Saturday, May 17, 2008

IGP Mwema atoa Tamko Rasmi..

*Wahaini wa Pemba waachiwa huru.


*Wahaini wa Pemba waachiwa huru.
Wadau Kama mlipata Taarifa leo kuwa wapemba walidai iwapo wenzao nane waliokamatwa na usalama wa Raia (jeshi la Polisi) na kuwekwa ndani kwa madai kuwa ni wahaini baada kupeleka malalamiko yao UNDP kwamba Pemba imetengwa kama wasingeachiliwa basi wapemba wote 10,000 wangejisalimisha vituo vya polisi.Hali ambayo imepelekea Mkuu wa Usalama wa Raia, (Jeshi la Polisi)Inspecta General Said Mwema Pichani (kulia)Kuamuru watu hao waliokuwa ndani kwa siku kadhaa waachiwe huru na uchunguzi wa kesi yao utaenda Taratibu kwa mujibu wa Sheria. Awali Jeshi la Polisi lilitoa tamko kwamba watuhumiwa hao hawaruhusiwi kutembelewa /ndugu zao kwakuwa kosa lao la Uhaini ni kubwa.


Akithibitisha hilo Kamishna wa Polisi Zanzibar Khamis Mohammed Simba alisema watu saba waliokuwa wamewashikilia katika vituo vya polisi kisiwani Unguja wamechiwa uhuru na kwamba watapewa usafiri wa kuwarejesha kwao Pemba.“Ni kweli leo Ijumaa tumewaachia watu saba tuliokuwa tumewakamata natunaandaa utaratibu wa kuwarejesha kwao wote,” alisema. Kamishna.Alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuwahoji na kukamilika kwa ushahidi wa awali na kuongeza kuwa iwapo kutahitajika maelezo zaidi watachukuliwa tena na kuhojiwa kwa mujibu wa sheria, kwa kuwa bado uchuguzi unaendelea.Habari hii na Mpoki Bukuku na Yahya Charahani.

No comments: