Yanga yalambwa 1-0..

-------
Miamba wa Tanzania,Simba na Yanga watakutana katika mchezo wa kuwania dola za Marekani 10,000(zaidi ya Sh milioni 12)za mshindi wa tatu katika michuano ya Kombe la Kagame kesho. Miamba hao wa Tanzania watakutana katika mchezo huo ambao utakuwa wa utangulizi kabla ya fainali ambayo itaikutanisha URA ya Uganda na Tusker ya Kenya.Mshindi wa kwanza wa michuano hiyo atapata dola za Marekani 30,000(zaidi ya Sh milioni 34)mshindi wa pili dola 20,000(zaidi ya Sh milioni 23).Habari na Emmanuel Mrema/Picha Bernard Rwebangira
No comments:
Post a Comment