Wednesday, September 17, 2008

Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni
Awakana Walimu 200...
Picha juu ni Baadhi ya Walimu wakiwa nje ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispa ya Kinondoni
Muda mfupi kabla ya kutembea kwa Mguu mpaka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambako kote walikanwa kwa madai kwamba hawastahili kupewa Malipo Yao.
------
SIKU moja baada ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuwakana walimu 200 waliopangiwa wilayani kwake,Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mwantumu Mahiza, pia amewakana akisema hawapaswi kulipwa na kwamba,kile walicholipwa ni msaada,huku mkurugenzi akifuta kauli ya kuwakana.

Hayo yametokea siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka walimu wasiokuwa na ajira wamwone ili awapatie ajira.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Waziri Mahiza alisema kuwa, walimu hao hawastahili kulipwa mishahara kwa kuwa hawako kwenye orodha ya malipo kutokana na baadhi yao kutokuwa na vibali vya kazi.
Alisema mshahara wa mwezi mmoja waliopewa,ambao Mkurugenzi wa Kinondoni alisema kuwa ulitolewa kwa makosa na ataufuatilia ili ukatwe kwenye mishahara ya walimu hao,ulikuwa msaada kwa ajili ya kuwawezesha kumudu gharama za maisha na si haki yao, hivyo wanapaswa kuendelea kuvuta subira ili utaratibu ukamilike.

"Kuchelewa kwa walimu hao kupata mishahara kumetokana na kuchelewa kupata vibali vya kazi. Baadhi yao walipata vibali hivyo Agosti 27 mwaka huu na wengine bado hawajapata," alisema Mahiza.Bofya na Endelea....>>>>>>

No comments: