Friday, May 23, 2008

Lady Jaydee kutumbuiza B'day ya Mandela...



Msanii Judith Wambura 'Lady Jay Dee' ni miongoni mwa wanaotarajiwa kutumbuiza katika tamasha la kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ‘Madiba’ litakalofanyika Juni 27, London,Uingereza.

Mkurugenzi wa Masoko wa Celtel, Margaret Kositany alisema jana kuwa Lady Jay Dee atatumbuiza pamoja na wasanii wengine wa Afrika wakiwamo Papa Wemba kutoka DRC Kongo na Susana Owiyo kutoka Kenya.

Pichani juu ni Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuchaguliwa kwake katika sherehe maalum za Rais Mstaafu wa Afrika Kusini,Nelson Mandela zinazotarajiwa kufanyika London Uingereza hivi karibuni.Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Celtel Tanzania,Margaret Kasitany

No comments: