Thursday, May 29, 2008

Makala ya Leo. *Siasa inahitaji uwe na subira


“KUNA watu wanafikiri kuwa kazi ya siasa ni kitu rahisi, la hasha!Siasa inahitaji zaidi uwe na subira na zaidi uwe mvumilivu, hiyo ndiyo siri ya mafanikio katika kazi ya siasa.” Ndivyo anavyoanza kueleza Mbunge wa Ilemela, Anthony Diallo,ambaye ni Waziri wa zamani wa Wizara ya Maliasili na Utalii na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Mifugo. Diallo pia amewahi kuwa naibu uwaziri katika wizara tofauti. Ameshika nyadhifa tangu mwaka 1995, alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuingia bungeni.

"Namshukuru Mungu kwa kipindi ambacho nimekuwa nikiongoza Wizara kama Naibu Waziri kwa miaka mitano na Waziri kamili kwa miaka mitatu. Nimejifunza mengi licha ya kuwa wanaowajibika zaidi katika Wizara ni watendaji. Waziri, yeye kazi yake ni kuchochea utekelezaji wa maamuzi na Naibu Waziri ni mshauri mkuu wa Waziri," anasema Diallo.
Dialo anasema waziri hana budi kujishughulisha katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi na kwenda na wakati. "Kubwa nililofaidi ni kupata muda mwingi wa kujisomea vitu vingi wakati wote nikiwa naibu waziri na waziri kamili, lakini pia nilipata fursa ya kujifunza kufanya kazi na watu. “Uzuri mwingine ni kuzijua shughuli za kiutawala, hii inakuwezesha kujenga kundi la kazi na zaidi unaaminiwa na watendaji walio chini yako," anasema Diallo. Kwa mengi zaidi juu ya makala hii iliyoandaliwa vyema kabisa na Nashon Kennedy

No comments: