Saturday, May 17, 2008
Tanesco Yapokea Sh Mil 81.5..
Mkurugenzi wa Tanesco nchini, Dk. Idriss Rashid (kushoto) akipokea hundi ya thamani ya shilingi milioni 81.5, ikiwa ni gawio la shirika hilo kutoka kampuni ya kutengeneza nyaya za umeme ya Afrika Mashariki ijulikanayo kama East African Cables Ltd.
Hundi ya gawiwo hilo ambalo ni asilimia 10 ya hisa za Tanesco ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Murithi Ndegwa kwa Mkurugenzi wa shirika la umeme, Dk. Idris Rashidi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Mei 16,2008 na Ofisi ya Mawasiliano ya Tanesco, gawiwo hilo limeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo Tanesco ikiwa ni mojawapo ya wanahisa ilipewa sh milioni 1.8 tu.
Akizungumza kwenye sherehe hizo, Ndegwa alisema uzalishaji na tija kwenye kampuni hiyo umekuwa ukiongezeka siku hadi siku hivyo kuwezesha kampuni yake kuongeza gawiwo kwa wanahisa wake mbalimbali ikiwamo Tanesco.Makampuni mengine yenye hisa kwenye kampuni hiyo ni pamoja na baadhi ya migodi ya dhahabu,viwanda vya saruji,kiwanda cha TANALEC Arusha na Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco.Aidha kwa upande wake,Dk. Rashidi aliupongeza uongozi wa kampuni hiyo kwa kuboresha bidhaa zake zinazouzwa ndani na nje ya nchi na kuongeza kuwa gawiwo hilo litaisaidia Tanesco kununua vifaa na kupeleka umeme kwa wateja wengi zaidi.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na mjumbe wa bodi wa kampuni hiyo, Profesa Joshua Dosiye na Meneja Mauzo Bridget Temba.Kwa mujibu wa picha ya mdau Mrocky Morcky anayetoa hundi hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa East African Cable, Murithi Ndengwa.Wapili kushoto katika picha hii ni Mkurugenzi wa Bodi ya East African Cable, Profesa Joshua Doriye, pamoja na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bridget Temba.Habari hii na Msimbe Lukwangule.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment