Wednesday, September 17, 2008

muhimbili kunani hapo wajameni ???!


Haya maneno hapa chini nimeyachukua katika blogu ya drfaustine (http://drfaustine.blogspot.com/). Natambua daktari anajua nini anachoandika na yuko serious katika ishu nyingi hasa zinazogusa maisha ya watu na haya ndiyo aliyoandika katika blogu yake. Something shoud be done, lakini sijui nani anatakiwa kufanya hili.

Wakati mwingine unabaki ukishangaa. Hebu isomeni .Lukwangule Katika pita pita yangu katika Blogu ya Bw Beda Msimbe nimekutana na stori ya kusikitisha na kufedhehesha inayohusu kukosekana kwa huduma ya muhimu ya CT scan.Kwa taarifa zilizopo ni kuwa mashine ya Muhimbili na ile ya Aga Khan zote hazifanyi kazi.

Kwa muda mrefu CT Scan ya Muhimbili imekuwa Spana mkononi.Huduma hii inazalisha fedha nyingi sana. Kipimo si chini ya Tsh 100,000. Fedha hizi zinazotokana na mashine hii zinakwenda wapi?Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa hakuna fungu maalum lililopo kwa ajili ya matengenezo ya mashine hii. Pia mashine hii haina service warranty.

Hivyo mashine ikiharibika inaweza kuchukua kipindi kirefu kabla ya kutengenezwa.Haijulikani ni idadi gani ya wanaopoteza maisha kutokana na kukosekana kwa huduma nyeti kama hii na ile ya kusafisha figo (renal dialysis).Siku za nyuma nimepiga kelele sana kuhusu suala la renal dialysis. Wataalam tunao, wafadhili wako tayari kutoa vifaa hivi muhimu, Muhimbili wanajivuta kutoa chumba cha kufunga vifaa hivi!

Swali la kujiuliza ni wagonjwa wangapi wenye ndugu wenye uwezo wa kupeleka wagonjwa wao Nairobi na Johannesburg? Hivi hatuoni fedheha miaka 47 ya uhuru bado tunakosa huduma muhimu kama hizi katika hospitali zetu za rufaa?CT scan sio kipimo cha anasa, ni kipimo cha msingi katika hospitali za rufaa.

Mgonjwa kama Bw Athuman Hamisi anakosa kupata matibabu ya msingi kutokana na madaktari kutojua majeraha katika uti wa mgongo yako wapi, kipimo hiki kingesaidia kujua tatizo liko wapi na kuweza kupata tiba stahili.Watanzania tunaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu.NB: Nampa pole mdau Athumani Hamisi. Mungu amjalie apone haraka.

Ujumbe huu nimeuchukua kama ulivyo kutoka kwa http://lukwangule.blogspot.com/

No comments: