Thursday, May 22, 2008

Heshima za Mwisho zitafanyika Kanisa la Mt. Stephen Washington DC...


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Patrick Mombo, amethibitisha kifo cha gavana Balali baada ya kupata taarifa Rasmi kutoka Balozi wa Tanzania nchini Marekani Ombeni Sefue.Balozi Mombo amesema kwamba,Balozi wa Tanzani nchini Marekani Balozi Sefue alipata taarifa hizo juzi saa 4:00 usiku kwa saa za Marekani.
Hata hivyo Ikulu imekiri kupokea taarifa za kifo cha aliyekuwa gavana wa Benki Kuu (BoT), Daudi Ballali. “Rais amesikitishwa na taarifa hizo za kifo cha Ballali,tunaandaa rambirambi tutazituma baadaye,” alisema mwandishi habari msaidizi wa Rais, Premi Kibanga. Hata hivyo, Premi alisema Ikulu haiwezi kutoa taarifa za kifo hicho badala yake wenye jukumu la kufanya hivyo ni ndugu zake marehemu, “Ikulu haihusiki na kutoa taarifa tafuteni ndugu zake waseme habari za hicho kifo.”
Wakati huohuo KLH News na Gazeti la Tanzania Daima imeweza kuthibitisha kwa uhakika kuwa misa ya kumuombea Marehemu Balali inatarajiwa kufanyika saa nne asubuhi katika Kanisa la Mt. Stephen Washington DC pamoja na Kutoa heshima za mwisho kutafanyika katika kanisa hilo hilo na itakuwa si kwa hadhara nzima.Mwili wake unatarajiwa kulazwa kaburini kwenye makaburi ya "Gate of Heaven" huko huko Jamaa wa karibu wa Ballali walioko Dar es Salaam na Washington walilithibitishia Tanzania Daima kuhusu kutokea kwa msiba huo.
“Ni kweli amefariki nyumbani kwake Ijumaa usiku.Na sasa hivi tuko katika maandalizi ya kwenda funeral home (Taasisi ya kuandaa shughuli zote za mazishi) kwa ajili ya kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya msiba,” alisema ndugu wa karibu wa Ballali kutoka Washington.

No comments: