Tuesday, May 13, 2008
Ufisadi umetuweka pagumu - Pinda ...
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na wahariri wa vyombo mbalimbali
vya habari nchini.
----
"Kwa kweli hapa mlipotufikisha mhh!!! ni pagumu sana,mnatufanya tufanye mambo kwa uangalifu sana" Pinda
--------
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kwamba kuibuliwa kwa masuala ya rushwa kwa viongozi wa serikali kulikofanywa na vyombo vya habari,kumeiweka serikali mahali pagumu, na kwamba sasa watendaji wake inabidi wawe makini zaidi.
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Dar es Salaam leo,Waziri Mkuu alisema kuibuliwa kwa masuala hayo ya rushwa kwa viongozi na kulazimisha wengine kujiuzulu, ni changamoto kubwa na sasa inabidi mawaziri wawe makini na waangalifu zaidi.
“Hapa mlipotufikisha sasa ni pagumu,” alisema Pinda na kuongeza kuwa ingawa masuala mengi ya vitendo vya rushwa yalifanyika katika awamu zilizopita,lakini ni changamoto kwa serikali ya sasa kujitahidi kuhakikisha haiangukii katika mtego wa wengine kutuhumiwa kushiriki vitendo hivyo.
“Hii imetufanya tuwe makini zaidi, (wanahabari) mmesukuma sana mambo. Mmefanya kazi nzuri na mnapaswa kuendelea kufanya kazi hiyo na ni juu yetu sisi kuhakikisha hatuingii katika mtego.Awamu hii inatakiwa tuwe waadilifu sana,ili hata kama itakapomalizika miaka mitatu minne, isije ikasemwa tena Mzee Pinda nawe ulichukua,” alisema Waziri Mkuu.Habari hii na Mgaya Kingoba wa Habari Leo.Picha na Bernard Rwebangira.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment