HARARE, Zimbabwe
WAZIRI Mkuu wa Zimbabwe, Bw. Morgan Tsvangirai amesema kwamba Serikali ya pamoja iko hoi kifedha na haiwezi kutimiza madai ya Umoja wa muungano wa vyama vya Wafanyakazi yakutaka iwalipe viwango vya juu vya mishahara.
Bw.Tsvangirai alisema kwamba kutokana na jinsi hali ilivyo hakuna mfanyakazi yoyote wa Serikali akiwemo Rais Robert Mugabe ambaye anapata zaidi ya dola za Marekani 100 sawana pauni 67 kwa mwezi.
Kauli ya Bw. Tsvangirai imekuja kufuatia madai ya Chama cha wafanyakazi ya kuitaka Serikali kuwalipa wafanyakazi dola 450 huku kikitisha kuitisha mgomo endapo madai hayo hayatatekelezwa.
Hata hivyo wakati akihutubia sherehe za siku ya wafanyakazi mjini Harare, Bw. Tsvangirai alisema kwamba hivi sasa Serikali inahitaji muda zaidi ili kuimairisha uchumi. "Serikali hii imefilisika na hatuna uwezo wa kulipa zaidi ya dola 100 tu," Bw. Tsvangirai aliuambia umati wa watu waliodhuria sherehe hizo na akaongeza kuwa hali hii itabadilika na kuanza kulipa mishahara mizuri wakati Serikali itakapoboreka na watu wengi wakaanza kulipa kodi."Ndio kwanza tuna miezi mitatu tangu tuingie ofisini na waombeni tupeni muda," aliongeza Waziri Mkuu huyo.
Bw. Tsvangirai alisema kwamba madai ya umoja huo vyama vya wafanyakazi ni ya msingi lakini yanapaswa kuangalia hali ; ya kifedha ya Serikali na utendaji mdogo wa viwanda vya nchi hiyo.Kabla ya taarifa hiyo ya Bw. Tsvangirai, awali Bw. Lovemore Matombo ambaye ni rais wa muungano huo wa vyama vya wafanyakazi wa (ZCTU) katika salamu zake kwa wanachama wa umoja huo alisema kwamba hivi sasa wanajiandaa kuitisha mgomo wa nchi nzima ingawa hakueleza ni lini.
No comments:
Post a Comment