Wednesday, May 21, 2008

Flora Mbasha kuzindua Furaha Yangu...


Mwanamuziki na mtunzi Maarufu wa nyimbo za injili Nchini Tanzania Flora Mbasha akiwa katika picha ya pamoja na Mumewe Emmanuel Mbasha.
---------------
Msanii wa muziki wa Injili nchini Florah Mbasha anatarajia kuzunguka Tanzania nzima kuweza ukitambulisha album yake mpya ya Furaha Yako,akiongea na waandishi wa Habari Florah alisema katika ziara hiyo ataongozana na Mumewe ambaye pia ni mmoja wa viongozi katika Band ya Florah.
"Tunatarajia kuzunguka Tanzania nzima kuitambulisha album hii ya tatu ili iwe changamoto kwa vijana nao waweze kuupenda na kuingia katika muziki huu wa Injili, pia tunataegemea vijana wengi kujiunga nasi katika ziara hii"
Album ya Furaha yako inatarajiwa kuzinduliwa katikati ya mwezi ujao mjini Dodoma, album hiyo ina nyimbo 11 ambazo ni Adui Yako wimbo ambao upo juu sana kwa sasa katika nyimbo za injili, Mteule usiogope,Natembea na Yesu na tutamuona hizo zote ni baadhi ya nyimbo zilizomo katika album hiyo iliyosheheni nyimbo nyingi nzuri.
Wasanii hawa wameweza kutoa album mbili ikiwa ni vol 1 ya Jipe Moyo wimbo uliowatoa sana mwaka 2004, na Unifiche ya mwaka 2007.

No comments: