ali kiba akiwa njiani kuelekea wichita




Alikiba anapenda kuwashukuru wale wote waliojitokeza kwa mamia kumsupport Washington d.c na Minnesota, Anawahaidi wakazi wote wa kansas kujitokeza kwa wingi kwa sababu amepania kuwasuuza roho zao na show kabambe.
Usingoje kuhadithiwa hakikisha unajionea mwenyewe kipaji cha mwanamuziki wetu kutoka nyumbani.
Wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini kijana huyu anapendwa hivi kila pembe ya dunia. Jibu ni rahisi sana. Ukiwachilia mbali kipaji na uwezo wake mkubwa wa kutawala jukwaa, nje ya jukwaa hana nyodo, halewi wala havuti na pia hufika kazini katika muda aliopangiwa na akianza amenza, tofauti na wasanii wengi wengine wa kibongo ambao hujisahau kwa kujiona wao ni wao.
No comments:
Post a Comment