Friday, September 26, 2008

kampuni mpya ya ringtones yazinduliwa jijini Dar





Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya biashara ya mawasiliano ya CELLULANT ,Bw. Jide Harisson akifafanua zaidi juu ya ujio wa kampuni hiyo hapa nchini,ambapo pia alisema kuwa ujio wa kampuni hiyo ni mkombozi kwa msanii wa Kitanzania


Vichwa kutoka Baucha Records (kati ni Mull B wa Clouds fm) wakijadiliana jambo kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa kampuni ya Cellulant jijini Dar


Msemaji wa kampuni ya Cellulant Bw.Khamis Dacota akifafanua zaidi kuhusiana zaidi na huduma za kampuni hiyo,pia alibainisha kuwa wimbo wa msanii atakae ingia nao mkataba utauzwa kwa shilingi 600 na msanii atalipwa shilingi mia


Msanii kutoka kundi la Wanaume Family Rich One akiomba ufafanuzi zaidi kuhusiana na kampuni hiyo ya Cellulant inavyofanya kazi, na kwamba msanii anatalipwa kiasi gani kwa kila wimbo


Msanii wa kizazi kipya kutoka kundi la wagosi wa Kaya.Dr John Mkoloni (mic) akiuliza swali kwa wataalamu wa kampuni hiyo mpya ambayo itaanza kufanya kazi zake muda si mrefu





Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo fupi,ambayo kwa asilimia kubwa walikuwa ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya



Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya biashara ya mawasiliano ya CELLULANT ,Bw. Jide Harisson akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika jana jioni ndani ya hotel ya Southern Sun (zamani Holiday In).Bw Jide alisema kuwa kampuni hiyo ni mpya na itajihusisha na masuala ya kuuza kazi za sanaa kupitia teknolojia ya mawasiliano ambayo ni simu.

Bw.Jide alisema kuwa wasanii wanaweza kuuza na wateja wa simu wanaweza kununua kazi mbalimbali kwa kupitia Cellulant kwa njia mbalimbali kama sms,kupiga namba maalumu pamoja na kuchagua nyimbo.Aidha ameongeza kuwa katika suala la uwazi kwa upande wao ni la asilimia mia moja,na kwamba wana namna ambayo msanii anaweza kuhakikisha nyimbo yake imetumika mara ngapi na kiasi gani anastahili kupata.

No comments: