Wednesday, May 21, 2008

Mzee Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro...


RAIS mstaafu Ali Hassan Mwinyi (83) anatarajiwa kuongoza msafara wa kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kupambana na Ukimwi nchini.Msafara huo 'Changamoto ya Kilimanjaro' ambao unaratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) utaanza Juni 14 mwaka huu na utajumuisha wapanda mlima 53, akiwemo Mzee Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk. James Msekela.


Taarifa iliyotolewa na GGM na Katibu wa Changamoto ya Kilimanjaro 2007, Sean Jefferys anasema maandalizi muhimu yamekamilika na tayari wapandaji 53 akiwamo Rais mstaafu Mwinyi tayari wanafanya mazoezi kujiandaa msafara huo.Rais Mstaafu Mwinyi alisema amekubali kushiriki katika changamoto hiyo baada ya kuridhishwa na malengo yake, ambayo ni kukusanya fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi hapa nchini pamoja na kujihusisha na kuwasaidia waathirika.

Mstaafu Mwinyi aliwaomba watu binafsi na kampuni wamuunge mkono na kudhamini ushiriki wake kwa kuwa kwa njia hiyo tu kutaleta maana ya ushiriki wake.“Umri wangu ni miaka 83 na mwaka jana wakati nazindua changamoto hii niliwaomba watayarishaji nami nataka kupanda mwaka huu. Wengi wao hawakuniamini na hata kwangu haukuwa uamuzi mwepesi lakini ni funzo la jamii,” alisema Mwinyi.
Kwa mujibu wa Jeffrey’s kampuni zilizojitokeza kudhamini upandaji huo mwaka huu ni pamoja na Anglo Gold Ashanti ambayo ni kampuni mama ya GGM, Celtel Tanzania, Barrick Gold, PanAfrican, Atlas Copco, Sandvik na Afrikan Explosives. Nyingine ni Rhino Lodge, Air Tan
zania, Kilimanjaro Kempinski Hotel, ATS, Sarova Hotel, Coastal Travel and Tours na Zara.Picha kwa Msaada wa Issa Michuzi

No comments: