--------
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL
COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI..
Sasa wakati wa kurudi mezani,Rais aviambia CCM and CUFAsema vyama hivyo vinakubaliana kimsingi na kuwa tofauti ni utekelezajiRAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa baada ya vyama CCM na CUF kuwa vimeweka misimamo yao kuhusu Mwafaka hadharani, sasa ni wakati wa kurudi mezani kuendeleza majadiliano.
Rais pia amesema kuwa anaamini kuwa majadiliano hayo hatimaye yatazaa matunda mazuri kwa mustakabali wa Tanzania.Rais ameyaeleza hayo kwa nyakati tofauti leo katika majadiliano na wageni ambao alikutana nao Ikulu,mjini Dar es Salaam.
mazungumzo yake na Waziri wa Nchi wa Ufaransa anayeshughulikia Mahusiano ya Kimataifa na Nchi Zinazozungumza Kifaransa, Alain Joyandet, Rais ametumia muda kumwelezea mgeni historia ya majadiliano ya mwafaka na sababu za msingi zilizopelekea kuanzishwa kwa majadiliano hayo.“Naamini mambo yatakwenda vizuri.
Hatimaye tutafanikiwa katika hili la mazungumzo la Mwafaka,” amesema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, kimsingi, CCM na CUF vinakubaliana kuhusu mambo ya kufanyika juu ya Mwafaka, na kuwa tofauti ni katika utekelezaji wa hayo yaliyokubaliwa.“CCM wanataka suala hilo kubwa la msingi liamuliwe moja kwa moja na wananchi.
CUF wao wanataka wanasiasa kuamua kwa niaba ya wananchi. Hivyo, tofauti iko katika namna ya kutekeleza yaliyokubaliwa,” amesema.Rais pia amemweleza Waziri huyo kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali Shirikishi katika Zanzibar ulichukuliwa miaka saba iliyopita, mwaka 2001, wakati wa majadiliano yaliyozaa Mwafaka wa Kwanza kati ya CCM na CUF.
Rais amesisitiza kuwa uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha karibu cha Butiama, Musoma haukubadilisha makubaliano ya msingi kati ya vyama hivyo.“Kilichofanyika ni CCM kuongeza mapendekezo mawili ili nayo yajadiliwe na timu za vyama hivyo viwili.”Amesema kuwa pendekezo moja ni kuwashirikisha wananchi kuamua utekelezaji wa mwafaka kati ya vyama hivyo,na la pili ni kuweka utaratibu wa ukomo wa utekelezaji (sunset clause) wa mwafaka huo.
Amesema “mwafaka unalenga kuitoa Zanzibar katika matatizo ya sasa ya kisiasa. Hauwezi kuwa utaratibu wa daima dumu na kuwa ukifika wakati kuwa mfumo huo wa utawala wa kisiasa umekamilisha kazi yake, basi unaweza kuondolewa na Zanzibar ikarudi katika ushindani wa kawaida wa kisiasa.”Amesema kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa katika nchi za Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),na sasa katika Kenya.
Katika mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Adam Woods, Rais amesisitiza kuwa bado iko nafasi ya kuokoa mazungumzo hayo ya Mwafaka.“Wote sasa wamezungumza kiasi cha kutosha. Sasa ni wakati wa kukaa chini na kuendelea na mazungumzo,” Rais amemweleza Balozi huyo.Amesisitiza: “Maamuzi ya CCM hajabadilisha jambo lolote la msingi katika makubaliano ya Mwafaka –no deviation on fundamental agreement – Tulichofanya sisi ni kuongeza jambo la kuwashirikisha wananchi na kuwataka wanaoendesha majadiliano kulifikiria na hili.”
---------------
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Mei, 2008
No comments:
Post a Comment