Friday, May 15, 2009

Ishini Kwa Amani Asema Papa Benedict XVI.


NAZARETH
Papa Benedict wa XVI amewatolea wito waumini wa dini zote wakaazi wa ardhi takatifu kuipinga chuki na badala yake waishi kwa amani.Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo alipoongoza misa katika mji wa Nazareth ulio na waArabu wengi.
Misa hiyo iliyofanyika nje ilihudhuriwa na waumini wapatao alfu 40.Baada ya misa hiyo Papa Benedict alikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika makazi ya watawa yaliyo karibu na kanisa linaloaminika kuwa mahali ambapo Bikira Maria alipokea ujumbe wa malaika Jibril kwamba atapata ujauzito wa mwana wa Mungu.
Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni ameingia katika mkondo wa mwisho wa ziara yake ya siku nane ya eneo la Mashariki ya Kati.Kundi moja dogo la Waislamu wa Palestina limeipinga kikao hicho cha mkesha wa Naqba kumbukumbu ya siku taifa la Israel lilipoundwa.
Habari Kwa Hisani:www.dw-world.de

No comments: