Friday, May 15, 2009

Kp na busara zake.

Msimamo wa Umoja wa Ulaya kuhusu uchaguzi wa Zanzibar .


Bunge la Umoja wa Ulaya mjini Strasbourg
************
Wakati Zanzibar inaelekea katika heka heka za uchaguzi mkuu wa mwakani, Umoja wa Ulaya umesema unajiandaa kuhakikisha kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki, na matakwa ya wananchi yanaheshimiwa.

Kauli hiyo imekuja wakati Umoja huo ukisheherekea kuundwa kwake miaka 49 iliopita na ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni kuhimiza ubunifu na uvumbuzi.
Mwandishi wetu wa Zanzibar, Salma Said.
Ishini Kwa Amani Asema Papa Benedict XVI.


NAZARETH
Papa Benedict wa XVI amewatolea wito waumini wa dini zote wakaazi wa ardhi takatifu kuipinga chuki na badala yake waishi kwa amani.Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo alipoongoza misa katika mji wa Nazareth ulio na waArabu wengi.
Misa hiyo iliyofanyika nje ilihudhuriwa na waumini wapatao alfu 40.Baada ya misa hiyo Papa Benedict alikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika makazi ya watawa yaliyo karibu na kanisa linaloaminika kuwa mahali ambapo Bikira Maria alipokea ujumbe wa malaika Jibril kwamba atapata ujauzito wa mwana wa Mungu.
Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni ameingia katika mkondo wa mwisho wa ziara yake ya siku nane ya eneo la Mashariki ya Kati.Kundi moja dogo la Waislamu wa Palestina limeipinga kikao hicho cha mkesha wa Naqba kumbukumbu ya siku taifa la Israel lilipoundwa.
Habari Kwa Hisani:www.dw-world.de
Mwanafunzi Rebeca Abdalah.


Mwanafunzi Rebeca Abdalah (13) wa Shule ya Msingi Mbagala Kuu, aliyeathiriwa na milipuko ya mabomu na kumsababishia matatizo ya kutosikia vizuri, moyo kwenda mbio na kuumwa na kichwa kila wakati akiwa nje ya darasa wakati wenzake wakicheza.

Picha na Fredy Azzah
Simu Za Mkononi Kuanza Kubanwa Julai.

Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICTs) katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Zaipuna Yonah akizungumza wakati wa maadhisho ya siku ya Tekinolojia ya Habari na mawasiliano Duniani (TEKNOHAMA) jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma.


*********************
Kuanzia Julai mosi mwaka huu, watumiaji wote wa simu za mkononi nchini watatakiwa kusajili kadi na simu zao upya kwenye kampuni za huduma za simu ili ziweze kuchukua taarifa binafsi za wateja. Taarifa binafsi zitawezesha kampuni za simu na serikali kufahamu kila mtu anayemiliki kadi ya simu ili kudhibiti matumizi mabaya ya simu hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma, alisema jana Dar es Salaam kuwa uandikishaji wa kadi utafanyika kwa miezi sita na ifikapo Desemba mwaka huu, kadi ambazo zitakuwa hazijaandikishwa hazitafanya kazi. Profesa Nkoma ambaye alikuwa akizungumza katika semina ya wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Wiki ya Mawasiliano na Habarijamii Duniani iliyoanza jana hadi Jumapili, alisema kuanzia muda huo, kadi za simu zitauzwa kwa utaratibu maalumu.
Alisema badala ya kadi kuuzwa kiholela mtaani, kampuni za simu zitalazimika kutafuta mawakala maalumu ambao watafahamika na watapewa namba za utambuzi kutoka TCRA ili waweze kufanya kazi kwa kufuata maelekezo ya mamlaka hiyo. Profesa Nkoma alisema baada ya kuandikishwa, wakala hao watapokea maombi mapya ya kadi za simu na kuchukua taarifa za wenye simu na kuzipeleka kwenye kampuni za simu.
Kampuni za simu nazo zitatoa huduma hiyo. Alisema taarifa zitakazohitajika ni zile ambazo zipo kwenye vitambulisho vya watumiaji simu na kama vitambulisho vitakuwa havina picha, mteja atalazimika kupeleka picha kwenye kampuni ya simu au wakala wake. “Baada ya miezi sita kupita, simu zote ambazo zitakuwa hazijasajiliwa hazitafanya kazi,” alisema na kuongeza kuwa kazi hiyo itafanywa kwa umakini baina ya mamlaka hiyo, serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Alisema lengo ni kudhibiti matumizi mabaya ya simu ambapo watu wengine wamekuwa wakitumia simu hizo kufanya udanganyifu na uhalifu, lakini baada ya mpango huo kukamilika, watu hao watadhibitiwa. Profesa Nkoma alisema hata simu za mkononi zitatambulika, hivyo kama simu ikiibwa, mmiliki akitoa taarifa simu yake itafungwa hivyo mwizi hataitumia. Alisema TCRA ilianza kwa kuzuia matumizi ya namba binafsi Machi mosi mwaka huu na hatua hiyo ilisaidia kuzuia vitendo vingi visivyo vya kawaida katika jamii.
Tanzania ina jumla ya kadi za simu milioni 13. Kaulimbiu ya mwaka huu ni kumlinda mtoto dhidi ya athari za matumizi ya mtandao wa intaneti.
Habari Na Picha Kwa Hisani: Faraja Mgwabati/Salhim Shao.
Baadhi ya waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea hivi karibuni Mbagala.

Baadhi ya waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea hivi karibuni Mbagala, Dar es Salaam wakipata msaada wa chakula kilichotolewa na Taasisi ya Kiislamu jana. Zaidi ya kaya 500 zilifaidika na msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni nne.

Habari Na Picha Kwa Hisani: HabariLeo
Nyumba zilizoharibika Mbagala sasa ni 7,000


Idadi ya nyumba zilizoharibiwa na milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Mbagala, jijini Dar es Salaam mwezi uliopita, imeongezeka kutoka nyumba 4,636 hadi nyumba 7,000.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alisema idadi hiyo imebainishwa na wataalamu wanaofanya tathmini ya nyumba na mali katika eneo la Mbagala.
Alisema zoezi la tathmini linaendelea vizuri na kwamba amewaongezea wataalamu wanaofanya tathmini vifaa muhimu kama kompyuta ndogo ili kurahisisha kazi hiyo.
Hata hivyo, Lukuvi ameonya kuwa serikali haitawalipa wananchi ambao hawajapata madhara
yoyote kutokana na milipuko hiyo.
“Maana kuna watu wamekaa kule hawaendi kazini na hawajaharibikiwa hata na kikombe cha chai wanasubiri kufanyiwa tathmini…zoezi hili ni kwa ajili ya wananchi walioathirika tu,” alifafanua.
Alisema taarifa ya awali kuhusu nyumba zilizoathirika itatolewa mwishoni mwa wiki hii.
Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, amewatahadharisha wananchi wa Mbagala na wakazi wa maeneo ya jirani na eneo ilipotokea milipuko hiyo kutogusa chuma chochote wasichokijua kwa kuwa vyuma vingine ni hatari.
Alisema eneo hilo bado lina vitu vingi vya hatari ambavyo vimesambaa na kwamba wananchi wanatakiwa kuwa makini.
“Kwa sasa hivi tunafanya usafi kuhakikisha takataka zote zinaondoka kwa sababu si salama, tumewaonya wananchi wasiguse kitu chochote wanachokitilia shaka ila watoe taarifa kwa wanajeshi walio katika eneo hilo,” alisema.
Kuhusu mlipuko wa juzi jioni katika eneo hilo, alisema wanajeshi walilipua bomu lililokuwa halijalipuka baada ya kulibaini.
Alisema wataendelea kuteketeza mabaki yote yatakayopatikana, lakini watakuwa wanatoa taarifa kwa wananchi wa karibu na kambi hiyo.
Katika hatua nyingine, ubalozi wa Marekani umetoa msaada wa fedha wa Sh. milioni 65 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa milipuko hiyo. Kaimu balozi wa Marekani nchini, Larry Andre, alitangaza kutoa msaada huo jana na kuahidi kuendelea kuisaidia serikali kutokana na janga hilo.
  • Na Marekani yatoa msaada wa mil. 65/-

