Wednesday, September 17, 2008

mwana FA azushiwa kifo!


Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA amezushiwa habari za kifo kuwa amefariki,habari hizo ambazo zimesambaa haraka kiasi hata baadhi ya mitandao kuripoti habari hiyo kuwa mwana FA hatunaye tena,habari ambazo si za kweli.Kadidi2 ilizipata habari hizo na kushituka sana! Katika kupata ukweli wa mambo Jiachie iliwasiliana moja kwa moja na Mwana FA,ambapo alikanusha vikali na kusema kuwa yeye ni mzima na anaendelea vyema kabisa."Watu wanazusha tu mambo kwa nini wasiwasiliane na mimi wakajua ukweli badala ya kuandika habari ambazo si za kweli" alisema Mwana FA kwa kuhoji.

Habari ndiyo hiyo FA yuko fiti

No comments: