Saturday, February 28, 2009

UPIMAJI WA VVU




Mamia ya wananchi jana walijitokeza katika upimaji hiari wa virusi vya Ukimwi, uliofanyika katika viwanja vya Vinyago, vilivyopo Mwenge, jirani na baa ya Igongwe na kuendeshwa na wahudumu wa Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

US kama Zimbabwe!


Du! E bwana e! Kumbe Marekani na ujanja wao waliwahi kuwa kama Zimbabwe! Nimefuma bonge la noti $100,000 ya mwaka 1934 kwa mdau Miruko. Maelezo soma mwenyewe http://www.rsmiruko.blogspot.com/

MAISHA YA MASHAKA

Mi nashindwa kuelewa wabongo tukoje, yaani mtu anakosa sehemu zote za kupumzika analala relini likija treni? baadae utasikia serikali mbovu kumbe mwenyewe fala! Hivi hawajui hili dude haligongi bali linagongwa?

STARS CHAN

Henry Joseph akifanya mambo siku walipocheza na Ivory Coast.
Nizar Khalfan akimkomalia muivory Coast siku ya mechi .
Stars sasa imenza kutisha baada yakuweka kandanda safi nakuinyuka Ivory Coast 1-0, sasa tunasubiri Zambia ambao wamekuwa wateja wetu kwamuda mrefu. Tutawamudu Aluta Contuinua!!!! Ni leo Hii tunacheza nao.

CCM # 1

Wabongo bwana sasa hivi wanashangaa, Mzee makamba anazunguka nchini kutangaza chama chake baadae wataanza Ooh, wameiba kura, sijui nini. Haya cheki anavyokusanya vichwa usitokee uchaguzi kampeni za mwishoni ndio tutoe majibu ya kulalamika CCM wezi!

Monday, February 23, 2009

Obama plans to slash deficit in half







Obama aims to control 'exploding' deficits

WASHINGTON – President Barack Obama has committed hundreds of billions of dollars to help revive the economy and is working on a plan to cut the federal deficit in half by the end of his first term.

Obama will touch on his efforts to restore fiscal discipline at a White House fiscal policy summit on Monday and in an address to Congress on Tuesday. On Thursday he plans to send at least a summary of his first budget request to Capitol Hill. The bottom line, said an administration official Saturday, is to halve the federal deficit to $533 billion by the time his first term ends in 2013. He inherited a deficit of about $1.3 trillion from former President George W. Bush.

The official, speaking on condition of anonymity because the president has not yet released his budget for the fiscal year 2010, which begins Oct. 1, said the deficit will be shrunk by scaling back Iraq war spending, ending the temporary tax breaks enacted by the Bush administration for those making $250,000 or more a year, and streamlining government.

"We can't generate sustained growth without getting our deficits under control," Obama said in his weekly radio and Internet address that seemed to preview his intentions. He said his budget will be "sober in its assessments, honest in its accounting, and lays out in detail my strategy for investing in what we need, cutting what we don't, and restoring fiscal discipline."

Republicans were not convinced. They said Obama's plan would hurt small businesses, including many filing taxes as individuals and possibly facing higher taxes under his plan.

"I don't think raising taxes is a great idea," Senate Republican leader Mitch McConnell of Kentucky told CNN's "State of the Union" on Sunday. "And when our good friends on the other side of the aisle say raising the taxes on the wealthy, what they're really talking about is small business."

Obama's budget also is expected to take steps toward his campaign promises of establishing universal health care and lessening the country's reliance on foreign oil.

Obama has pledged to make deficit reduction a priority both as a candidate and a president. But he also has said economic recovery must come first.

Last week, he signed into law the $787 billion stimulus measure that is meant to create jobs but certainly will add to the nation's skyrocketing national debt. He also is implementing the $700 billion financial sector rescue passed on Bush's watch; about $75 billion of which is being used toward Obama's plan to help homeowners facing foreclosure.


taifa stars yalala 0-1 kwa senegal
sura za wadau zinajieleza huko abidjan usiku huu...
kidedea kililia hadi filimbi ya mwisho katika wanja la felix houphet boigny
mashabiki kibao walijitokeza kuipa taff taifa stars huko abidjan, wengine wakiwa wamesafiri na timu
bendera yetu ilipendezesha jukwaa la wabongo, ila ndo hivyo tena. gemu...
mpira umeisha na stars imelala 0-1 kwa senegal huko ivory caost katika mtanange wa CHAN. Pichani ni wadau wakifuatilia mechi hio ya taifa stars na senegal katika luninga kubwa iliyowekwa na tbc wakishirikiana na kampuni ya nova media katika viwanja vya bustani ya mnazi mmoja gaden usiku huu. february 25 taifa stars inakutana na wenyeji iliyopigwa 3-0 na zambia katika mechi ya ufunguzi

rwanda's mission impossible
No one has ever accused President Paul Kagame (pictured) or his administration of a lack of ambition.

This is a government that has made it a habit to undertake seemingly impossible tasks and more or less succeed in most of them.

Take the example of the almost quixotic goal of harnessing the methane gas in Lake Kivu for electricity.

The gas has been bubbling up from the bottom of the lake for thousands of years and no one ever thought to use it for anything.

Up to now, it actually has been something of a time bomb, given what happened in Cameroon in 1986, when Lake Nyos suddenly emitted a large cloud of carbon dioxide, killing 1,700 people.

Enter the administration of Kagame, which instead saw an opportunity in a problem...

Saturday, February 21, 2009

mambo ya gado
President Kagame of Rwanda and Rebel Laurent Nkunda (FDLR), DR Congo, Great Lakes.
waya wa fibre optic waanza kutandazwa
Wahandisi wa kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wanafunga kamba ili kuvuta waya ya mawasiliano (fbre optic cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar
Wafanyakazi ya Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wamebeba waya ya mawasiliano (fibre optic cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam
Mafundi ujenzi wakijenga kituo cha waya ya mawasiliano ( Fibre Optic Cable) cha Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo itaanza kutoa huduma hiyo ya kuboresha network nchini mwezi wa sita mwaka huu.

kp na Busara zake.

KIBAKA MSALABANI

Jamaa hoi baada ya kutolewa misumali aliyokuwa amewambwa nayo.

Wahudumu wakiokoa maisha ya kibaka huyo!
Kibaka aking'olewa misumali katika hospitali ya Mwananyamala

MKAZI wa Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam, amenusurika kufa baada ya kupigiliwa na misumari kwenye msalaba na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, kwa tuhuma za kuiba baiskeli.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea leo maeneo ya Manzese Uzuri baada ya kijana huyo kukutwa na baiskeli iliyodaiwa kuwa ya wizi.

Wakazi wa eneo hilo walimkamata na kisha kutengeneza msalaba na kumtundika juu kwa kumpigilia misumari ya nchi sita kisha kumwacha hapo.

Baadaye wasamaria wema waliopita katika eneo hilo walimwona wakautoa ubao mmoja na kisha kijana huyo akaenda kujisalimisha katika kituo cha polisi akiwa na ubao wa mikononi ambako alipigiliwa mishumari. Polisi wa kituo hicho wakamkimbiza katika Hospitali ya Mwananyamala akiwa kwenye msalaba huo kwa ajili matibabu.

“Sijawahi kuiona katika maisha yangu, wananchi kweli wamekuwa wanyama,” alisema mfanyakazi mmoja wa hospitali hiyo mara baada ya kumpokea mtu huyo aliyeletwa na polisi hospitalini hapo mapema asubuhi jana.

Akisimulia mkasa huo baada ya kumhudumia kwa kumtoa misumari iliyokuwa imepigiliwa mikononi na mabegani; mtumishi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema: “Baadhi misumari iliingia katika mifupa ya mikono na kumuumiza vibaya.”

“Ameumia sana na kuna mifupa ambayo imevunjika baada ya kutobolewa na misumari hiyo mikubwa, lakini ana bahati hajafa,” alisema mtumishi huyo.

Imeelezwa kuwa kijana huyo mara baada ya kukutwa na baiskeli hiyo, wananchi walimkamata na kumsulubu kwa kutengeneza msalaba na baadaye kumpigilia kwenye msalaba na kumwacha akiwa ananing’inia.

Baadaye walipita wasamaria wema walioamua kumsaidia kwa kuondoa ubao mkubwa uliokatisha mgongoni na hivyo yeye kujisalimisha polisi huku ubao uliopigiliwa mikono ukiwa bado mwilini mwake.

Polisi walimchukua na kumpeleka hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na hakufunguliwa mashtaka yoyote kwani hakukuwa na mtu aliyelalamika kuibiwa.

Baada ya kufikishwa hospitalini hapo kijana huyo alikuwa kivutio kwa wagonjwa na ndugu waliowatembelea pamoja na baadhi ya watumishi waliokuwa hapo.

Wengine kwa kushangazwa ama kuvutiwa na kitendo hicho waliamua kupiga picha kwa kutumia simu zao ambazo zilimwonyesha kijana huyo akiwa katika maumivu makali.

Baada ya hapo wahudumu wa hospitali hiyo walimchukua na kumtoa misumari hiyo na kumpatia matibabu.







Vijana wapya wa JWTZ walionyesha manjonjo yao baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi ya Makutupora mkoani Dodoma.

STARS CHAN


Taifa Stars tayari imewasiri mjini Abidjan kwa jili ya kututoa kimasomaso wabongo na kesho ndio mpambano wakwanza na Senegal katika michuano ya wachezaji wanaocheza nyumbani (CHAN). Hapa Kocha maximo akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya kwanza jana kabla ya mechi hiyo. wachezaji wote wako fit.

UMASKINI

Mtoto aliyeuzwa na mamake apatikana Mtoto Fatma Kisawiro akiwa na Mama yake mzazi Tabu Wiliamu katika makao makuu ya jeshi la Polisi jijini Da r es Salaam jana


MTOTO anayedaiwa kuuzwa na mama yake amekutwa katika maeneo Chalinze akiwa hai na kwamba mtu anayedaiwa kumnunua mtoto huyo amekimbia.

Kupatikana kwa mtoto huyo ni matokeo ya bibi wa mtoto kutoa taarifa baada ya mtoto huyo kudaiwa kuuzwa na mama yake mzazi kwa mwanamke wa kimasai ambapo kwa kile alichodai kuwa kuwa ni hali ya maisha imekuwa ngumu na kwamba asingeweza kumtunza mtoto huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema wamempata mtoto huyo Chalinze na kwamba aliyemunua ametoroka.

Mwanamke anayedaiwa kumuuza mtoto wake huyo mwenye umri wa miezi tisa, Tabu William (36), bado anashikiliwa na polisi katika Kituo cha Chang’ombe baada ya kupimwa kama ana matatizo ya akili ama la.

Tabu alipelekwa jana katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke chini ya ulinzi wa polisi ambapo alipimwa na daktari wa afya ya akili hospitalini hapo, lakini hata hivyo majibu ya vipimo hivyo hayakufahamika mara moja kutokana na madaktari hao kugoma kutoa majibu kwa waandishi kutokana na maadili ya taaluma hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Emmanuel Kandihabi, alisema mama huyo anaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Mwanamke huyo alikamatwa Jumamosi iliyopita nyumbani kwao Mtoni Kidande, baada ya mama yake mzazi aliyekuwa akiishi naye, Fatuma Ally (70), kuripoti kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mjukuu wake huyo katika kituo cha polisi Chang’ombe
.

USAFIRI


Mambo ya Zenji hayo, usafiri wa mlalahoi!

Zimbabwe

Thursday, February 19, 2009

Ni Kama Miujiza Fulani!
























Isimila Stone Age site, Kilomita 20 kutoka Iringa Mjini. Ukifika Iringa tembelea Isimila, hutajutia.

Ya Kale Dhahabu: Pijoti La Urithi Hili !
Peugeot 203. Liko Makanyagio, Iringa. Tunaambiwa Ulaya na Marekani kuna watu wenye kupanda madau kwa vitu kama hivi.

Davidson Kiwia na Vivian
Wanameremeta..

Mdau Davidson Kiwia kaachana na Club ya Ukapera na Kufunga pingu za Maisha na Kimwana Viviana Massawe kanisa la Kilutheri la Azania Front Jijini Dar es Salaam na kufwatia na sherehe la nguvu.kwa wadau mbalimbali mtakaopenda kudungwa picha za maaana kwenye harusi kama hizi wasiliana na Mdau Abdallah Mrisho kwa simu number 0713 839363 au Email:abbymrisho@gmail.com
Hivi Mheshimiwa
Slaa..
Ni

Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Laurance Masha(Kushoto)akitete jambo na Mbunge wa Karatu Mheshimiwa Dr Willbroad Slaa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Wednesday, February 18, 2009





MWANAMUZIKI mahiri wa Msondo Ngoma, Joseph Maina amefariki ghafla jana asubuhi akiwa ndani ya daladala.
Dereva wa basi la daladala lenye namba za usajili T582 AFL linalofanyika safari kati ya Mwenge na Temeke Mikoroshoni, Kassim Salum aliiambia Mwananchi jana kwenye Hospitali ya Temeke kuwa msanii huyo alifariki akiwa amekaa kiti cha mbele mlangoni.
"Unajua aliwahi kuingia, na sisi ilikuwa zamu yetu kupakia hapo Temeke Mikoroshoni, kulikuwa na abiria anataka kupanda, nilipomwambia asogee kiti cha kati, nikaona anakakamaa na muda mfupi akalala.
"Baada ya kuona hali ile, watu walijaa na niligeuza gari hadi kituo cha polisi Maghorofani, lakini na wao walinipa askari wakaniambia tuelekee hospitali ya Temeke," alisema Salum.
Hata hivyo, mwili wa Maina ulibakia kwenye kiti cha daladala kwa takriban saa nzima katika hospitali hiyo huku mashabiki na watu wengine wakielezea kumfahamu kama ni Maina. Mwananchi ilifika hospitalini hapo na kukuta umati wa watu wakielezea masikitiko yao kutokana na kifo hicho.
Saa 7:11 mchana, kiongozi wa Msondo Ngoma, Muhidin Maalim Gurumo aliiwasili akifuatana na mpiga solo, Said Mabera, wacheza shoo na wanamuziki wengine.
Hata hivyo, wasimamizi wa chumba cha maiti walimruhusu Mabera kwenda kutambua mwili na aliporudi alithibitisha kuwa kweli ni Maina.
Gurumo alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na miguu na bendi walikuwa wakiandaa utaratibu wa kumtafutia matibabu.
"Kwa kweli ni pigo kubwa kwani Maina alishiriki katika nyimbo zote za Msondo, alishiriki albamu zote ni pigo kwa sasa hatuna la kusema tutatoa taarifa," alisema.
Maina ambaye ameacha mke na watoto wa wawili alitunga kibao kumuimbia mke wake, Mama Cossy ambacho hakijatoka.
Maina ameongeza pengo la wanamuziki wakali wa bendi hiyo waliofariki miaka ya karibuni, akiwemo TX Moshi William, Athumani Momba na Suleiman Mbwembwe.

NATIONAL STADIUM

Huu ndio lunyasi ndani ya Uwanja wa taifa baada ya kukamilishwa kwa zuria la kukimbilia wambulu na kukabidhiwa juzi na wachina kwa wabongo waweze kufanya mambo! Ila kweli tukiachia mameneja kama waliopo sasa hivi tutafika kweli?

Kibonzo cha leo !!!!

MNASHANGAA?

Jamani muda mrefu mzee Mkapa alikuwa hajaonekana mitaani, hata Sumaye lakini kikubwa alichotuachia ni uwanja mpya wa taifa kumbe hata yeye alikuwa hajauona? Cheki anavyoshangaa!!! Watanzania badala wamwache mzee wa watu ale uzee vyema wanamletea fitna!

Monday, February 16, 2009

MATUMLA ABONDWA

Nyumbani ni nyumbani tu, Cheka akipongezwa na walugulu.
Afande Sele akimpongeza Cheka baada ya Ushindi, hii ni mambo ya Dar mpaka Moro.

Mashambulizi yakiendelea usoni mwa Matumla.


Matumla akiondoka akiwa hoi baada ya kichapo hasa round ya 11 kidogo aanguke.
RC Moro, Said Kalembo akimvika mkanda wa Ushindi Cheka.

BONDIA francis Cheka jana usiku aliendeleza ubabe wake kwenye familia ya Matumla baada ya kumpiga kwa mara ya tatu Rashid Matumla kwa pointi kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania ulishudia mabondia hao wakionyesha ujuzi wa kutumia makonde katika raundi zote 12 za mchezo huo.
Majaji wote watatu walimpa Cheka ushindi wa pointi 19/18 dhidi Matumla aliyeonyesha upinzani mkali kwa bingwa huo wa ICT.
Rashid Matumla kabla ya mpambano huo alisema endapo atapigwa atatangaza kujiuzuru rasmi. SIJUI INAKUWAJE SASA?