Habari Kwa Hisani: Na Restuta James
Tsvangirai: Hakuna nyongeza ya mishahara

HARARE, Zimbabwe
WAZIRI Mkuu wa Zimbabwe, Bw. Morgan Tsvangirai amesema kwamba Serikali ya pamoja iko hoi kifedha na haiwezi kutimiza madai ya Umoja wa muungano wa vyama vya Wafanyakazi yakutaka iwalipe viwango vya juu vya mishahara.
Bw.Tsvangirai alisema kwamba kutokana na jinsi hali ilivyo hakuna mfanyakazi yoyote wa Serikali akiwemo Rais Robert Mugabe ambaye anapata zaidi ya dola za Marekani 100 sawana pauni 67 kwa mwezi.
Kauli ya Bw. Tsvangirai imekuja kufuatia madai ya Chama cha wafanyakazi ya kuitaka Serikali kuwalipa wafanyakazi dola 450 huku kikitisha kuitisha mgomo endapo madai hayo hayatatekelezwa.
Hata hivyo wakati akihutubia sherehe za siku ya wafanyakazi mjini Harare, Bw. Tsvangirai alisema kwamba hivi sasa Serikali inahitaji muda zaidi ili kuimairisha uchumi. "Serikali hii imefilisika na hatuna uwezo wa kulipa zaidi ya dola 100 tu," Bw. Tsvangirai aliuambia umati wa watu waliodhuria sherehe hizo na akaongeza kuwa hali hii itabadilika na kuanza kulipa mishahara mizuri wakati Serikali itakapoboreka na watu wengi wakaanza kulipa kodi."Ndio kwanza tuna miezi mitatu tangu tuingie ofisini na waombeni tupeni muda," aliongeza Waziri Mkuu huyo.
Bw. Tsvangirai alisema kwamba madai ya umoja huo vyama vya wafanyakazi ni ya msingi lakini yanapaswa kuangalia hali ; ya kifedha ya Serikali na utendaji mdogo wa viwanda vya nchi hiyo.Kabla ya taarifa hiyo ya Bw. Tsvangirai, awali Bw. Lovemore Matombo ambaye ni rais wa muungano huo wa vyama vya wafanyakazi wa (ZCTU) katika salamu zake kwa wanachama wa umoja huo alisema kwamba hivi sasa wanajiandaa kuitisha mgomo wa nchi nzima ingawa hakueleza ni lini.
Homa ya nguruwe si janga la kimataifa, Asema Ban ki Moon.

NEW YORK
Margaret Chan, afisa mkuu wa Shirika la Afya duniani, W.H.O., amesema hadi sasa ni visa 1000 ambavyo vimeripotiwa kuhusiana na homa ya nguruwe katika nchi 20 duniani, na kwamba kasi ya maambukizi imepungua sana.
Naye Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon, amethibitisha kwamba shirika hilo la afya duniani halina mpango wa kuipandisha homa ya nguruwe katika daraja la sita- ambayo ndio daraja ingetambulika kama janga la kimataifa.
Ban ki moon amesema shirika hilo la afya ulimwenguni linafuatilia kwa makini jinsi homa hii inavyosambaa, lakini hawatazidisha tahadhari iliopo sasa ambayo ni daraja ya tano.
Idadi ya vifo nchini Mexico imefika watu 26, huku kifo kimoja pia kikiripotiwa katika nchi jirani ya Marekani. Nchini Mexico, mji wa Mexico City unajitayarisha kufunguliwa tena kwa mikahawa na maeneo mengine wanakokusanyika watu, baada ya serikali kutangaza kwamba hatari ya homa ya nguruwe imepita.
y, May 15, 2009 |
Kesi ya Manji dhidi serikali kusikilizwa Julai.


Na Sadick Mtulya
GODWIN Muganyizi, wakili wa mkurugenzi wa kampuni ya Quality Group Ltd, jana alikwamisha usikilizwaji wa kesi dhidi ya Manji na serikali.
Kesi hiyo namba 265/2008 inayosikilizwa na Jaji Richard Mziray, ilifunguliwa na Manji Novemba 7, 2008 katika Mahakama Kuu
Kitengo cha Ardhi na kuanza kusikilizwa Februari 11, 2009.
Manji anaishtaki serikali akiidai fidia ya Dola 29, 694, 750 za Kimarekani baada ya kumzuia kuendeleza shughuli za ujenzi katika kiwanja namba 2199, kitalu namba 6 kilicho katika makutano ya Barabara ya Samora na Mkwepu. Kiwanja hicho aliuziwa na serikali.
Jana Muganyizi alifika mahakamani hapo, lakini akaieleza mahakama kuwa asingeweza kuendelea na kesi hiyo kwa kuwa amepata udhuru.
Katika maombi yake mfanyabiashara huyo anataka serikali imlipe fidia hiyo pamoja na riba ya asilimia 12, gharama zote za kesi hiyo, kulisafisha jina lake pamoja na gharama nyingine kadri mahakama itakavyoona zinafaa.
Mchanganuo wa fidia hiyo ni kuwa, Manji anataka alipwe dola 23, 694, 750 za Kimarekani kama hasara aliyoipata kutokana na hatua ya ujenzi aliyokuwa amefikia, na Dola 6,000,000 za Kimarekani kama fidia kutokana na kuchafuliwa jina lake, kampuni na biashara zake.
Agosti 26, 2006 serikali kupitia Wizara ya Utalii na Mali Asili ilimsimamisha Manji kuendelea na ujenzi katika kiwanja hicho kutokana na Sheria Namba 23(1) ya kutotaka kubadilisha mandhari ya maeneo ya kihistoria
Katika hati ya mashtaka, Wakili Muganyizi kwa niaba ya Manji, amemshitaki katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi na Makazi pamoja na Mwanasheria Mkuu.
Hati hiyo inasema katibu mkuu huyo anashtakiwa kwa kuwa ndiye aliyetangaza zabuni ya kuuza kiwanja hicho ambacho alikinunua kwa fedha taslim Sh295 milioni.
Manji anadai kuwa alihalalishwa kumiliki kiwanja hicho na kupewa hati namba 186166/102 baada ya kushinda zabuni iliyotangazwa na serikali kupitia wizara hiyo.
Pia anadai Novemba 30, 2005, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilimuidhinisha kama mmiliki halali wa jengo hilo ambalo kwa wakati huo lilikuwa likikaliwa na mpangaji aliyejulikana kwa jina la Shekigendo Simon.
Manji anadai kuwa Februari 14, 2006 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilimtaka kuliendeleza jengo kwa kubadilisha aina ya jengo alilokuwa akitaka kulijenga la ghorofa 20 na kama asingefanya hivyo angetozwa faini ya kutoendeleza kiwanja na hiyo ilikuwa ni amri kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hati hiyo, inasema uamuzi wa Manji kudai fidia hiyo umetokana na serikali kutomjibu barua yake aliyowapelekea na kutotoa maelezo kwa wananchi kuhusu ukweli wa tatizo hilo. Kesi hiyo itasikilizwa tena Julai Mosi mwaka huu.
Habari Kwa Hisani: www.mwananchi.co.tz
y, May 15, 2009 |
Kesi ya Manji dhidi serikali kusikilizwa Julai.


Na Sadick Mtulya
GODWIN Muganyizi, wakili wa mkurugenzi wa kampuni ya Quality Group Ltd, jana alikwamisha usikilizwaji wa kesi dhidi ya Manji na serikali.
Kesi hiyo namba 265/2008 inayosikilizwa na Jaji Richard Mziray, ilifunguliwa na Manji Novemba 7, 2008 katika Mahakama Kuu
Kitengo cha Ardhi na kuanza kusikilizwa Februari 11, 2009.
Manji anaishtaki serikali akiidai fidia ya Dola 29, 694, 750 za Kimarekani baada ya kumzuia kuendeleza shughuli za ujenzi katika kiwanja namba 2199, kitalu namba 6 kilicho katika makutano ya Barabara ya Samora na Mkwepu. Kiwanja hicho aliuziwa na serikali.
Jana Muganyizi alifika mahakamani hapo, lakini akaieleza mahakama kuwa asingeweza kuendelea na kesi hiyo kwa kuwa amepata udhuru.
Katika maombi yake mfanyabiashara huyo anataka serikali imlipe fidia hiyo pamoja na riba ya asilimia 12, gharama zote za kesi hiyo, kulisafisha jina lake pamoja na gharama nyingine kadri mahakama itakavyoona zinafaa.
Mchanganuo wa fidia hiyo ni kuwa, Manji anataka alipwe dola 23, 694, 750 za Kimarekani kama hasara aliyoipata kutokana na hatua ya ujenzi aliyokuwa amefikia, na Dola 6,000,000 za Kimarekani kama fidia kutokana na kuchafuliwa jina lake, kampuni na biashara zake.
Agosti 26, 2006 serikali kupitia Wizara ya Utalii na Mali Asili ilimsimamisha Manji kuendelea na ujenzi katika kiwanja hicho kutokana na Sheria Namba 23(1) ya kutotaka kubadilisha mandhari ya maeneo ya kihistoria
Katika hati ya mashtaka, Wakili Muganyizi kwa niaba ya Manji, amemshitaki katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi na Makazi pamoja na Mwanasheria Mkuu.
Hati hiyo inasema katibu mkuu huyo anashtakiwa kwa kuwa ndiye aliyetangaza zabuni ya kuuza kiwanja hicho ambacho alikinunua kwa fedha taslim Sh295 milioni.
Manji anadai kuwa alihalalishwa kumiliki kiwanja hicho na kupewa hati namba 186166/102 baada ya kushinda zabuni iliyotangazwa na serikali kupitia wizara hiyo.
Pia anadai Novemba 30, 2005, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilimuidhinisha kama mmiliki halali wa jengo hilo ambalo kwa wakati huo lilikuwa likikaliwa na mpangaji aliyejulikana kwa jina la Shekigendo Simon.
Manji anadai kuwa Februari 14, 2006 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilimtaka kuliendeleza jengo kwa kubadilisha aina ya jengo alilokuwa akitaka kulijenga la ghorofa 20 na kama asingefanya hivyo angetozwa faini ya kutoendeleza kiwanja na hiyo ilikuwa ni amri kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hati hiyo, inasema uamuzi wa Manji kudai fidia hiyo umetokana na serikali kutomjibu barua yake aliyowapelekea na kutotoa maelezo kwa wananchi kuhusu ukweli wa tatizo hilo. Kesi hiyo itasikilizwa tena Julai Mosi mwaka huu.
Habari Kwa Hisani: www.mwananchi.co.tz

KITAFUNIO

Utamu wa kusafiri Tanganyika ni jinsi vitafunio vinavyouzwa hasa ukiwa msimu wa mahindi mabichi, utapata ya kuchoma na kuchemsha! kwa wasafiri wa mud amrefu wanaweza kuotea hapa wapi!!?

CHAKACHAKA KIBOKO

Hapa alipokuja bongo siku za karibuni!!











Pamoja na kuhuzunishwa lakini baadae alipagawisha watu wa Mtwara kichizi ,cheki aliweza akumchezesha mpaka afande!!




CHAKACHAKA AMWAGA CHOZI





Yvonne Chakachaka akibubujikwa na machozi baada ya kutembelea wodi ya watoto katika hospitali ya mkoa wa Mtwara juzi na kupata taarifa ya mama aliyemleat mtoto aliyeugua malaria na baadae kulazwa kabala ya kufa. mama huyo alilazimika kumbeba marehemu mwanane mgongoni na kurudi kijijini kwao kwa kukosa uwezo wa kumsafirisha!!!! Ndio mambo ya Bongo. Chakachaka ambaye ni balozi wa maralia alijitolea gari moja ili kusaidia wamama kama hao!

NGASA AOA




Mchezaji Mahili wa Taifa Stars na yanga Mrisho Ngasa amefunga pingu ya maisha jijini Dar es Salaam na Latifa. Sasa mimi sisemi lakini Hongera zake nyingi kwa uwamuzi wake huo.

KITIMOTO

Jamani wabongo wabishi yaani pamoja na Masri kuamua kuchinja vitimoto vyao vyote kuepuka mafua ya nguruwe, wao wanaendelea kufyeka tu!!! Cheki shehena hii ilikuwa ikipelekwa sehemu kwajili ya kufanya mambo!!!

STARS NA MABINGWA WA CHAN




Ndugu zangu hata kusema sitaki, ni kwamba Tanganyika ilipolambwa 2-0 katika Uwanja wa taifa sijui main Stadium lakini ndio huko. Jamaa wameonyesha kweli ni mabingwa wa Chan though, tumejitajidi kwa kiasi kikubwa bila ya kuvunjika moyo wachezaji. Wamepigana mpaka kufa lakini kwa kuwa bahati haikuwa yetu. Kuna mafisadi wachache walizomea taifa Stars laskini Maximo kasema wanaozomea leo ndio watashangilia baadae.
dawa ya wanaodengua kupokea simu
video
baraka chibiliti katuletea hii kutusalimia toka italy
washika bunduki nao wamo
Arsenal’s new away kit 2009/2010…tupo baba, msimu ujao wetu.
Miss IFM 2009 kupatikana Leo dar
Kuanzia kulia ni mwakilishi wa Mwasu Fashions Bw.Sam Mshana,Manakamati wa Miss IFM 2209 Bw.Sarungi Daniel,Mwenyekiti wa miss IFM 2009 Peter Sarungi pamojana Mjumbe Bw.Lazaro Lutobeka walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar kuhusiana na shindano hilo la Miss IFM 2009 ambalo Leo usiku ndio itampata kinara wa shindano hilo litakalofanyika ndani ya ukumbi wa New Msasani club,Kinondoni Jijini Dar.

Shindano hilo lenye mvuto wa kipekee hasa kutokana na warembo wake wote kuwa fiti kila idara, litaleta ushindani na changamoto mpya katika mchakato mzima wa kumpata mlimbwende wa kuiwakilisha MissTanzania katika ngazi ya Taifa 2009.
Juu na chini warembo wa Miss IFM 2009 wakijifua katika ukumbi wa Break point ya mjini

PSI kuzindua ATM za kondomu wiki ijayo
Kampuni ya PSI inayosambaza mipira ya kiume ya Salama Kondom wiki ijayo itazindua uuzaji wa kondomu hizo kwa njia ya ATM kama hii ionekanayo pichani.

Cpwaa na Mambo ya Advanced Bongoflava
CP

Katika kuendeleza na kuupeleka muziki wetu level za mbele “ Advanced Bongoflava” ningependa kushare na wadau wote product yangu mpya ambayo iko tayari.

MOBILE PHONE WEBSITE,ili uweze kupata habari mbalimbali za msanii CPWAA, miziki yake, uweze kudownload video, wallpapers na michezo ya simu bure! Basi tembelea tovuti yake ya simu za mkononmi na utapata huduma zote hizo.

Kwa sasa msanii C.p a.k.a CPWAA anatamba na kibao chake kipya cha PROBLEM bofya hapo ujionee video
http://www.youtube.com/watch?v=OXhqQY4QxvE .

Ukitaka kudownload wimbo huo kwenye simu yako tembelea tovuti yake ya simu . Jinsi ya kuingia kwenye tovuti hiyo:
Tuma neno CPP kwenda 15551 na utapokea link itakayokupeleka kwenye tovuti hiyo. ( Hakikisha simu yako imeunganishwa na GPRS,WAP au INTERNET).
Kama simu yako haina internet unaweza kupata kwa kutumiwa nyimbo hizo baada ya kujiunga na CPWAA SMS FAN CLUB kwa kutuma neno CPWAA kwenda 15551.Ukishajiunga utakuwa unapokea nyepesi nyepesi za Cpwaa, Interview zake na show zake mahala zinapofanyika ( BUREE!), pia utapata discount ya 20% kwenye kila bidhaa za Cpwaa zitakazouzwa kuanzia saba saba.
Also: Wakae tayari kwa super dupa website
www.cpwaa.co.tz
to be launched Soooon!!!
Regards,
Ilunga khalifa,
IT Manager,
Push Mobile media Ltd, Tanzania.
P .o box 11133.
5th Floor, Barclay's House.
Dar-eS-alaam.
Tanzania.
Mobile Number: +255785000017
Email: cp@push.co.tz
Web: www.push.co.tz
bob marley day kusherehekewa Leo dar
uingereza yasaidia walioathirika na mabomu mbagala
DFIDT Head Darren Welch prsenting books donation to Mbagala Kuu Primary school Head Teacher, Paul Daniel

DFIDT Head Darren Welch with one of the Mbagala kids Elionora Prosper

UK assists children affected by Mbagala explosions

The UK through its Department for International Development (DFID) is providing $90,000 (about Tsh. 122 million) to give immediate help to more than 7,000 children affected by the Mbagala explosions late last month.

This support, delivered through Save the Children, will help the two schools closest to the military base resume teaching as quickly as possible. It includes providing 7,332 textbooks, 32,900 exercise books and 3,400 school bags for the children, items which were lost in the stampede following the explosions.

“We want to make sure that children can go back to school”, says Catherine Kennedy, Country Director for Save the Children in Tanzania, “After a traumatising experience like this, they need the routine of everyday life to deal with the shock and start feeling secure again.”

Darren Welch, Head of DFID’s office in Tanzania, said “We are happy to be able to assist the children of Mbagala. DFID provides support to education in Tanzania, so it makes sense for us to do something to help the children. We think Save the Children, and the relief agencies, are doing very important work here and are pleased to play a small part.”

The support will also help schools to create spaces for psychosocial support to help children who have been traumatised by the experience. This includes providing material such as balls and skipping ropes, paper and colour pencils as well as professional assistance to children and teachers on how to deal with the psychological effects of the experience. This support will be provided to children in the community, whether they are in school or not.

This assistance is being provided after a joint team with members from Save the Children and the Temeke Municipal Council assessed the needs of more than 7000 children in the Mbagala Kuu area who were affected by the explosions.

DFID Tanzania’s support to the children of Mbagala is in line with our overall aim of improving the quality of education in Tanzania.


ndinga mpya kwa maendeleo bonde la ziwa tanganyika
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Batilda Burian akizinduwa Gari Kwajili ya Mradi Endelevu ya Hifadhi ya Bonde la Ziwa Tanganyika Kulia Mkurugenzi UNDP Tanzania Bw Alain Noudehou, Katibu Mkuu Ofisi wa Makamu wa Rais Bi Ruth Mollel na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Shabaani Mwinjaka iliyofanyika leo Mtaa wa Luthuli Mjini Dar es Salaam. Picha na mdau Ali Meja
uzi mpya wa kina nanihii...

Dah! kama nini hiyo ya away ....... Mi homa.... tehe tehe tehe...
- The Blues-
uzi wa ugenini wa darajani msimu ujao

Huo uzi wetu wa away mwakani chamtoto tu hizo zenu bwawa la main na mashetani wekundu, cheki uzi huo wa darajani, mtakoma ubishi,
Mdau wa Darajani
--------------------------
uzi wetu mpya wa ugenini
uzi mpya wa ugenini wa bwawa la maini umeshatoka Haya Dogo tumeuona !!
taswira ya kumbukumbu
Baba wa Taifa akila pozi Taj Mahal enzi zake
mpiganaji athumani hamisi aendelea vyema
mpiganaji athumani hamisi akila pozi na wapiganaji wenzie waliomtembelea katika hospitali ya netcare rehabilitation jijini johannesburg. kutoka shoto nyuma ni joseph kulanga (mhariri mkuu wa habari leo), japhet sanga (mhariri wa habari daily news) freddy maro (mdau wa ikulu) mdau alimwene mwakyusa, john lukuwi (mdau wa maelezo) na ben apiyo ambaye ni mtoto wa mzee timothy apiyo aliyekuwa katibu mkuu ofisi ya rais ambaye anauguzwa hospitalini hapo. hivi sasa athumani ameshapona majeraha kilichobaki ni mazoezi ya viungo ya 'mama cheza' katika hospitali hiyo

JK aongoza baraza la mawaziri
JK akiongoza kikao cha baraza la mawaziri ikulu jijini Dar Juzi asubuhi

Wednesday, May 13, 2009

" Nawapa Siku 90 Kukamilisha Michango...." Pinda


NAWAPA SIKU 90 KUKAMILISHA MICHANGO YA MAJI - PINDA

*Asema wasipokamilisha, mradi uhamishiwe kijiji kingine



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewapa miezi mitatu wakazi wa kijiji cha Kilyamatundu kata ya Kipeta wawe wamekamilisha kutoa michango kwa ajili ya mradi wa maji safi la sivyo utahamishiwa katika kijiji kingine.



Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumatatu, Mei 11, 2009) wakati akihutubia mkutano wa hadhara na kujibu maswali ya wakazi wa kata hiyo ambako alikuwa katika siku ya pili ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani Sumbawanga, mkoani Rukwa.



Waziri Mkuu alishangazwa na ugumu wa wakazi hao kuchelewa kukamilisha michango wakati wana mifugo mingi na wamevuna mpunga kwa wingi, jambo ambalo alisema lingeweza kuwasaidia kumudu michango ya sh. 2,000 kila mwanakijiji.



“Serikali imetenga sh. milioni 150 kwa ajili ya mradi huu. Haiwezekani tangu mwaka 2004 muwe mmechangia sh. 500,000 tu… sisi kama Serikali tunaandaa mipango na tunataka umiliki wa wananchi katika miradi kama hii, ndiyo maana mnaombwa mchangie asilimia tano tu ya gharama zote ambayo ni sh. milioni 7.5/-,” alisema.



Alisema kuna vijiji zaidi ya 100 katika wilaya hiyo ambavyo vinahitaji kupatiwa miradi ya maji safi lakini ni vijiji 10 tu ambavyo viliteuliwa kupatiwa mradi huo. “Huu ni mwezi Mei, ifikapo Agosti 31, kama hawajakamilisha michango yao, Mkurugenzi warudishie michango yao, na upeleke huu mradi kwenye kijiji kingine,” alisema Waziri Mkuu.



Akijibu maswali ya wananchi, Waziri Mkuu aliwaagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Bw. Thobias Sijabaje na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Mussa Zungiza wafuatilie madai ya ujenzi hafifu wa shule ya sekondari ambayo wananchi walisema ujenzi wake umelipuliwa. “DC wenu ni mpya lakini itabidi aje na Mkurugenzi watafute ni kwa nini hadhi ya majengo hailingani na thamani halisi ya fedha,” alisema.



Akijibu maombi yao ya kupatiwa mradi wa umwagiliaji kwenye kutoka mto Momba unaomwaga maji yake katika ziwa Rukwa, Waziri Mkuu aliwaagiza viongozi wa halmashauri hiyo wafuatilie kama mradi huo upo na kama ulishafanyiwa upembuzi yakinifu kama wananchi hao wanavyodai.

Leo Waziri Mkuu anaanza ziara ya siku mbili katika jimbo lake la Mpanda Mashariki kwa kutembelea kata za Muze na Mamba ambako atafanya mikutano ya hadhara na kukabidhi kasiki ya kutunzia fedha kwa SACCOS ya Muze.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMANNE, MEI 12, 2009.
Iringa Usiseme Mbwa....

Sema ' mduadua mung'asi'- anayecheza-cheza njiani. Kitoweo hicho baba.Iringa,leo alfajiri.