Thursday, May 22, 2008

Daudi Balali Afariki Dunia..


Aliyekuwa gavana mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Timoth S. Ballali amefariki.
Kwa habari zenye uhakika toka kwa ndugu wa karibu na mkewe,Mama Anna Muganda zinatonya kuwa amefariki Tarehe 16.05.2008 huko BOSTON, USA na anatarajiwa Kuzikwa ijumaa Boston Nchini Marekani.
------------
Nyadhifa Alizoshika Enzi ya
Uhai Wake..
-Mwaka 1967-1976 alikuwa mtumishi katika Benki kuu ya Tanzania alishika nyadhifa mbalimbali.
-Mwaka 1979 -1984 alifanya kazi nchini nGhana akiwa kama mtumishi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kama mchumi.
-Mwaka 1984-1986 akiwa IMF alihamishiwa Zimbabwe katika nafasi hiyo ya mchumi.
- 1986-1997 aliongoza Timu ya IMF kwa ajili ya majadiliano na usimamizi wa sera ya mageuzi ya uchumi.
-1997-1998 aliteuliwa kuwa mshauri wa Rais wa mambo ya uchumi. na
Mwaka 1998 aliteuliwa Rasmi kuwa Gavana wa BoT,wadhifa aliodumu nao hadi Januari 2008.Kabla ya Rais Kikwete Kutengua uteuzi Bw Balali Mwezi January 2008.
Hat Hivyo wakati akiwa Gavana IMF ilimteua tena mwaka 2006-2008 kuwa mjumbe wa bodi ya Magavana akitokea Tanzania. Na mwaka 2006 alikuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato (TRA).

No comments: