Wednesday, May 13, 2009

libeneke la rostam na mengi: serikali yatoa tamko
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera

SERIKALI imewataka Wafanyabiashara Rostam Aziz na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuacha mara moja malumbano kati yao na kutotumia vyombo vyao vya habari kwa maslahi yao binafsi.

Sambamba na hilo imewataka kuwasilisha vielelezo na madai yao kwa mamlaka husika ili hatua zinazofaa zichukuliwe na wananchi wapewe taarifa na vyombo hivyo.

Akitoa tamko la serikali leo mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera kwa niaba ya Waziri wake, George Mkuchika alisema serikali haitakubali kusikia malumbano hayo ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani nchini yakiendelea.

“Serikali imeyatafakari malumbano ya wafanyabiashara hawa na kubaini yanalipeleka taifa letu mahali pabaya kwani yana mwelekeo wa uvunjaji wa amani kama yataachwa kuendelea.

"…pia haitavumilia kuona vyombo vya habari nchini vikichangia kuligawa taifa katika makundi na kudumaza maendeleo”,alisema.

Badala yake amevitaka vyombo hivyo vya habari kutotomiwa kwa manufaa binafsi ya mmiliki au mtendaji; viongozwe na maadili ya taaluma na jamii husika na kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, kabila, dini, jinsia au ulemavu na kuchochea uhasama

No comments: