Monday, May 12, 2008
Rais Kikwete abadili Mawaziri...
Pichani ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari Ikulu,
Bw Salva Rweyemamu.
-------------
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko madogo ya Baraza La Mawaziri kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Mheshimiwa Andrew Chenge hivi karibuni. Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam jana, Rais amemteua Mheshimiwa Dk. Shukuru J. Kawambwa kuwa Waziri mpya wa Miundombinu.
Mheshimiwa Kawambwa anatokea Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Peter M. Msolla ambaye alikuwa anashikilia wizara hiyo ya Mawasiliano sasa anakuwa Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Mhe. Celina O. Kombani ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.
Mheshimiwa Celina Kombani alikuwa ni Naibu Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI. Aidha, Mhe. Stephen M. Wassira ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Mheshimiwa Wassira anatokea Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.
Katika mabadiliko hayo, Rais pia amewagusa naibu mawaziri ambapo amemteua Mhe. Aggrey Mwandri, Mbunge wa SIHA kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI. Naye Mheshimiwa Ezekia Chibulunje anahama kutoka Wizara ya Kazi na kwenda Wizara ya Miundombinu, wakati Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana inashikwa na Mhe. Dk. Milton M. Mahanga. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu, mawaziri hao wataapishwa leo Ikulu, Jijini Dar es Salaam, saa tatu asubuhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment