Friday, May 15, 2009

Homa ya nguruwe si janga la kimataifa, Asema Ban ki Moon.

NEW YORK
Margaret Chan, afisa mkuu wa Shirika la Afya duniani, W.H.O., amesema hadi sasa ni visa 1000 ambavyo vimeripotiwa kuhusiana na homa ya nguruwe katika nchi 20 duniani, na kwamba kasi ya maambukizi imepungua sana.
Naye Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon, amethibitisha kwamba shirika hilo la afya duniani halina mpango wa kuipandisha homa ya nguruwe katika daraja la sita- ambayo ndio daraja ingetambulika kama janga la kimataifa.
Ban ki moon amesema shirika hilo la afya ulimwenguni linafuatilia kwa makini jinsi homa hii inavyosambaa, lakini hawatazidisha tahadhari iliopo sasa ambayo ni daraja ya tano.
Idadi ya vifo nchini Mexico imefika watu 26, huku kifo kimoja pia kikiripotiwa katika nchi jirani ya Marekani. Nchini Mexico, mji wa Mexico City unajitayarisha kufunguliwa tena kwa mikahawa na maeneo mengine wanakokusanyika watu, baada ya serikali kutangaza kwamba hatari ya homa ya nguruwe imepita.

No comments: