Friday, September 26, 2008

Mtikila Apigwa Mawe Tarime


Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila (pichani), jana alishambuliwa kwa mawe wakati akihutubia mkutano wa hadhara. Mchungaji Mtikila alishambuliwa mjini Tarime alipokuwa akiwanadi wa gombea wa chama chake wa Udiwani na Ubunge. Habari zilizopatikana kutoka huko jana jioni zilisema kua, Mchungaji Mtikila alipatwa na mkasa huo wakati akizungumzia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime (CHADEMA), marehemu Chacha Wangwe kwamba kilisababishwa na watu fulani. Kwa mujibu wa habari hizo, Mchungaji Mtikila alipata maeraha kadhaa kichwani ambapo alipelekwa katika zahanati ya Tarime na kushonwa nyuzi tatu na Dk. Philemon Hugilo. Aidha, ilielezwa kwamba, Mchungaji Mtikila alilazimika kuvalishwa shuka nyeupe kutokana na nguo zake alizokuwa amevaa, kutapakaa damu. Habari zaidi zilisema watu wanne wametiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo.
SOURCE: Nipashe/Mzee Wa Mshitu

No comments: