Friday, September 19, 2008

tbl yahujumiwa kweupeeee

kwa kile kinachoonekana kushindwa gemu inasemekana kuna baadhi ya mahasimu wa kampuni ya kilaji nchini TBL wamekuwa wakiihujumu kwa kufuta matangazo ya biashara kwenye sehemu kadhaa nchini, hasa mjini moshi na a-taun kama inavyoonekana kwenye picha hizi zilizoletwa na mdau wa huko. kitendo hiki haramu na cha aibu kimelaaniwa sio tu na TBL bali pia walaji wa bidhaa zake ambao kwa hasira wamesema wataendeleza libeneke na TBL hadi kieleweke. wamedai kuwa mtu ukishindwa gemu hii tafuta mbinu ingine na sio hujuma

No comments: