Saturday, September 20, 2008

mwajabu aibuka na rav 4 mpyaa.!

Bi Mwajabu Hassani Salum akiwa ndani ya mchuma aliojinyakulia kutoka kampuni ya Zain kupitia promosheni kubwa ya magari ya Endesha Ndoto Yako 2,

Meneja masoko wa Zain Tanzania Kelvin Twissa akimkabidhi ufunguo wa gari jipya aina ya Toyota RAV 4, mshindi wa sita wa promosheni kubwa ya magari ya Endesha Ndoto Yako 2, Mwajabu Hassan Salum, katika hafla iliyofanyika jijini Dar leo



Zain yakabidhi Rav 4 kwa Mwajabu

* Ni muuza mbao wa Keko Toroli
* Ni mshindi wa sita wa Endesha Ndoto 2
Septemba 18, 2008
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania imemkabidhi gari jipya aina ya Toyota RAV 4, mshindi wa sita wa promosheni kubwa ya magari ya Endesha Ndoto Yako 2, Mwajabu Hassan Salum, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam (Alhamisi, Septemba 18, 2008).

Mwajabu mwenye umri wa miaka 48 ambaye ni mkazi wa eneo la Keko Toroli wilayani Temeke, Dar es Salaam, alikabidhiwa gari hilo na Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa.

Mwajabu, ambaye kazi yake ni kuuza mbao, ndiye aliibuka mshindi katika droo ya sita Agosti 18, mwaka huu.
Promosheni hiyo inahusisha magari 11 yanayotolewa na Zain Tanzania kwa kipindi cha mwaka mzima.

Akiwa na uso uliojaa tabasamu na bashasha, Mwajabu alikabidhiwa gari hilo lenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 40, mbele ya umati wa watu waliojitokeza kwenye eneo lake la biashara, kushuhudia makabidhiano hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya.

“Kama mnavyofahamu Zain Tanzania bado inaendeleza jitihada zake za kubadilisha maisha ya wateja wake kwa kuwazawadia magari mapya kutoka Toyota Tanzania yakiwa yamesajiliwa kwa jina la mshindi na kulipiwa ushuru na bima zote husika. Zain, kampuni namba moja ya simu za mkononi inayotoa huduma katika nchi 22, inaendesha promosheni ya Endesha Ndoto 2, tutakabidhi jumla ya magari 11 mapya kwa Watanzania wenye bahati likiwemo jipya la kifahari aina ya Toyota Land Cruizer, ” alisema Twissa.

“Mwajabu tumemkabidhi akiwa mshindi wa sita wa RAV 4 na Jumatatu (Septemba 22, 2008) saa 5 :00 asubuhi tutamchagua mshindi wa saba wa RAV 4 ofisi za makao makuu ya Zain na tunawaomba wateja wetu wasizime simu zao ili wasipoteze bahati yao ya kunyakua gari,” alisema Twissa.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ufunguo na kadi ya gari hilo lililovuta umati mkubwa wa watu kulishuhudia, Mwajabu
, alisema anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kutimiza ndoto yake ya kumiliki gari lake binafsi kutokana na kushinda bahati nasibu hiyo ya Zain.

"Kwa kweli nina furaha isiyo kifani, pia sina budi kuishukuru Zain kwa kunitimizia ndoto yangu... hivi sasa nitatulia kwanza, nikae chini na familia yangu kabla ya kuamua nifanyie nini hilo gari," alisema Mwajabu.
Mwajabu ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja na wajukuu wawili, alitoa mwito kwa wateja wengine wa Zain kutokata tamaa bali waendelee kushiriki, watafanikiwa kutimiza ndoto zao.

"Nawashauri watu wajiunge kucheza bahati nasibu mbalimbali zinazoendeshwa na Zain, wajue kwamba wanaobahatika si matajiri tu, bali hata masikini na wenye vipato vya chini wanashinda," alisema Mwajabu na kubainisha kwamba licha ya kunyakua gari hilo la RAV 4, hataacha kazi yake ya kuuza mbao, kwani ndiyo iliyomwezesha kununua simu na vocha zilizompa ushindi wa gari hilo.

Promosheni ya Endesha Ndoto ni sehemu ya programu endelevu ya Zain Tanzania. “Lengo letu ni kuboresha maisha ya wateja wetu na kuwafanya waishi kwa raha zaidi kwa kuzingatia kauli mbiu yetu ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa),” alisema Twissa.

Mpaka sasa droo ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain imekwishawawezesha watu sita kuibuka washindi wa magari aina ya RAV 4. Mshindi wa kwanza alitoka Dar es Salaam, wa pili alitoka mkoani Mbeya, wa tatu Iringa, wa nne Pwani, wa tano Tanga na wa sita Dar es Salaam.

Ili kushiriki katika promosheni ya Endesha Ndaoto 2, mteja anapaswa kutuma sms ya neno ndoto kwenda nambari 100 na atakuwa ameingia rasmi kwenye promosheni hiyo.

Mbali ya zawadi ya magari, Zain pia inatoa zawadi nyingine anuwai kupitia Ndoto Pointi. Kila mara mteja wa Zain anapozungumza anajisogeza karibu na Ndoto Pointi. Kwa kila Tsh 500 anayozungumza anajipatia ndoto pointi moja.

“Mteja akifika kati ya Ndoto Pointi 1,000 hadi 3,000 anajishindia kufurishi cha zawadi kutoka Zain, akifika Ndoto Pointi 3,001 hadi 5,000, anajishindia simu mpya aina ya Nokia 1110i. Mteja akifika pointi 5,001 hadi 7,001 anajishindia simu aina ya Nokia 1650 wakati pointi 7,001 hadi 9,000 anajinyakulia Nokia 5310 au Ipod.
Pointi 9,001 na kuendelea mteja anajishindia simu ya kisasa ya Blackberry bure, alisema Twissa.

No comments: