Saturday, May 31, 2008

Ajali Ya Ndege


Honduras jana Ijumaa. Ndege hii katika kutua imeacha njia yake na kuingia barabarani. Watu wanne wamefariki dunia na wengine 81 kunusurika. Naam. Ugumu wa ndege ni kwenye kupaa, kutua itatua tu,kwa njia moja au nyingine.

Japan yamwaga Bilioni 21.3 Kuboresha Umeme jijini .....


Pichani ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi,Gray Mgonja
------------
SERIKALI ya Japan imeisadia Tanzania sh bilioni 21.3 kwa ajili ya mradi wa uboreshaji na upanuaji wa miundombinu ya usambazaji wa huduma ya umeme katika Jiji Dar es Salaam.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kufanyika kwa makubaliano na utiaji saini wa mradi huo, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja na Balozi wa Japan nchini, Makoto Ito, wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kuhusu mradi huo, Balozi Ito alisema umebuniwa kwa sababu upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme utasaidia kuondoa umasikini na kukuza uchumi.
Alisema Dar es Salaam ni kitovu cha biashara, hivyo jiji linahitaji umeme wa uhakika wakati wote.

“Msaada huo umetolewa ili kuweza kutatua tatizo la umeme katika Jiji la Dar es Salaam na kukipunguzia mzigo kituo kidogo cha huduma ya umeme cha Ilala,” alisema Balozi Ito.
Alisema fedha hizo zitatumika kuboresha kituo kidogo cha Ubungo na ujengaji wa kituo kingine kama hicho katika eneo la Oysterbay. Ito aliongeza kuwa msaada huo utakuwa ni wa awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza inaanza mwaka huu, ya pili itatekelezwa mwaka ujao na ya tatu 2010.

Kwa upande wake, Mgonja aliishukuru Japan kwa kuendelea kutoa msaada na kuongeza kuwa fedha hizo ni nyongeza ya msaada wa kwanza wa kuisaidia Tanzania kuboresha huduma hiyo nchini. Alisema msaada huo utasaidia kuboresha huduma za umeme katika maeneo ya Mikocheni, Oysterbay, Msasani, Magomeni, katikati ya jiji, Kariakoo na Kurasini. Habari hii na kutoka ukumbi wa habari Maelezo

Mtanange wa Taifa Stars na Mauritius leo umeshafanyika ......


Mwenyekiti wa baraza la michezo nchini (BMT )Idd Kipingu,katikati,akifafanua jambo kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha watanzania kwenda kuishangilia timu hiyo kwenye pambano la kimataifa na Mauritius litakalofanyika jumamosi wiki hii kwenye uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilifanyika kwenye ofisi za shirikisho la soka Tanzania (TFF) jana,kushoto ni Afisa habari wa Kampuni ya Serengeti Bia(SBL) Tedy Mapunda na kocha mkuu wa Stars Macio maximo.

Marc Anthony » I Need You Lyrics

“I Need You”
From the day that I met you girl
I knew that your love would be
Everything that I ever wanted in my life
From the moment you spoke my name
I new everything had changed
Because of you I felt my life would be complete

[Refrain]
Oh baby I need you
For the rest of my life girl I need you
To make everything right girl
I love you
And I’ll never deny that I need you

Nothing matters but you my love
And only God above
Could be the one to know exactly how I feel
I could die in your arms right now
Knowing that you somehow
Would take my soul and keep it deep inside your heart

[Repeat refrain]

Girl your love to me feels just like magic
When you smile you have total control
You have power like nothing I’ve felt before
I’ve let all of my feelings show
Cuz I want you to know that.. I need you

I need you, for the rest of my life girl
I need you, say that you’ll be my wife oh
I love you, Wont you marry me marry me
Oh I need you (nobody but you)
Oooh I need you, for the rest of my life
Oh I need you (nobody but you)
Wont you marry me marry me
I love you, I really need ya baby (I really need nobody but you)
I need you
Girl I really need… need you girl I really need you need you (I need you)
Oohhh baby I love you (I love you)
I need you, Girl I really need ya need ya … oh baby…
Wont you marry me (I need you)
Wont you marry me marry me
I love you.. oohh ..
I need you... (I really need nobody but you)

Kp na Busara zake !!!

Break News kutoka taifa !!

Taifa stars watoa Droo na wageni ambao ndio wanasemekana kuwa ndio vibonde vya kundi sijui itakuwaje mechi zanazokuja hadi sasa stars imekosa ule ushindi tulioutarajia !!!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

--------------
Benki ya Dunia imeahidi kulisaidia bara la Afrika katika kutatua tatizo la chakula kwa kuongeza msaada katika mbolea na mbegu ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji. "Tutawasaidia muweze kuondokana na tatizo la chakula, tunataka tuwasaidie katika matumizi ya mbolea na mbegu bora".


Alisema Rais wa Benki ya Dunia Robert Zoellick wakati wa mazungumzo na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambaye pia ni Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete walipokutana kwa ajili ya mazungumzo Mjini Yokohama leo mei 29,2008 mchana.Katika mazungumzo hayo Mhe. Zoellick amesema Benki ya Dunia imedhamiria kuongeza msaada na kubuni njia za kuongeza msaada katika kuendeleza kilimo na kuweza msaada huo kufikiwa kwa urahisi na nchi za Kiafrika ili kuondosha uhaba wa chakula.


Rais Kikwete ameishukuru Benki ya Dunia ambapo Rais Kikwete amemueleza Mheshimiwa Zoellick kuwa Tanzania inahitaji msaada zaidi katika kukuza uwezo wa wataalamu wa kilimo katika kufanya utafiti.


Rais Kikwete amemweleza Mhe. Zoellick kuwa kwa sasa Tanzania inafanya utafiti katika swala la kukuza na kuongeza ubora wa mbegu zinazohitajika katika mazingira ya Tanzania,lakini uwezo wa wataalamu hao bado ni mdogo hivyo kulifanya taifa kuagiza mbegu kutoka nje kwa asilimia 75,ilhali mbegu bora zinaweza kutengenezwa na kuzalishwa nchini.


Tukiweza kuongeza mbegu bora zinazozalishwa nchini kwetu mara dufu tutaondokana na tatizo kwa kiwango kikubwa"amesema Rais Kikwete.Mbali na uwezo wa kuzalisha mbegu bora, Rais amemueleza Mhe. Zoellick kuwa pamoja na serikali kutoa ruzuku kwenye mbolea ili kuongeza matumizi ya mbolea katika kilimo, hatua hiyo haionyeshi unafuu wowote kwa wakulima kwa vile bei ya mbolea duniani imepanda mara dufu.


"Msaada mkubwa unaoweza kutupa sisi Tanzania ni kutuongezea uwezo katika vituo vyetu vya utafiti wa mbegu na mbolea kwa ajili ya wakulima wetu kwani kilimo chetu kimedumaa kutokana na kuwa cha asili zaidi badala ya kuwa cha kisasa" Ameongeza.Mapema asubuhi Rais Kikwete ameongoza Kikao cha wakuu wa nchi na mashirika ya kimataifa katika mkutano uliojadili hali ya chakula na changamoto za bei za chakula duniani.


Katika kikao hicho Rais Kikwete amesema, wahisani wanajukukumu la kulisaidia bara la Afrika kutumia ardhi yake kwa ajili ya kilimo bora na cha kisasa ili kuongeza uzalishaji hasa kwa wakati huu ambapo kuna upungufu mkubwa wa chakula.Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Waziri Mkuu wa Japan Mheshimiwa Yasuo Fukuda amesema ifikapo mwezi Julai mwaka huu, Japan itakuwa imetenga $100milion za dharura za msaada wa chakula kwa Afrika.


Benki ya Dunia nayo imeahidi kuongeza pesa zaidi kutoka $4 billion za sasa hadi $6billion katika kilimo .Wakichangia katika kikao hicho wawakilishi mbalimbali kutoka Mfuko wa Chakula Duniani (WFP) amesema dunia inamhitaji mkulima wa Kiafrika sasa kuliko wakati wowote ule na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na serikali za Kiafrika ili kutatua tatizo hilo.


Nayo Benki ya Afrika ADB imesema inafanya marekebisho katika mfumo wake ili kuweza kutenga pesa zaidi katika kutatua swala la chakula barani Afrika.Rais pia amefanya mazungumzo na kukutana na viongozi mbalimbali kuzungumzia hali ya kisiasa na kidiplomasia ya nchi za Afrika,ambapo amefanya mazungumzo na Rais Omar Bashir wa Sudan na Louis Michel Kamishna wa Maswala ya kibinadamu na maendeleo katika Umoja wa Ulaya,ambapo amemweleza kuwa Umoja wa Afrika na nchi za SADC zitapeleka waangalizi katika marudio ya uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.


Rais Kikwete yuko nchini Japan kuhudhuria mkutano kuhusu maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development (TICAD IV) unaomalizika kesho (30 Mei 08); ameshiriki katika vikao mbalimbali na kuongoza baadhi ya mikutano ambapo atashiriki katika kupitisha azimio la Yokohama na baadaye,yeye na Waziri Mkuu wa Japan Mheshimiwa Fukuda, watafanya mkutano na waandishi wa habari na kuondoka mara baada ya mkutano huo.Rais na ujumbe wake watawasili Dar-es-Salaam Tarehe 31 Mei,08.
Mwisho
Imetolewa na Premi Kibanga
Yokohama,
Japan29 Mei, 08

Tujadili Swala Hili..


KWELI MAISHA NI SAFARI NDEFU,WATOTO HAWA WAPO NJIANI KATIKA SAFARI YA MAISHA WAKITAFUTA ELIMU,USAFIRI TATIZO,WANAKAA VITUONI MASAA MENGI, WAKIFIKA SHULENI WAMECHOKA NA WANAPOREJEA NYUMBANI MAMBO NI YALE YALE,HIVI TATIZO HILI LA USAFIRI LITAISHA LINI???
Picha na Mdau Yahya Charahani

Haya Taifa stars ya sawazisha !!

dakika ya 69 ya mchezo danny Mrwanda kafanya mambo kwa kutusawazishia bao ila mpira unaendelea !!

Wanaongoza wageni !!!

Ila inauma sana ila sijui kama tutashinda gemu hii ila ndio wageni wanaongoza kwa sasa ila lolote laweza kutokea ila goli limeingia dakika ya 39 na pia kwa sasa mpira ni dakika ya 42 !!

Diddy THROWS NAOMI CAMPBELL OFF HIS YACHT ... And She Runs Off IN TEARS




Two nights ago Diddy and Naomi Campbell got into it aboard his yacht. Word is that Diddy agreed to host Naomi's 38th birthday party aboard his yacht - but they had a falling out and Diddy ended up tossing her off.

While it's still not clear what happened, I spoke with a person close to Diddy who claims that Diddy has very little patience for Naomi's attitude. The insider explained, "Diddy thinks she's a drama queen, when she starts to act up - he shuts her down ... He has no problem getting in her face and saying all kinds of crazy stuff."

Dang Diddy, it was ole girl's birthday. Was it really that serious to throw her off your boat .....

FIREBOMBED!! 50 CENT'S BABY MOTHER'S HOME BURNED TO THE GROUND ... 50 A SUSPECT!!



May 30, 2008. Just got EXCLUSIVE news!! According to an anonymous source, the home which 50 Cent and his child's mother were fighting over BURNED TO THE GROUND last night.

Right now it's not clear what occurred. But I can OFFICIALLY confirm that everyone (including 50's son Marquis was in the home when the fire started) and no one was injured. And there's more. One of Inawezekana sources close to Shaniqua claim that 50's baby mother suspects that 50, or someone close to him, may have intentionally burned down the house!!!

There's a lot more to this story

Here's an official statement from 50 Cent - via his lawyer

Informed this morning while filming a new motion picture on location in Louisiana, Curtis Jackson expressed deep concern over this fire at his property," a representative for 50 said in a statement. "He is extremely thankful that everyone including his son, Marquise, escaped the burning house safely. He is confident that authorities will be conducting a thorough investigation of the incident and is eager to review their findings

MNAJIM

Sheikh Yahya Hussein
azindua tovuti
www.astrosheikhtz.com

Haya haya haya Taifa stars !!!

Mpaka muda huu stars wanakosa penati katika dakika ya 35 ila tuko hewani tukisubiri lolote ila gabriel kakosa penati hiyo.

Friday, May 30, 2008

KINDS OF CAMERAS !!!!





Ali Kiba Awasha Moto Uingereza...





BONGO FAMILY UK PRESENTS..SPRING BREAK TOUR '08 FEATURING ALI KIBA PERFORMING HIS HIT SINGLE CINDERELLA,NAKSHI NAKSHI MREMBO AND MANY MORE.LONDON ON FRIDAY 30TH MAY@ CLUB AFRIQUE MORE INFO www.bongouk.com

Mamlaka husika tupieni Macho Swala hili..


Pichani ni Abiria waendao maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam,kutoka Posta Mpya, wakipanda gari kupitia mlango wa nyuma na wale wanaoshuka kutumia mlango wa kawaida kutokana na shida ya magari(Mabasi) yaendayo maeneo hayo nyakati za mchana jana. Picha na Kassim Mbarouk.

Mambo Mapya ya Air Tanzania...



Wahudumu wapya katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wakiwa katika sherehe maalum ya kumaliza mafunzo na kukabidhiwa vyeti iliyofanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam jana.Wahuduma hao, wanatarajiwa kuanza kazi muda wowote kwanzia sasa.Picha na Athuman Hamisi/TSN

Mtuhumiwa..


Mtuhumiwa pekee wa kike ambaye ametambuliwa na shahidi jane Andrew akitolewa mahakamani juzi wakati mashahidi wakiendelea kutoa ushahidi wao kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini waliouawa Januari 14, 2006 jijini Dar es Salaam.Picha na Mpoki Bukuku

Mtoto Mwenye Upungufu wa Viungo Azaliwa....


Binti aliyefahamika kwa jina la Foibe Shedrack Kusaga (22) Pichani,mkazi wa kijiji cha Igando Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,amejifungua mtoto wa ajabu ambaye hana mkono wala miguu

Thursday, May 29, 2008

JIJI LETU...................


Mimi nashangaa yaani mpaka gati kufungwa chuma linakuwa kosa la mgambo wa jiji ama mmiliki wa gari? Watu wengi tunapenda kuwalaumu mgambo! Makosa ni ya nani?

Kp na Busara zake !!!

Mafuru..


Pichani mdau Issa Michuzi (kushoto) akimpa hongera Ephraim Mafuru kwa kuula leo kwenye hoteli ya impala mjini arusha.baada ya kuteuliwa kuwa bosi mpya wa masoko na udhamini na mawasiliano wa kampuni ya vodacom Tanzania.

Mzee Makamba Arejea Fiti..


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Yusuf Makamba na mkewe,maarufu kwa jina la Mama January,wakiwapungia mkono baadhi ya wanachama wa chama hicho,mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, akitokea India ambako alikwenda kwa matibabu.Habari na Ahmed Michuzi.

Tallest Man Ukrainian !!!










This giant Ukrainian man is one of the tallest people in the world! Crazy!

Ziara ya Waziri Mkuu Muhimbili....


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimpa pole mtoto Kazija Abdallah (kushoto) ambaye kalazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali hiyo.Kushoto kwake ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Profesa David Mwakyusa na kulia ni Daktari wa magonjwa ya moyo katika hospitali hiyo, Philly Chillo.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Makala ya Leo. *Siasa inahitaji uwe na subira


“KUNA watu wanafikiri kuwa kazi ya siasa ni kitu rahisi, la hasha!Siasa inahitaji zaidi uwe na subira na zaidi uwe mvumilivu, hiyo ndiyo siri ya mafanikio katika kazi ya siasa.” Ndivyo anavyoanza kueleza Mbunge wa Ilemela, Anthony Diallo,ambaye ni Waziri wa zamani wa Wizara ya Maliasili na Utalii na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Mifugo. Diallo pia amewahi kuwa naibu uwaziri katika wizara tofauti. Ameshika nyadhifa tangu mwaka 1995, alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuingia bungeni.

"Namshukuru Mungu kwa kipindi ambacho nimekuwa nikiongoza Wizara kama Naibu Waziri kwa miaka mitano na Waziri kamili kwa miaka mitatu. Nimejifunza mengi licha ya kuwa wanaowajibika zaidi katika Wizara ni watendaji. Waziri, yeye kazi yake ni kuchochea utekelezaji wa maamuzi na Naibu Waziri ni mshauri mkuu wa Waziri," anasema Diallo.
Dialo anasema waziri hana budi kujishughulisha katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi na kwenda na wakati. "Kubwa nililofaidi ni kupata muda mwingi wa kujisomea vitu vingi wakati wote nikiwa naibu waziri na waziri kamili, lakini pia nilipata fursa ya kujifunza kufanya kazi na watu. “Uzuri mwingine ni kuzijua shughuli za kiutawala, hii inakuwezesha kujenga kundi la kazi na zaidi unaaminiwa na watendaji walio chini yako," anasema Diallo. Kwa mengi zaidi juu ya makala hii iliyoandaliwa vyema kabisa na Nashon Kennedy

Waziri Mkuu ashuhudia Upasuaji wa Moyo Muhimbili..



Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (katikati) akishuhudia upasuaji wa moyo ulioongozwa na Daktari,William Mahalu wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
--------------

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda alishuhudia mgonjwa akifanyiwa upasuaji wa moyo (Kwa Kiingereza "open heart surgery") kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,ikiwa ni mwanzo wa mpango mkubwa wa kufanya operesheni za namna hiyo hapa nchini badala ya nje ya nchi.


Baada ya kushuhudia operesheni hiyo alikwenda wodini kuwakagua baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo na wengine wanaojiandaa kufanyiwa.Tangu Mei 21, mwaka huu tayari wagonjwa watano wamekwishafanyiwa upasuaji huo uliokwenda salama, ukiashiria kuwa tiba ya aina hiyo inawezekana hapa nchini kwa kutumia wataalamu wa Kitanzania badala ya nje ya nchi, hasa India.


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa alimwambia Waziri Mkuu kuwa kwa miaka tisa tangu mwaka 1999 hadi mwaka jana, wagonjwa 586, ambao kati yao asilimia 70 ( wapatao 402) ni wa moyo, walipelekwa nje kwa upasuaji na kugharimu kiasi cha Sh. Bilioni 10.


"Tunatarajia tuondokane na gharama hizi kubwa kwa kufanya kazi hii ya upasuaji wa moyo hapa hapa Muhimbili," Profesa Mwakyusa alisema wakati akimwelezea Waziri Mkuu mpango huo. Kwa sasa shughuli hizo zinafanyika katika jengo la Taasisi ya Mifupa (MOI) eneo hilo hilo la Muhimbili, lakini jengio jipya la kitengo cha upasuaji wa moyo linatarajiwa kujengwa hapo hapo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Mitambo, mashine na vifaa vya kazi hiyo vilipatikana kwa kughharimiwa na serikali. Wataalamu 27 wa Kitanzania, wakiwemo madaktari wa upasuaji, wataalamu wa ganzi, mafundi na wauguzi walipelekwa India kwa mafunzo ya mwaka mmoja hadi miwili ili kupata uzoefu wa tiba ya upasuaji wa moyo na wote wamekwisharudi nyumbani.


Waziri Mkuu Pinda alipongeza jitihada hizo na kusema kwamba serikali itaendelea kuziunga mkono ili kuleta ufanisi na kuhakikisha zinakuwa endelevu."Najua sasa wagonjwa watakuwa wengi na kazi itakuwa nzito. Lakini mjitume. Yale ambayo mtayaona hayaendi vizuri, msiyahamishie kwa wagonjwa bali tuleteeni sisi ili tupate njia za kuyatatua," alisema. Kuanza kwa mpango huo wa upasuaji wa moyo nchini kwa kutumia wataalamu wa hapa hapa ni mafanikio makubwa katika kutoa huduma za afya nchini na kutapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi kwa tiba ya aina hiyo.
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021

Akamatwa !!


Wamjua huyo aliekamatwa !! Ama kweli hakuna alie juu ya sheria !!

Kp na Busara zake !!!

Ally Rehmtullah na Temptation Fashion Show...


Mbunifu machachari wa mavazi bongo Ally rehmtullah (Pichani)akipita kuwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye show yake ya mavazi ya Temptation iliyofanyika kwenye hotel ya Kilimanjaro Kempiski jijini Dar es Salaam juzi.

Mengi na PM wa Tanzania !!


Katika kikao cha kujadili maswala ya umeme !! Hivi karibuni !!

Wednesday, May 28, 2008

Dewji amwaga Mil 10..


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo,Joel Bendera,akipokea hundi ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Mbunge wa Singida mjini,Mohamed Dewji kwa ajili ya mchango wake katika maandalizi ya Mashindano ya Riadha ya Taifa yanayotarajiwa kufanyika mkoani Singida Juni 26-30 Hivi karibuni.Picha na Athumani Hamisi/TSN

Wanaonituhumu Wananisingizia -Mkapa


RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Benjamin Mkapa (Pichani)amekanusha matumizi mabaya ya ofisi yake(ikulu) na kuanzisha biashara akiwa madarakani.Akihutubia wananchi katika Kijiji alichozaliwa cha Lupaso,Wilaya ya Masasi,Mkapa alisema wanaomtuhumu wanamchukia kwa kutowapendelea wakati wa utawala wake.


Katika hotuba yake hiyo aliyoitoa wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kwa Kituo cha Afya kinachomilikiwa na Kanisa la Katoliki kijijini hapo, alisema; “Msisikilize uongo huo kwa sababu hauna msingi wowote isipokuwa ni chuki..hasa inayotokana na watu ambao walifikiri nitawapendelea … sikuwapendelea,wananisingizia” alisema Mkapa huku akishangiliwa na wanakijiji wenzake waliohudhuria makabidhiano hayo.


Alisema kuwa yeye si tajiri na kwamba tuhuma hizo ni za uongo na hivyo kuwataka wananchi kuzipuuza kwa kuwa hazina msingi wowote wala chembe ya ukweli.“Sina uwezo wa fedha ingawa najua mnasikia na kusoma mengi …naishi kwa pensheni yangu kutoka serikalini kutokana na kuwa kiongozi kwa miaka 10 ambayo hata Mzee Mwinyi anaishi hivyo maana sisi sote ni wastaafu.
Huo (uvumi) ni uongo …uongo ….uongo ….uongo …uongo….uongo….uongo,” alisema Mkapa.Katika hotuba yake hiyo Mkapa hakujibu tuhuma dhidi yake moja kwa moja Kwa kipindi kirefu sasa Mkapa amekuwa akituhumiwa kwa kuendesha biashara akiwa Ikulu na hasa kuhusu umiliki wa Kampuni ya Tanpower inayomiliki hisa nyingi katika Mgodi wa Makaa ya Mawe ya Kiwira mkoani Mbeya.


Imekuwa ikidaiwa kwamba Mkapa alishirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona katika kununua hisa za Kiwira kwa matarajio kwamba umeme ungezalishwa kutoka hapo baada ya muda mfupi ujao na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lingelazimika kuwalipa takribani Sh milioni 140 kwa siku, hata bila umeme kuzalishwa.Habari na Msimbe Lukwangule

Tenda Wema Uwende Zako...


Mdau David Silaa wa Uswazi anasema.'' Hali inazidi kuwa mbaya jijini Dar es salaam Usafiri nao ni tatizo kubwa huku serikali na mamlaka husika zikiwa kimya tuliwahi kuahidiwa mabasi yaendayo kasi kama (umeme) ila mpaka leo hakuna dalili ya kasi....waathirika wakubwa ni wanafunzi kama muonavyo pichani ni leo asubuhi maeneo ya Kigogo Msamaria mwema alipojitolea kuwapa lift wanafunzi hawa baada ya kushindwa kupata usafiri mapema wa kuwahi shule huku vikwanzo vikubwa vikiwa ni makondakta wa mabasi na madereva kuwanyanyasa wanafunzi kila kukicha.,Nini kifanyike wadau Maana hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku huku mamlaka husika zikiwa kimyaa
kabisa..
Mdau
David Silaa na Haki ngowi.

Mabingwa wa Taifa Cup 2008..


Wachezaji wa timu ya Ilala jijini Dar es Salaam,wakiwa katika picha ya pamoja na kombe na cheki yao baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Taifa kwa kuifunga Kinondoni 5-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini juzi.Picha na Yusuf Badi.

Mkapa achokoza nyuki

Mkapa achokoza nyuki

Na Muhibu Said

WATU wa kada mbalimbali jijini Dar es Salaam jana waligeuka kama nyuki waliochokozwa baada ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kujaribu kujisafisha tuhuma zinazomkabili, huku wengi wakiwa hawaridhiki na utetezi wake na kumtaka ajibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili moja baada ya nyingine.

Watu hao, wakiwamo wanasiasa, wabunge na wanasheria, kwa nyakati tofauti, pia wamemtaka Mkapa kutokwenda kujisafisha kijijini, badala yake azungumze na waandishi wa habari ili apate kuulizwa maswali na kuzitolea ufafanuzi tuhuma za ufisadi zinazomkabili.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema Mkapa hapaswi kwenda kuwaeleza wanakijiji kuhusu ufisadi anaotuhumiwa kuufanya wakati wa utawala wake, kwani hawawezi kumhoji, badala yake wataishia kumpigia makofi kwa vile aliwapelekea msaada wa vifaa vya zahanati.

Alisema anachotakiwa kufanya ni kuzungumza na waandishi wa habari ili ajibu tuhuma hizo kwa vile zina vielelezo na Watanzania waweze kumwelewa.

"Hizi ni tuhuma nzito, alipaswa kuzijibu akizungumza na waandishi wa habari. Na badala ya kuzieleza kwamba ni uongo, tuhuma hizi zimetolewa na vielelezo. Na ni nyingi," alisisitiza Profesa Lipumba.

Alisema tuhuma ya kwanza nzito, ambayo Mkapa anapaswa kuijibu, ni ile inayohusu kuanzisha kampuni ANBEN mwaka 1999 ambapo anadaiwa kuwa alikopa dola nusu milioni kutoka benki wakati huo akiwa rais na akiwa Ikulu na akaweza kuzirejesha katika kipindi cha mwaka mmoja.

Lipumba alisema kitendo cha mtu kuanzisha kampuni akiwa kama rais, ni ukiukwaji wa maadili ya uongozi, kwani kwa kawaida viongozi hata wakiwa na makampuni, huwa wanamweka mtu mwingine anayeendesha kusudi pasiwe na migongano ya masilahi.

"Hilo hajalijibu. Kwamba, ilikuwaje akaanzisha kampuni mwaka 1999 na akakopa nusu milioni na akawa mfanyabiashara bora kweli kuweza kuzirudisha fedha hizo katika kipindi cha mwaka mmoja. Si rahisi kukopa dola nusu milioni ambazo ni zaidi ya Sh milioni 500 na kuweza kuzirejesha na kulipa riba kwenye benki. Hilo la kwanza," alisema Lipumba.

Lipumba alisema shutuma nyingine nzito ambazo Mkapa anatakiwa azijibu ni zile zinazohusiana na rada ambazo zimethibitishwa na Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza ambayo imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya Kampuni ya BAE System iliyoiuzia Tanzania rada hiyo mwaka 2002.

Alisema mwaka 1995, kulikuwa na jaribio la kuiuza rada hiyo na kwamba, ili serikali iinunue, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitakiwa iweke dhahabu iliyonayo kama dhamana ya kununulia ili kama serikali itashindwa kulipa, dhahabu hiyo iende kwa muuzaji.

Lipumba alisema jaribio hilo lilikakataliwa na mradi huo wa kununua rada ukafa, lakini ulikuja kufufuliwa baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kufariki dunia.

Alisema pamoja na mradi huo kufufuliwa, SFO imeeleza kwamba, wakala Shailesh Vithlani aliyesimamia ununuzi wa rada hiyo, amelipwa rushwa ya dola 12 milioni na Kampuni ya BAE, zikawekwa kwenye akaunti nchini Uswisi.

"Mimi binafsi nilikuwa nikipiga kelele kwamba, hii rada ina kila harufu ya rushwa. Serikali ikapinga, ikasema ni utaratibu mzuri kabisa, hauna matatizo. Leo hii tunafahamishwa kwamba, kulikuwa na rushwa ya dola milioni 12," alisema Lipumba.

Alisema wakati ununuzi wa rada hiyo unafanyika, ripoti ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Mambo ya Anga (ICAO) ilitoa taarifa kwamba, rada ambayo inakidhi mahitaji ya Tanzania inaweza kupatikana kwa dola 5 milioni, lakini serikali ya Tanzania ikaenda kununua rada ya dola 40 milioni, huku wakala aliyesimamia ununuzi huo, akiwekewa dola 12 milioni.

Alisema wakala huyo ndiye ambaye alikuwa wakala wa kununua ndege ya rais iliyogharimu zaidi ya dola 40 milioni ambayo pia yeye (Lipumba) aliipigia kelele kwamba haihitajiki, kwa vile ni gharama kubwa, lakini Mkapa wakati huo akasema kwamba, ni muhimu.

Alisema wakala huyo pia alishiriki katika ununuzi wa magari na helikopta za jeshi na kwamba, mambo yote hayo yalitokea katika kipindi cha Mkapa, licha ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Maendeleo, Claire Short wa Uingereza kupinga katika Bunge la nchi hiyo kwamba, rada hiyo isinunuliwe na serikali ya Tanzania kwa vile ina kila harufu ya rushwa, ingawa akazidiwa nguvu na Waziri Mkuu wake, Tony Blair.

"Kwa hiyo kuna suala la rada anapaswa atujulishe, imekuwaje wakati sisi tulikuwa tunamweleza kwamba, ununuzi wa rada, una kila harufu ya rushwa na sasa imethibitishwa kwamba, Shailesh Vithlani alilipwa dola 12 milioni. Je, yeye alipatiwa chochote katika hili? Swali hilo atujibu," alisema Lipumba.

Alisema tuhuma nyingine, inahusu suala la ununuzi wa mgodi wa Makaa ya Kiwira ambapo taarifa zinaeleza kwamba, Mkapa na jamaa zake wa familia pamoja na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Yona walianzisha kampuni ya TanPower Resources Limited iliyonunua mgodi huo kwa bei poa ya Sh milioni 700, lakini wamelipa Sh milioni 70.

Alisema kutokana na hali hiyo, Mbunge wa Vunjo (CCM), Aloyce Kimaro alilieleza suala hilo Bungeni.

"Sasa Mheshimiwa Aloyce Kimaro ana chuki gani binafsi dhidi ya Mkapa, ama Mheshimiwa Mkapa alimnyima nini Kimaro, mpaka sasa Kimaro amelieleza hili na kwamba, katika mkataba huu kuna Capital Payment ambapo kila siku tunalipa Sh milioni 146 kama Capital Charge. Hilo anapaswa kulieleza," alisema Lipumba.

Alisema kashfa nyingine, ni ufisadi wa Sh 133 bilioni katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje katika BoT ambazo alisema benki hiyo isingeweza kutoa malipo kwenye makampuni husika 130 bila serikali kuwa na taarifa.

"Pana kashfa nyingine ambazo bado hazijafanyiwa uchunguzi, kama gharama za majengo ya ofisi za BoT", alisema.

Alisema Mkapa alipoanza kutawala, alitangaza mali zake, lakini alipoondoka madarakani hadi sasa hajasema ameondoka akiwa na mali kiasi gani.

"Laiti Mwalimu angelikuwa hai baada ya shutuma zote hizi, nadhani angejilaumu sana kwamba amedanganywa vibaya na mwanafunzi wake aliyemsimamia na kumpigia debe mpaka kuwa rais," alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa alisema yeye ni kati ya waliomtuhumu Mkapa hadharani kwa rekodi na kwa hiyo hajawahi na kamwe hatoajiriwa na serikali.

Hivyo, Dk Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu alisema anachotakiwa kukifanya Mkapa ni kujibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili na kwamba, hawatahitaji kusikia kutoka kwake jambo la pensheni ambalo hajaulizwa.

"Brela (Kitengo cha serikali cha Kusajili Makampuni) inaonyesha yeye (Mkapa) na mkewe, walianzisha kampuni yenye S.L.P 15 Luthuli Street akiwa Ikulu. Kwa maana alikuwa mjasiriamali akiwa Ikulu. Tunataka kujua mtu huyo ni yeye au la. Na pia alilipa pango ya jengo la Ikulu shilingi ngapi kwa kuitumia Ikulu kufanya biashara?" alisema Dk Slaa.

Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro alimtaka Mkapa kujibu hoja na kwamba, maelezo aliyoyatoa Bungeni kuhusu Mkapa namna alivyonunua mgodi wa Kiwira bila kufuata utaratibu, alifanya hivyo kwa vile zama hizi ni za ukweli na uwazi.

"Hajajibu hoja. Wabunge wangetaka kusikia hayo yanayosemwa dhidi yake. Tunataka yasiendelee kutokea, pia serikali ibadilike, bunge libadilike na viongozi wa ngazi zote wabadilike, watumikie wananchi, siyo wananchi wawatumikie," alisema Kimaro.

Kimaro alisema ataendelea kusema ukweli kwani fitina kwake ni mwiko na Mkapa ndiye muasisi wa kauli mbiu ya uwazi na ukweli.

Naye Hussein Issa anaripoti kuwa, Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Cyriaws Kamugisha, alisema iwapo Mkapa atapatikana na hatia ya kuhusika na tuhuma za ufisadi, anatakiwa afikishwe kizimbani kwani, sheria ni msumeno.

Alisema ikiwa rais aliyeko madarakani akiwa na kosa la madai, anatakiwa ashitakiwe na kuhoji iweje aliyemaliza muda wake asishitakiwe ikiwa ana kosa la kujibu?

Tuhuma za kununua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira (KMCL) ulioko wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya , zililipuka mwanzoni mwa mwaka huu.

Kufuatia tuhuma hizo, hadhi ya Mkapa ambaye aliingia madarakani akiwa safi na kujulikana 'Mr Clean' inazidi kuporomoka miongoni wananchi mbalimbali, ambao wanaamini kuwa alitumia vibaya wadhifa wake kujipatia mali kinyume na maadili ya uongozi.

Juzi Mkapa alikaririwa na vyombo vya habari, akisema watu wanaomtuhumu wamefanya hivyo kwa vile aliwanyima vyeo wakati alipokuwa madarakani kwa miaka 10 na kwamba watu wote wanaomuita fisadi ni wa kupuuzwa kwa kuwa wana chuki binafsi naye.

Mkapa alikuwa akiwahutubia wanakijiji wa Lupaso wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa uongozi wa kituo cha afya kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki kijijini hapo.

Tafakari...


Mahali:Jijini Dar es Salaam

Kp na Busara zake !!!

Haya haya mambo Kazi !!!

Job Title:: Deputy Secretary General-Finance and Adminstration
Company Name:: Evangelical Lutheran Church in Tanzania
Address:: Secretary general, Evangelical Lutheran Church in Tanzania. Box 3033, Arusha
Qualifications:: Holder of CPA (T) or Equivalent. Holder of MBA will be an added advantage
Source:: Daily News
Advert Date:: May 24, 2008
Deadline :: Jun 30, 2008

"Sanaa Imeokoa Maisha Yangu!"

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

May 23 2008

'Sanaa imeokoa maisha yangu' asema msanii anayeunda zawadi za shindano la Faidika na BBC

Msanii kutoka Uganda, mshindi wa tuzo kadhaa, Peter Oloya, amechaguliwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, kubuni na kuunda tuzo za washindi wa shindano la vijana. Faidika na BBC linatafuta kijana mwenye umri wa kati ya miaka 16 hadi 24, ambaye ana wazo zuri la biashara, ambalo litakuwa na manufaa kwa jamii. Zawadi ya kwanza ina thamani ya Dola Elfu Tano za Marekani.

Peter ataunda mataji ambayo yatazawadiwa kwa washindi wa kitaifa nchini Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda, na pia katika fainali itakayofanyika Kampala, mwezi Juni. Peter aliwasilisha michoro yake kupitia Ruwenzori Sculpture Foundation, ambayo inaratibu ubadilishanaji wa utamaduni na elimu kati ya wasanii wa Afrika na Uingereza. ' Nimefurahishwa na BBC Idhaa ya Ulimwengu, shirika ambalo naliheshimu kwa ubora wa kazi yake, kwa kunichagua mimi katika nafasi kubwa kama hii katika shindano hili. Ni ndoto ambayo kwangu imekuwa kweli'

'Usanii ndio maisha yangu, na hakika imejenga mwelekeo wa maisha yangu' ameongeza msanii huyo mwenye umri wa miaka 30. 'nimepitia maisha ya vita na kushuhudia mengi wakati nikiwa mdogo, na nikatumia sanaa yangu kama njia ya kuondokana na nyakati hizo ngumu, kwa hakika fani hii inaendelea kunisaidia kila siku' ameongeza Peter.

Changamoto kubwa kwa Peter ilikuwa kubuni kitu ambacho kinatoa taswira nzito. ' Niliambiwa na BBC kubuni kitu kinachoonesha mtazamo wa mbali na uvumbuzi unaoakisi kufanya vyema katika biashara, na vilevile kuonesha kustawi na kukua kwa jambo. Ilikuwa kazi ngumu, lakini nimeweza kupata suluhu ya hilo'

Suluhu hiyo, ni sanamu ya mtu aliyesimama katika ramani ya nchi zinazoshiriki katika shindano hili, za Afrika Mashariki na Kati na zinazozungumza kiswahili. Mfano huyo wa mtu amesimama akitazama anga huku akiwa amenyoosha mikono yake, inayoshikilia nyota. Peter anaeleza kuwa mchongo huo 'Unakutaka unyooshe mikono yako kufikia nyota, maana yake uendelee kukua, na uelewe ya kwamba hakuna linaloshindikana. Shaba na kioo ambazo zimetumika kutengeneza tuzo hiyo zinashabihiana na zitadumu kwa miaka mingi'

Peter, ambaye alizaliwa katika kijiji cha Lemo Bongolewich katika wilaya ya Kitgum, Kaskazini mwa Uganda, anasema anaweza kujihusisha na vijana wanaoshiriki katika shindano la Faidika na BBC. Akiwa ni msanii aliyejifundisha uchoraji, na ambaye alifanya jitihada na kujilipia mwenyewe elimu ya Sekondari hadi chuo kikuu, anasema ' Mafanikio sio jambo la kupatikana kwa bahati, bali kupitia dhamira na kazi ngumu, mambo ambayo natazamia washiriki wa shindano hili watakuwa nayo. Kuenzi jamii pia ni muhimu, na ni jambo ambalo limenivutia katika shindano la Faidika na BBC.

Peter amekuwa akisaidia jamii yake kupitia shirika lijulikanalo kama Sanaa kwa maendeleo ya jamii, ambalo alilianzisha mwaka 2004. Likiwa na makao yake katika wilaya za Kitgum na Gulu, Kaskazini mwa Uganda, shirika hilo linatoa huduma za elimu ya sanaa na uchongaji, na pia elimu ya uraia kupitia sanaa ya maigizo kwa vijana wa eneo hilo. Sehemu ya shirika hilo linadhaminiwa na fedha zinazotokana na mauzo ya kazi zake Peter. 'Watoto wengi na vijana wanaokuja kujiunga nasi wanakuwa wameathiriwa na vita, lakini mafunzo tunayotoa yanawasaidia kuondokana na hali waliyonayo. Kusaidia kuleta hali ya kawaida kwa vijana ni muhimu kwangu, kwa kuwa wao ndio mategemeo ya baadaye, na siku moja watasaidia kuleta amani nchini'

Peter, ambaye anasema kazi yake imechochewa na msanii wa Kiingereza Damien Hirst, ametunukiwa zawadi kadhaa kwa kazi zake za uchongaji, ikiwemo zawadi ya kwanza ya shindano la ' Sanaa kwa amani' la Uganda, na zawadi nyingine ya uchongaji kutumia shaba, lililoendeshwa na shirika la Uingereza la uchongaji, Pangolin Editions, katika chuo kikuu cha Makerere.

Peter alifuzu katika fani ya uchongaji katika kitivo cha uchoraji cha Margaret, kilichopo chini ya Makerere, na kupata shahada ya uchoraji sanifu. Amefanya kazi nyingi katika sanaa hiyo ikiwemo kuchonga zawadi aliyotunukiwa Malkia wa Uingereza, Elizabeth wa pili, wakati wa mkutano wa wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya Madola, mjini Kampala, mwaka 2007. Mapema mwaka huu, Peter aliwasilisha picha ya kuchora kutumia rangi za mafuta, kwa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, alipozuru chuo kikuu cha Makerere.

Picha ya Peter Oloya inaweza kupatikana iwapo inahitajika.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Christine George, Afisa mwenezi msaidizi, BBC World Service
+44 (0) 2075571142; christine.george@bbc.co.uk

Maelezo kwa Wahariri.

Muda wa kupokea michanganuo ya shindano la Faidika na BBC, sasa umekwisha. Taarifa zaidi kuhusu shindano zinapatikana katika mtandao wetu bbcswahili.com/faidika

BBC Idhaa ya Kiswahili ni Shirika la Utangazaji ambalo hutoa huduma zake kupitia radio na kwenye mtandao kwa wasikilizaji wanaozungumza Kiswahili barani Afrika na ulimwengu mzima kwa ujumla. Kipindi cha BBC cha asubuhi Amka na BBC hurushwa hewani saa 12.00 asubuhi saa za Afrika mashariki, na hukuletea habari za eneo zima na duniani, pamoja na muziki na habari mbalimbali za kijamii. Kipindi maarufu cha BBC cha habari na uchambuzi Dira ya Dunia huanza saa 12 na nusu jioni. Leo Afrika husikika saa tatu kasorobo Afrika Mashariki, na hukuletea habari mbalimbali zilizotokea barani Afrika kwa siku hiyo. Mtandao wa BBC kwa kiswahili unapatikana katika bbcswahili.com. Katika mtandao huu, unaweza kupata taarifa za maandishi, matangazo yetu, makala na uchambuzi wa habari za Afrika na dunia nzima. Pia katika mtandao huu utapata taarifa na matangazo ya kipindi maarufu cha Kimasomaso, ambacho hutoa elimu ya afya ya uzazi na kuchambua mila na desturi zinazozingira suala zima la uzazi. Kipindi hicho kilianzishwa na kitengo cha kimataifa cha BBC cha misaada - BBC World Service Trust.

BBC World Service - Idhaa ya Dunia, ni shirika la habari la kimataifa la utangazaji linalotoa huduma za matangazo kwa lugha 33 mbalimbali. Shirika hili linatumia njia kadhaa kuwafikia wasikilizaji wake milioni 183 ulimwenguni kote, kwa kupitia Masafa mafupi, masafa ya kati, FM, satellite na viunganishi. Vituo washirika vya radio vipatavyo 2,000 hupitisha matangazo ya BBC, huku vituo kadhaa vukirusha taarifa zake kupitia simu za mkononi na vifaa mbalimbali visivyotumia nyaya. Wavuti wa BBC unatoa habari mbalimbali kwa maandishi, sauti na video, na vilevile kutoa nafasi kwa wasikilizaji kushiriki moja kwa moja katika vipindi kufuatana na matukio ya duniani. Takriban watu milioni 700 huvinjari katika wavuti huu kwa mwezi, na hivyo kuvutia karibu watumiaji milioni 40 kwa mwezi. Kwa taarifa zaidi tembelea bbcworldservice.com. kufahamu zaidi kuhusu Idhaa ya Kiingereza ya BBC, au kujiandikisha kupata majarida ya kwenye mtandao tembelea bbcworldservice.com/schedules.

Maonyesho ya Ndege za kivita Kwa BUsh !!!