Tuesday, September 16, 2008

kibaka aonja joto ya jiwe



Cheki jamaa walivyokuwa wakimtamani wamshushie kipondo, hawaogopi suala la kujichukuria sheria mkononi ambalo linapigwa vikali na serikali

Baada ya kipondo cha kiasi,akatulia tuliii huku akisikilizia maumivu


Pamojana kuokolewa na polisi jamaa bado walikuwa na hamu nae kweli kibaka huyo,ona walivyokuwa wakimfuata hadi kwenye STG tena bila woga



Mara STG ya polisi ikapita sehemu ya tukio,ikabidi wasimame na kutoa msaada wa kumtoa mikononi mwa watu waliokuwa na hasira ya kumshushia kisago kibaka huyo,hapa ndio ilikuwa nafuu yake baada ya polisi kufika




Mlinzi wa watu alijaribu kumtetea sana kibaka huyo asipewe kipondo sana kwani tayari lundo la watu lilikuwa limeishajongea kumpa kisago.Wakati huo polisi badoa hawajatia timu kumuoko huyo kibaka





Si wakaanza kuongezeka mmoja baada ya mwingine, na kama ujuavyo mambo ya kati kati ya jiji wengi wao wamechoshwa na hawa vibaka wa kila siku mjini






Mara akatokea mwenye gari yake ilioibiwa hiyo saiti mila,ebwana jamaa alitoka mbogo wacha amuangushie kipondo cha nguvu







" Unampeleka wapi huko,mpeleke hukuu"






Kijana mmoja ambaye hakutambulika jina lake kwa urahisi leo jioni ameonja joto ya jiwe na wananchi wenye hasira kali na kumpa kipigo baada ya kumnasa akiiba saiti mila ya gari na mlinzi pichani nje ya jengo la benki ya watani wetu wa jadi (Kenya komesho benki)

No comments: