Makala ya Leo...
*Ya Zimbabwe Tumeyaona,Sasa bado ya Zanzibar
*Ya Zimbabwe Tumeyaona,Sasa bado ya Zanzibar
WANANCHI wa Zimbabwe jana walishuhudia wanasiasa viongozi wa vyama viwili vya siasa nchini humo, Rais Robert Mugabe wa Zanu PF na hasimu wake wa miaka mingi,Morgan Tsvangirai,wakitiliana saini mkataba wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
Makubaliano hayo ambayo yamefikiwa chini ya Uenyekiti wa Rais Thabo Mbeki,wa Afrika Kusini,yamefikiwa baada ya serikali ya Rais Mugabe kuridhia uamuzi wa kukubali,Tsvangirai awe Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Tukio hili linakuja miezi kadhaa baada ya viongozi wa Kenya,Rais Mwai Kibaki na hasimu wake wa wakati huo,Raila Odinga,kufanya kile kile kilichofanywa na Mugabe na Tsvangirai jana.
Kwa maelezo yoyote yale,japo ni kweli kwamba mazungumzo yaliyofanikisha tukio la jana yalichukua muda mrefu hata kufikia hatua ya kukatisha tamaa,ni ya kutia moyo na yaliyojaa faraja.
Tunasema ni ya kutia moyo,Kwani tunaamini makubaliano hayo ya jana kati ya Mugabe na Tsvangirai yanaweza kwa kiwango kikubwa kuanza kuwapunguzia makali ya kimaisha wananchi wa taifa hilo la kusini mwa Afrika,ambalo maisha ya kijamii na kiuchumi yamekuwa ni ya tabu sana.Bofya na Endelea......>>>>>>>
No comments:
Post a Comment