA


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE DK AMANI ABEID KARUME,AKIFURAHIA JAMBO NA WAZIRI MKUU WA KENYA MHE RAILA OMOLO ODINGA,KATIKA MAZUNGUMZO YAO YALIYOFANYIKA IKULU NDOGO YA MIGOMBANI
PICHA KWA HISANI YA RAMADHAN OTHMAN IKULU/ZANZIBAR

bushoke aja na dunia njia


Msani wa muziki wa kazazi kipya aitwaye Bushoke tayari amekwisha ikamilisha albamu yake mpya itakayojulikana kwa jina la Dunia njia itakayokuwa na jumla ya nyimbo 12.Bushoke mpaka sasa amekwisha zirusha singo zake mbili kwenye vituo kadhaa vya redio hapa jijini na zinafanya vyema ile mbaya,singo hizo ni Dunia njia pamoja na rain on me.


Bushoke amezitaja nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo zilizotawaliwa na maudhui ya taratibu, kwani ndani yake kuna miondoko ya Zouk, RnB, Dansi, reggae na ina zina beat flani za African Rhythm, kuwa ni Acha Mapenzi Yaongee, Dunia Njia, Hallo, Kama, Koka Kola, Mapenzi Yaongee, Nimekuchagua Wewe, Nimeshafika, Wanashindwa Lala, Rain On Me, Angel

kiwanja cha maakuli ifm


Kiwanja cha maakuli chuo cha IFM kilichopo mtaa wa Samora jijini Dar kinavyoonekana leo mchana
Mabomu yatumika Taifa
Askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia (fFU) akifyatua bomu la machozi kuwasambaratisha mashabiki wa timu ya Simba waliokuwa wanataka kuwashambulia waamuzi wa mchezo kati ya Simba na Polisi Dodoma katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka uwanjani 2-2 na kuifanya Simba kushindwa kufurukuta kwa timu zote za Majeshi kwani Ilishafungwa na Prisons 1-0, JK Ruvu 1-0 na sasa Polisi 2-2.
Blue Finance waikabidhi Polisi Pikipiki
Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi Lawrence Masha (kushoto) akipanda moja ya pikipiki zilizotolewa na Kampuni ya BlueFinancil ya Jijini Dar es Salaam kwa Polisi, Katikati ni Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Synarge Navin Kanabar na kulia ni Mkuu wa Polisi Tanzania (IGP) Saidi Mwema. Makabidhiano hayo yalifanyika juzi jijini Dar es Salalaam.
KLYNN NDANI YA LONDON!


KLYNN one of Tanzania'S SONG BIRD for the firtst time in LONDON creation during her stage performance at a CLUB JJ (THE ICE), 17 Haymarket,High Street, Leicester, LEI 3GD on 4 & 5 OCTOBER 2008
K-lynn who real name is Jacquline Ntuyabaliwe was also Miss Tanzania 2000,Perfoming smash hit’s ‘CRAZY OVER YOU’ and More £10 before 12pm, more after.
Mtikila Apigwa Mawe Tarime


Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila (pichani), jana alishambuliwa kwa mawe wakati akihutubia mkutano wa hadhara. Mchungaji Mtikila alishambuliwa mjini Tarime alipokuwa akiwanadi wa gombea wa chama chake wa Udiwani na Ubunge. Habari zilizopatikana kutoka huko jana jioni zilisema kua, Mchungaji Mtikila alipatwa na mkasa huo wakati akizungumzia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime (CHADEMA), marehemu Chacha Wangwe kwamba kilisababishwa na watu fulani. Kwa mujibu wa habari hizo, Mchungaji Mtikila alipata maeraha kadhaa kichwani ambapo alipelekwa katika zahanati ya Tarime na kushonwa nyuzi tatu na Dk. Philemon Hugilo. Aidha, ilielezwa kwamba, Mchungaji Mtikila alilazimika kuvalishwa shuka nyeupe kutokana na nguo zake alizokuwa amevaa, kutapakaa damu. Habari zaidi zilisema watu wanne wametiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo.
SOURCE: Nipashe/Mzee Wa Mshitu
Mgao Wa Umeme Waishtua Serikali


Serikali kesho itatoa tamko kuhusu mgao wa umeme ulioanza juzi, baada ya wahandisi wa umeme kutoka Marekani kuifanyia uchunguzi mitambo ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Songas iliyopata hitilafu na kusababisha kuwepo kwa mgao huo. Wakati hayo yakiendelea, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka Watanzania kuwa wavumilivu na kuvuta subira wakati serikali ikilishughulikia tatizo hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Pinda, alisema kuwa serikali inalishughulikia kwa haraka tatizo hilo ili kuondoa kero kwa wananchi na athari zinazoweza kujitokeza. Alisema kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Songas ina uwezo wa kuzalisha umeme wa kiwango cha megawati 180, lakini kutokana na hitilafu hiyo umeme unazozalishwa kwa sasa ni megawati 140, hivyo kusababisha upungufu wa megawati 40. Pinda, alisema kutokana na tatizo hilo kutakuwa na mgao wa umeme nchi nzima muda wa jioni na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu na kuvuta subira wakati serikali ikilishughulikia. Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alieleza kuwa mitambo iliyoharibika ni mitatu kati ya sita ya kampuni ya Songas na kwamba hali hiyo iligundulika wakati mafundi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) walipokuwa wakiifanyia ukaguzi. Alisema kuwa, baada ya hitilafu hiyo kugundulika, mafundi hao walitoa taarifa kwa kampuni iliyotengeneza mitambo hiyo ya General Electrical (GE) ya Marekani, ambayo nayo baada ya kupata taarifa hiyo iliagiza mitambo hiyo izimwe ili itume mafundi wake kwa ajili ya kufanya uchunguzi na tathmini ya hali halisi ilivyo. ``Siyo kwamba mitambo hii imeharibika kabisa na haifanyikazi, kwani hata wakati ikizimwa ilikuwa inaendelea kufanyakazi kama kawaida, lakini baada ya mafundi wa GE kutaarifiwa kuhusu tatizo lililoonekana wameshauri izimwe ili waweze kufanya uchunguzi,`` Ngeleja alifafanua. Waziri huyo aliongeza kuwa mafundi hao watawasili nchini leo na kwamba baada ya kufanya tathmini na kutoa ripoti yao, serikali kesho itatoa tamko rasmi kuhusu nini kifanyike kutegemea na ukubwa wa tatizo lenyewe. Hata hivyo, Ngeleja alisema ana imani kuwa tatizo hilo siyo kubwa sana na kwamba mgao wa umeme utakuwa si wa muda mrefu kwani serikali inalifuatilia kwa karibu suala hilo. Juzi Tanesco ilitoa taarifa ya kuharibika kwa mashine za kuzalisha umeme za Songas na kusababisha upungufu wa umeme wa zaidi ya megawati 40, hali iliyolilazimu shirika hilo kuanza kutoa umeme kwa mgao kwa maeneo yanayopata nishati hiyo kupitia gridi ya taifa. Taarifa ya mgao wa umeme iliyotolewa jana na Tanesco na kusainiwa na Meneja wa Mawasiliano wa shirika hilo, Badra Masoud, ilieleza kuwa kuanzia jana maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam hayatakuwa na umeme kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 4:30 usiku, isipokuwa maeneo nyeti tu kama Ikulu, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Benki Kuu na viwandani. Ratiba hiyo inaonyesha kuwa leo mikoa saba itakumbwa na na mgao wa umeme. Mikoa hiyo ni Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga, Morogoro na Tanga kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 4:30 usiku na kwamba maelezo kuhusu mgao yatazidi kutolewa kadri siku zinavyokwenda. Kabla Tanesco kutangaza kuwa hakutakuwepona mgao wa umeme kwa taasisi na maeneo nyeti jana, Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) lilieleza wasiwasi kuwa uamuzi wa kuanza kutoa umeme kwa mgao kwa maelezo kuwa hali hiyo ingeweza kuathiti sekta ya viwanda. Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Mtendaji wa CTI, Christine Kilindu ,alipozungumza na Nipashe. Alisema mgawo wa umeme kila unapotokea athari zake ni kubwa katika sekta ya viwanda. Kilindu alisema, mwaka 2006 uliathiri sekta hiyo ingawa hakuweza kutoa takwimu sahihi za athari hizo. Alipoulizwa ni hatua gani ambazo wangeweza kuchukua kama hali hiyo ingejitokeza alisema, angewasiliana kwanza na wananchama wake. Mwaka 2006 nchi ilikumbwa na tatizo hilo baada ya kupungua kwa kina cha maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme ya Mtera, Nyumba ya Mungu na Kidatu. Uhaba huo wa umeme ndio ulioilazimisha serikali kuingia katika mkataba na Kampuni ya Richmond ya Marekani kwa ajili ya kufua umeme wa dharura wa megawati 100. Hata hivyo, baadaye mkataba huo uliiingiza serikali katika hasara na kashfa kubwa, baada ya kampuni hiyokushindwa kuzalisha umeme na kubainika kuwa ilikuwa kampuni bandia. Chini ya mkataba huo wa miaka miwili, Tanesco ilijikuta ikilazimika kuilipa Richmond na baadaye mrithi wake Kampuni ya Dowans kiasi cha Sh. milioni 152 kila siku hata kama hazikuzalisha umeme.
SOURCE: Nipashe
Ujenzi unao bagua
Mkazi wa jiji la Dar es Salaam (kushoto) akimwangalia mtu mwenyeulemavu aliyekuwa akishuka ngazi za kuingilia katika ofisi za Mahakama ya Kazi zilizopo katika jingo la NSSF jijini Dar es Salaam jana. Usumbufu kama huu unawapata walemavu wengi wanaotembelea majengo mengi nchini ambayo hayana njia maalum za kuingilia walemavu ni vyema mamlaka husika na wakandarasi wakazingatia mahitaji ya watu wenyeulemavu katika ujenzi.

Thursday, September 25, 2008

Vihiyo' 8 wa BoT kizimbani




Baadhi ya wafanyakazi 8 wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) waliofikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kistu jijini Dar es Salaam jana kujibu tuhuma za kughushi vyeti wakijifunika nyuso zao kuwakwepa paparazi Septemba 20 wakati wakienda kupanda karandinga tayari kwa safari ya Mahabusu hadi Oktoba 6 shitaka lao litakapo anza kusikilizwa.
Wafanyakazi hao, ni Justina J Mungai, ambaye imeelezwa kuwa ni mtoto wa Joseph Mungai, ambaye amewahi kushika wizara tofauti ikiwemo ya elimu, Christina G Ntemi, Siamini Eddie Kombakono, Janeth John Mahenge, Beatha Constantine Massawe, Jacquiline David Juma, Philimina Philibert Mutagurwa na Amina Mohamed Mwinchumu.