Tuesday, September 23, 2008

athumani hamisi kutibiwa india


mpiganaji Athumani Hamisi ambaye alipata ajali ya gari huko Kibiti siku kadhaa zilizopita atapelekwa hospitali ya Apollo huko New Delhi, India, kwa matibabu zaidi ya mgongo na shingo ambavyo viliathirika na ajali hiyo.

Athumani alikuwa akienda Kibiti kikazi akiwa na waandishi wenzake wawili ndani ya gari lake mwenyewe.

Athumani ambaye ni mhariri wa dawati la picha katika magazeti ya Habarileo na HabariLeo Jumapili na majalida yake anaweza kuondoka wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilika kwa taratibu zinaozohusu safari ya mgonjwa wa aina yake nchi za nje.

Hadi sasa kinachotafutwa ni usafiri wa ndege ya moja kwa moja hadi jijini New Delhi ili mgonjwa asiathirike zaidi endapo kama atasafiri kwa ndege za kuunganisha ambapo itabidi awe anahamishwahamishwa.

No comments: